Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,193
- 25,500
Jana, kwenye mabandiko tofauti humu JF, niliyaponda na kutamani mapingamizi yote yaliyowasilishwa dhidi ya wagombea wa Ubunge wa Kinondoni yatupiliwe mbali. Lengo langu halikuwa kukiuka sheria,lilikuwa ni kutaka uchaguzi uendelee kama ulivyopangwa. Busara iongoze!
Wapo walionishambulia na kunipinga bila ya kufikiri mara mbili. Wapo pia walionipongeza na kupenda msimamo wangu. Nilisema, mapingamizi yote hayana msingi na yanapaswa kutupiliwa mbali. Nikasema pia kuwa wakati mwingine mapingamizi huwanyima wananchi viongozi bora.
Nimefurahishwa na uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni wa kuyatupilia mbali mapingamizi yote dhidi ya wagombea wa CCM,CHADEMA na SAU. Sasa, wagombea wote wanabaki na uchaguzi utafanyika vyema.
Kila la heri wana Kinondoni!