Uchaguzi wa Igunga haukuwa huru na wa haki! - Freeman Mbowe

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,440
113,449
Kwa wenye access na Channel Ten, watch kipindi cha Channel Ten on Monday Live!, Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe yuko hewani...

Mwenyekiti Mbowe amesema uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki, ndio sababu ya msingi ya mgombea wa Chadema kususia kusaini ile karatasi ya matokeo na hivyo Chadema kitakwenda mahakamani kuyapinga matokeo hayo.

Mhe. Mbowe amesema, uchaguzi huo umeendeshwa na Tume isiyo huru ya Uchaguzi ambayo imekiuka kwa makusudi baadhi ya sheria, taratibu na kanuni kulikowaondolea haki ya kupiga kura, watu wengi wenye haki hiyo.

Pia serikali, imekiuka sheria, taratibu na kanuni, kwa kuingia Igunga kama serikali, wakati serikali haukupaswa kujiingiza kwenye direct campaingn za CCM.

Mbowe amesema, Chadema itakwenda mahakamani sio kwa lengo la kutaka matokeo ya Igunga yabatilishwe, bali inakwenda mahakamani ili mahakama kama chumbo huru, kihakikishe haki inatendeka kwa kuimuru Tume ya Uchaguzi itende haki na kupress kupatikana kwa Tume huru ya uchaguzi ili kuweka presedence kwa chaguzi nyingine zitakazofuatia.

Mbowe ameshamaliza kuhojiwa na sasa ni wachangiaji wakichangia kuu iitwayo "Uchaguzi wa Igunga, Tumejifunza Nini?.
 
Mkuu mbona mimi namuona marcus albany ndio yuko hewani live.

Unaweza kutupatia kwa muhtasari alizungumza nini.
 
Tusio na acces tufanyeje? tuwekeee tips ya anachozungumza chairman tafadhali ili twende sawa, lazima ni mambo ya msingi and tangible anayoongea
 
Kwa wenye access na Channel Ten, watch kipindi cha Channel Ten on Monday Live!, Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe yuko hewani...

Mwenyekiti Mbowe amesema uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki, ndio sababu ya msingi ya mgombea wa Chadema kususia kusaini ile karatasi ya matokeo na hivyo Chadema kitakwenda mahakamani kuyapinga matokeo hayo.

Good move, hata kama wanamiliki pasipo halali mahakama na polisi,we go for records and good references. Pipoz power watakapo sema sasa basi,nakuingia mtaani, itakuwa basi na CCM na dola yake .....The hague.
 
wamefukuzwa studio. 4 minutes to time. jamaa anawapasua ccm, naona magamba yamekosa uvumilivu. ngoja tuone show inayofuata maana kuwafukuza watu studio ni kama vile kifuatacho kina mashiko zaidi.
 
Sasa kama hapingi matokeo mahakamani anaenda fanya nini,je mahakama ndo inateua tume ya uchaguzi?sijaelewa kidogo hapo.
 
mbowe na kelele za mfa maji, nimemsikia anabwabwaja kama mtu aliyechanganyikiwa, wamepoteza pesa nyingi na jimbo wamelikosa.

Vipi mbona unaingia msikitini na viatu!!!,changia vitu vya maana acha ushabiki maandazi
 
Chaguzi za nchi hii zitakuwa halali pale Tume itakapokuwa huru.
 
mbowe na kelele za mfa maji, nimemsikia anabwabwaja kama mtu aliyechanganyikiwa, wamepoteza pesa nyingi na jimbo wamelikosa.

mfamaji ni wewe mtatiro uliyepata kura elf 2.Huna hata haya kuchangia hapa wewe CCM B
 
Hivi nani hakuona au kusikia au kusoma ukiukwaji mkubwa uliofanyika? Tuweke uzalendo mbele jamani inatia uchungu kuona watz badala ya kujenga hoja watu wanaponda! Tujibu hoja kwa kutoa hoja.
 
Sasa kama hapingi matokeo mahakamani anaenda fanya nini,je mahakama ndo inateua tume ya uchaguzi?sijaelewa kidogo hapo.
Mapu', lengo la kwenda mahakamani sio tuu kuililia Igunga ambapo Chadema imepokwa ushindi wa haki, bali mahakama ihakikishe haki inatendeka katika chaguzi nyingine zijazo.

Mbowe amesema, Chadema itakwenda mahakamani sio kwa lengo la kutaka matokeo ya Igunga yabatilishwe, bali inakwenda mahakamani ili mahakama kama chumbo huru, kihakikishe haki inatendeka kwa kuimuru Tume ya Uchaguzi itende haki na kupress kupatikana kwa Tume huru ya uchaguzi ili kuweka presedence kwa chaguzi nyingine zitakazofuatia
 
mbowe na kelele za mfa maji, nimemsikia anabwabwaja kama mtu aliyechanganyikiwa, wamepoteza pesa nyingi na jimbo wamelikosa.
Naona CUF wameshinda uchaguzi kwa kura 2000 halafu hawakutumia pesa yeyote kwenye kampeni, Chadema tu ndio waliotumia pesa
 
Back
Top Bottom