Uchaguzi wa Kanda 2019: Sumaye kupigiwa kura ya hapana

KAMWENE NYELA

New Member
Nov 26, 2019
4
2
Asalaam wakuu,

Waziri mkuu mstaafu bwana Fredric Sumaye ambaye ni mjumbe wa kamati kuu na Mwenyekiti wa kanda ya Pwani anayemaliza muda wake huenda akapigiwa kura ya hapana katika kinyanganyiro cha nafasi hiyo katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 28/11/19 wiki hii.

Sumaye ambaye alijijengea heshima ya pekee baada ya kuhamia chadema mwaka 2015 akiwa hana nia ya kushika nafasi yoyote ndani ya chama hicho kikuu cha upinzania nchini Tanzania ameandamwa na kashfa nzito ya kushirikiana na Serikali ya Tanzania na Vyombo vyake vya ulinzi hasa hasa TISS kukihujumu chadema katika uchaguzi huu mkuu ndani ya chama hicho.

Taarifa zisizo rasmi kutoka katika viunga vya mitaa ya ufipa kinondoni na Magomeni yalipo makao makuu ya kanda ya Pwani ni kwamba bwana sumaye ameamua kuchukua fomu ya nafasi ya uenyekiti wa chadema Taifa kimyakimya katika ofisi hiyo ya kanda. Kuchukua kwa Sumaye fomu hiyo kimya kunatokana na ukweli kwamba wanachadema wengi wasingependa Mh Freeman Mbowe aachie ngazi licha ya ushindani kiduchu atakao upata kutoka kwa mgombea mwingine katika nafasi hiyo kubwa zaidi ndani ya chama hicho.

Aidha taarifa kwamba mh. Sumaye yupo katika kundi la mh. Mwambe ndizo zinazochagiza na kuleta sintofahamu ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani. Mwambe bado hajajipambanua kwamba ni mwanachadema halisi licha ya kushikilia nafasi nyeti ikiwemo ya ujumbe wa kamati kuu kwa kipindi cha miaka mitatu sasa.

Kundi la Mwambe linajumuisha makamanda waaminifu kabisa na wa muda mrefu wa chadema. Inasadikika kwamba zaidi ya makatibu tisa (9) wa kanda wanamuunga mkono Mwambe. Miongoni mwao ni Kizota wa kanda ya kati, Mabina wa kanda ya Pwani, Katibu wa kanda ya Serengeti na yule wa kanda ya Victoria. Wapo pia wagombea wa nafasi mbali mbali ndani ya mabaraza ya chama.

Katika baraza la vijana, Hemedi Ally, Edward Simbeye na Gwamaka Mbughi ambao ni wagombea wa nafasi ya ukatibu Mkuu wanatajwa kumuunga mkono mh.Mwambe. Wapo pia Pambalu na Mhere Mwita kwa nafasi ya Uenyekiti wa Baraza la vijana. Gwamaka Mbughi anasemwa kama ndiyo turufu kubwa zaidi ya mh. Mwambe na Sumaye kuingiza watu wake katika Sekretariet ya kamati kuu endapo atafanikiwa kuukwaa ukatibu mkuu wa baraza la vijana.

Aidha wanatajwa Mh. Selasini na Malilo kama wagombea kwa nafasi za uenyekiti wa kanda. Taarifa hizi ambazo hazijawa njema kwa upande wa wapigania mabadiliko zinawafanya wapigane kufa na kupona kuhakikisha kwamba mh.Sumaye hapati nafasi yoyote ndani ya Chama katika uchaguzi huu mkuu wa ndani ya Chama.
 
nani atakuwa mwenyekiti Wa muda kwenye kikao cha kumpata mwenyekiti mpya kama Mbowe atashiriki? Huyo ndio atatenda haki kwa wote bila huyo kujulika Mbowe atakuwa mwenyekiti Wa maisha
 
Mmeanza kumwaga sumu. Nina shaka kama nakutakia mema chama hicho. Mtu kutembea sio dhambi. Mtu kutofautiana kimtazamo na baadhi ya wanachama wenzake sio dhambi. Kukosoa viongozi sio dhambi. Lakini huku kumwaga sumu ni dhambi na sio kujenga chama. Hasa kwa sababu inaelekea umefunga kwa ajili ya kazi hii tu. Inasikitisha sana.

Amandla......
 
tunakwenda kuipima demokrasia ya chadema, tofauti na CCM ambayo mwenyekiti hapingwi.
 
Mmeitisha uchaguzi ili iweje? Fomu zimetolewa ili iweje?

Wasiotaka mabadiriko wanaongozwa kifalme au kisultani, na nyinyi kama mnaamini hakuna MTU zaidi ya Mbowe badilisheni katiba yenu ili muntangaze Mbowe kuwa mwenyekiti wa màisha, shida iko wapi?
 
Mungu ibariki Chadema
 
Asalaam wakuu,

Waziri mkuu mstaafu bwana Fredric Sumaye ambaye ni mjumbe wa kamati kuu na Mwenyekiti wa kanda ya Pwani anayemaliza muda wake huenda akapigiwa kura ya hapana katika kinyanganyiro cha nafasi hiyo katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 28/11/19 wiki hii.

Sumaye ambaye alijijengea heshima ya pekee baada ya kuhamia chadema mwaka 2015 akiwa hana nia ya kushika nafasi yoyote ndani ya chama hicho kikuu cha upinzania nchini Tanzania ameandamwa na kashfa nzito ya kushirikiana na Serikali ya Tanzania na Vyombo vyake vya ulinzi hasa hasa TISS kukihujumu chadema katika uchaguzi huu mkuu ndani ya chama hicho.

Taarifa zisizo rasmi kutoka katika viunga vya mitaa ya ufipa kinondoni na Magomeni yalipo makao makuu ya kanda ya Pwani ni kwamba bwana sumaye ameamua kuchukua fomu ya nafasi ya uenyekiti wa chadema Taifa kimyakimya katika ofisi hiyo ya kanda. Kuchukua kwa Sumaye fomu hiyo kimya kunatokana na ukweli kwamba wanachadema wengi wasingependa Mh Freeman Mbowe aachie ngazi licha ya ushindani kiduchu atakao upata kutoka kwa mgombea mwingine katika nafasi hiyo kubwa zaidi ndani ya chama hicho.

Aidha taarifa kwamba mh. Sumaye yupo katika kundi la mh. Mwambe ndizo zinazochagiza na kuleta sintofahamu ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani. Mwambe bado hajajipambanua kwamba ni mwanachadema halisi licha ya kushikilia nafasi nyeti ikiwemo ya ujumbe wa kamati kuu kwa kipindi cha miaka mitatu sasa.

Kundi la Mwambe linajumuisha makamanda waaminifu kabisa na wa muda mrefu wa chadema. Inasadikika kwamba zaidi ya makatibu tisa (9) wa kanda wanamuunga mkono Mwambe. Miongoni mwao ni Kizota wa kanda ya kati, Mabina wa kanda ya Pwani, Katibu wa kanda ya Serengeti na yule wa kanda ya Victoria. Wapo pia wagombea wa nafasi mbali mbali ndani ya mabaraza ya chama.

Katika baraza la vijana, Hemedi Ally, Edward Simbeye na Gwamaka Mbughi ambao ni wagombea wa nafasi ya ukatibu Mkuu wanatajwa kumuunga mkono mh.Mwambe. Wapo pia Pambalu na Mhere Mwita kwa nafasi ya Uenyekiti wa Baraza la vijana. Gwamaka Mbughi anasemwa kama ndiyo turufu kubwa zaidi ya mh. Mwambe na Sumaye kuingiza watu wake katika Sekretariet ya kamati kuu endapo atafanikiwa kuukwaa ukatibu mkuu wa baraza la vijana.

Aidha wanatajwa Mh. Selasini na Malilo kama wagombea kwa nafasi za uenyekiti wa kanda. Taarifa hizi ambazo hazijawa njema kwa upande wa wapigania mabadiliko zinawafanya wapigane kufa na kupona kuhakikisha kwamba mh.Sumaye hapati nafasi yoyote ndani ya Chama katika uchaguzi huu mkuu wa ndani ya Chama.
😆😆😆😆😆
 
Back
Top Bottom