Uchaguzi wa Kesho Kinondoni na Siha: Wito kwa Chadema na CCM, Tukubali Matokeo!. Asiyekubali Kushindwa Sii Mshindani

Pale mnapojiandaa kisaikolojia na kuwaandaa watu wenu.
Poleni sana kwa maana dalili nyingi zinaonyesha mnaenda kupoteza jimbo lenu. Na hiyo ni dalili kuwa "MJIREKEBISHE"
Uchaguzi wa kata 43 ulistaajabisha wengi sasa ni uchaguzi wa majimbo mawili.
Kwa wale wengine (ccm) ambao walipoteza majimbo awali kwa ujinga wao, nadhani kuna kitu wamejifunza.
 
Utaratibu wa kujiunga na CCM unafahamika, utaratibu wa mtu kugombea ubunge ndani ya CCM, unafahamika ni mchakato fulani. Sasa mtu anajiunga leo CCM, kesho anateuliwa mgombea bila utaratibu na mchakato kufuatwa. Huu ni uthibitisho wa rushes ya ahadi, kisheria inaitwa "promissory estoppel" ambayo ni ushahidi usiotia shaka mtu alihongwa ahadi ya kusimamishwa yeye kama atanitoa!. Ndicho kilichofanyika Kinondoni na Siha, na kitaendelea!. Rushwa sio lazima iwe ni pesa tuu!, hata ahadi ya uteuzi ni rushwa!, halafu hili lidudu li PCCB lipo tuu, na mijitu imejazana ofisini inakula tuu kiyoyozi, eti tunapiga vita rushwa!.
Uko sahihi kabisa !!!!!!
 
Chadema malalamiko mengi, na kukata tamaa, hizo ni dalili za kushidwa mapema, hata kabla ya Uchaguzi kuanza.
jipangeni kwa 2025 , kwa sasa bado sana.
 
Paskali, you have missed the point. Kuna mtu alisema hivi " Gari nikupe mimi,mashahara nikulipe mimi,halafu umtangaze mpinzani ameshinda?huna kazi kuanzia siku hiyo" nukuu rais Magufuli
Nini kifanyke CDM kulinda haki yake? Wataweza mbele ya polisi, mabomu, utekeji unaofanywa na dola, mauaji yanayofanywa na dola etc? Unwashauri nini , wafanye nini kupata haki yao?
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya aomba radhi kwa Rais Magufuli baada CCM kushindwa kata ya Ibighi! Akana baada ya kuhojiwa
Aisee kazi kweli kweli kwa upinzani ,
UPINZANI V/S CCM, NEC,JESHI LA POLISI ,RC, DC NA WAKURUNGEZI.
 
Sikiliza Pascal, nguvu za dola ambazo CCM inazitumia ili kushinda chaguzi hizi za marudio, hawataweza kuzideploy kwa nchi nzima wakati wa uchaguzi mkuu, ndipo nguvu na hasira za wananchi zitakapoanza kuonekana! Mark my words.
 
loser always think only a weak part and not strength part that's why they never win. there is always a benefit of losing; you learn from your mistake.
CHADEMA never took time to learn from their weakness that's why they spend time on blaming than on creativity and innovative side. my advice to all is that:- the role of war is to learn from your enemy in order to win
 
CHADEMA never took time to learn from their weakness that's why they spend time on blaming than on creativity and innovative side. my advice to all is that:- the role of war is to learn from your enemy in order to win
you need muster mind in order to win and not opportunist. there is a different between muster mind and opportunist. muster mind is after achieving objective but opportunist is after profit. that's my take
 
Wewe unaumizwa na matusi yangu ambayo hayakuachii kovu lolote lile mwilini, lakini wakati huo huo unashindwa kukemea mauaji yanayoendelea nchini watu wanapoteza wapendwa wao kutokana na huyu dikteta uchwara. Siku ukipigwa panga la uso au rungu la kichwa kuhusiana na hizi vurugu za uchaguzi uchwara ndiyo utatia akili kichwani na kujua hizi vurugu ni kama mtego wa panya wataingia waliokuwemo na wasiokuwemo. Angalia yaliyotokea Rwanda, Burundi, Misri na sasa yanashamiri tartatibu nchini kwetu lakini mpuuzi wewe uko kimya unalalama kuhusu matusi tena wala si ya nguoni. Ukiandika upuuzi hapa siwezi kukuita genius. Tia akili kichwani simama kutetea maslahi ya nchi yako na wananchi wenzio dhidi ya dhuluma na udhalimu mkubwa unaozidi kuota mizizi nchini.

Kwanza kwa mkongwe kama wewe kuchangia kwa matusi unashangaza sana. Pili kusema haya uliyotaja kwenye uchaguzi wa Kinondoni kuwa ni exceptional unazidi kushangaza. Kuhusu waraka wa maaskofu nafikiri nikuache tu .....
 
Paskali umesahau Bw Pole Pole aliosema juu ya uchaguzi wa Kinondoni na huko Siha hayana tofauti na ya Comrade Stalin japo ni enzi tofauti lakini the mission is the same.

"It is enough that the people know there was an election. The people who cast the votes decide nothing. The people who count the votes decide everything.''by Josef Stalin

Haitakiwi kutumia akili ya ziada kujua uchaguzi utafanyika lakini nani ameteuliwa iwe ashinde au asishinde anajulikana nae ni yule yule wa siku zote lakini safari hii anagombea kwa tiketi ya wenye nazo.
 
Naona mikakati yote ya wizi imekwishakamilika kinachosubiriwa ni utekelezaji tu.

Hizi by elections ni kuharibu tu pesa za walipa kodi kwani wa kushinda tayari anakuwa ameshapangwa, hakuna uchaguzi hapo.!
 
Kuna mgombea mmoja Yuko hoi kiafya......Jana hakuhutubia aliishia kusalimia na kupunga mkono!
Leo ktk kufunga Mkutano wake akizungumza Sijui......

Ova
 
Back
Top Bottom