Uchaguzi wa Igunga ni ushindi wa vita vya ufisadi

Pius Kafefa

Member
Aug 9, 2011
88
20
Wote tuliokuwa tunafuatilia vita dhidi ya ufisadi tunafahamu hatua kwa hatua tangu kutangazwa kwa ile 'list of shame' hadi kujing'atua kwa Rostam na hatimaye uchaguzi mdogo jimbo la Igunga. Kwangu mimi uchaguzi huu umeonyesha gharama halisi za kuwang'oa mafisadi. Nazo ni jumla ya fedha zote zilizotolewa kugharimia uchaguzi wa Igunga, madhara yote ya kimwili na kisaikolojia waliyopata baadhi ya watu wakati wa mchakato wa uchaguzi, na mwisho ni hofu mpya ya kushindwa kwa baadhi vyama vilivyoshiriki uchaguzi huu kwa chaguzi zijazo.

Tumejifunza nini?
Ni kwamba gharama ya vita dhidi ya ufisadi ni ndogo sana, kumng'oa fisadi mmoja inahitaji shilingi zisizozidi bilioni 5. Ni fedha kidogo sana. Kumbe tukihitaji kung'oa mafisadi wachache waliobaki halafu nchi ikapata mwelekeo ni busara kuingia gharama kidogo kama tulivyofanya Igunga. Naomba vita dhidi ya ufisadi viendelezwe na watanzania wote bila kujali itikadi zao. Tumeanza vizuri kwa kumuondoa mmoja, tuendelee kwa waliobaki.

"To every problem there is always a solution if you tackle it ACTIVELY, but not if you approach the same problem PASSIVELY".
 
Pius hata wakisema tuchange ili bil 5 zipatikane raia tuko tayari maana huo ufisadi unaboa na unakera sana, dodoma pakavu sana alafu kila kipindi cha bunge tunatimuliwa vumbi tu na magari ya mafisadi huku hospitali ya mkoa haitoi huduma bora yani ni ovyo kabisa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom