Uchaguzi wa kesho Unaweza kuwa mwanzo wa Kusambaratika CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi wa kesho Unaweza kuwa mwanzo wa Kusambaratika CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Oct 1, 2011.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ukiangalia mambo critically, kuna watu ndani ya CCM wangependa CCM ishindwe Igunga ili wawashe moto kuwashutumu akina NAPE kwa kukisambaratisha chama kwa hoja yao ya kujivua gamba. natabiri ikiwa CCM ikianguka kesho ndio utakuwa mwisho wa umoja ndani ya chama. Makundi yatajitokeza hadharani na kushutumiana kuhusu kudhoofisha chama kwa hija za kujivua gamba. Mwisho chama kitagawanyika kabla ya uchaguzi wa mwaka kesho. natamani hiyo itokee
   
 2. i

  ibange JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ukitaka kuyaamini maneno yangu, soma gazeti la RAI la juzi uangalie lilivyoiponda CCM kuanzia mwanzo hadi mwisho. Gazeti hili mara zote limekuwa mdomo wa kundi la Lowassa.
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Oct 1, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Deo Balile (wa Rai) amemshambulia Mukama na Chama Chake. Kumbe Mukama ndiye aliyekuja na falsafa ya kujivua gamba baada ya kujifungia chumbani na Prof gani sijui na kutoa ushauri kwa CCM jinsi ya kurudisha mvuto kwa wananchi!! CCM ina mpasuko mkubwa na kwa hakika vimelea vya CCJ vipo tena vina nguvu.
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kimbunga mambo mengi unayo yaona yanaikaba koo CCM mpishi mkuu ni Mukama na genge lake.Ndiyo maana akapewa ukatibu mkuu .Ssaa kesha kalia kitu jamaa alimwahidi ushirikiano lakini kila akigusa JK anaona moto mkali so Mukama kabakia kama Nape wote wana elea tu .Msekwa yeye anawaza kuuza vitalu vyetu huko mbugani .JK na mikutano ya DIKOTA .
   
 5. O

  Omr JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM ikishindwa tutasema kuwa Tanzania kuna demokrasi na itaonekana kuwa Kikwete alishinda kwa haki kwenye uchaguzi ulio pita. Hapo ndio ulimwengu utawaona Kina Slaa ni wanafiki.
  CCM ikishinda basi kuna mawili, CDM kufa au CDM kuonekana kuwa chama cha msimu. Na ukweli ni kuwa hakuna fujo itakayo tokea.
   
 6. BABA JUNJO

  BABA JUNJO JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Adui yako mwombee njaa usimwombee balaa kama hilo watatoka wenyewe baada ya kuona maji shingo hawawezi ogelea
   
 7. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pro erginald mihanjo wa chuo cha st john cha dodoma.
   
 8. only83

  only83 JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Simple analysis,but very true...
   
 9. iron finger

  iron finger JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakuu miaka yote tumeishi kwa ndoto tunasubiri ccm ife lakini hamna kitu,migogoro ndani ya chama haijaanza leo lakini mara zote kipo imara tu,me nafikiri umefika muda tuache kuishi kwa ndoto tuimarishe chama letu la wachaga kusubiri ccm ife ni tamaa za fisi na mkono wa binadamu,na kuthibitisha upinzani tanzania ni dhaifu
   
 10. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  1. Naamini kabisa kuna wana-Magamba wanaombea kesho CHADEMA ISHINDE kwa hali na mali ili hii SERA FAKE YA KUJIVUA GAMBA IDHIBITIKE KUWA NI MOJAWAPO YA SIASA UCHWARA ZA CCM.
  2. Naamini kuna Viongozi waandamizi wa CCM hawakukanyaga Igunga kabisa na wengine wameenda huko kwa KULAZIMISHWA!RA ni mojawapo ya wana-Magamba anayesubiri ANGUKO LA CCM kesho kwa shauku kubwa.
  3. Naamini kuna wanachama wa CDM na Watz wapenda HAKI,AMANI,UPENDO na DEMOKRASIA YA KWELI ambao usiku wa leo wataomba kwa Mungu ili Mungu abatilishe mipango yote miovu ya CCM na hatimaye CHADEMA kiweze kuchukua kiti cha Igunga.
  Tusubiri matokeo baada ya dk.90.
   
 11. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Naitakia chadema kila la kheri.
   
Loading...