Uchaguzi wa Igunga haukuwa huru na wa haki! - Freeman Mbowe

Kwa wenye access na Channel Ten, watch kipindi cha Channel Ten on Monday Live!, Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe yuko hewani...

Mwenyekiti Mbowe amesema uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki, ndio sababu ya msingi ya mgombea wa Chadema kususia kusaini ile karatasi ya matokeo na hivyo Chadema kitakwenda mahakamani kuyapinga matokeo hayo.

Mhe. Mbowe amesema, uchaguzi huo umeendeshwa na Tume isiyo huru ya Uchaguzi ambayo imekiuka kwa makusudi baadhi ya sheria, taratibu na kanuni kulikowaondolea haki ya kupiga kura, watu wengi wenye haki hiyo.

Pia serikali, imekiuka sheria, taratibu na kanuni, kwa kuingia Igunga kama serikali, wakati serikali haukupaswa kujiingiza kwenye direct campaingn za CCM.

Mbowe amesema, Chadema itakwenda mahakamani sio kwa lengo la kutaka matokeo ya Igunga yabatilishwe, bali inakwenda mahakamani ili mahakama kama chumbo huru, kihakikishe haki inatendeka kwa kuimuru Tume ya Uchaguzi itende haki na kupress kupatikana kwa Tume huru ya uchaguzi ili kuweka presedence kwa chaguzi nyingine zitakazofuatia.

Mbowe ameshamaliza kuhojiwa na sasa ni wachangiaji wakichangia kuu iitwayo "Uchaguzi wa Igunga, Tumejifunza Nini?.

Mhe. Mbowe is correct.

Mimi naomba CHADEMA wafanye haraka kupeleka hiyo kesi Mahakamani. Kuna vipengele kadhaa ambavyo vilikiukwa kwa uwazi kabisa na CCM kwenye kampeni za Uchaguzi wa Igunga.
  1. CCM wamekiuka matumizi ya Bajeti ya Uchaguzi iliyoidhinishwa na Msajili wa Vyama ambayo ilitakiwa iwe au isizidi Tshs.milioni 80. CCM wametumia zaidi ya Tshs.Bilioni 10!
  2. CCM wametumia Resources za Serikali kufanya kampeni Igunga. Tumeshuhudia Mawaziri na viongozi wengi waandamizi wa serikali wakitumia magari ya Serikali yenye namba ST(X) kuifanyia CCM kampeni ambayo ni kinyume cha sheria za Uchaguzi.
  3. CCM wamefanya Kampeni wakiwa na SILAHA kama bastola kinyume cha sheria ya Uchaguzi. Ushahidi ni upo wa kina Aden Rage(MB-Tabora mjini-CCM) na Aesh(MB-Sumbawanga-CCM).
  4. CCM wametumia RUSHWA kwenye Kampeni za Igunga. Wamehonga PESA na MAJI kuwarubuni wananchi wa Igunga wawape kura. Ushahidi upo kwamba MAJI yalikatwa mjini na yakaelekezwa VIJIJINI ili wanavijiji wapate maji na kuna gari la CCM lililokamatwa likiwa na Tshs.Milioni 20 siku ya Uchaguzi likigawa pesa kwa wapiga kura.
Haya ni mambo yako wazi kabisa CCM, NEC na MSAJILI WA VYAMA-John Tendwa knowa all these. Kwa hiyo CHADEMA fanyeni haraka kufungua hiyo kesi mahakamani ili haki itendeke.
 
Mhe. Mbowe is correct.

Mimi naomba CHADEMA wafanye haraka kupeleka hiyo kesi Mahakamani. Kuna vipengele kadhaa ambavyo vilikiukwa kwa uwazi kabisa na CCM kwenye kampeni za Uchaguzi wa Igunga.
  1. CCM wamekiuka matumizi ya Bajeti ya Uchaguzi iliyoidhinishwa na Msajili wa Vyama ambayo ilitakiwa iwe au isizidi Tshs.milioni 80. CCM wametumia zaidi ya Tshs.Bilioni 10!
  2. CCM wametumia Resources za Serikali kufanya kampeni Igunga. Tumeshuhudia Mawaziri na viongozi wengi waandamizi wa serikali wakitumia magari ya Serikali yenye namba ST(X) kuifanyia CCM kampeni ambayo ni kinyume cha sheria za Uchaguzi.
  3. CCM wamefanya Kampeni wakiwa na SILAHA kama bastola kinyume cha sheria ya Uchaguzi. Ushahidi ni upo wa kina Aden Rage(MB-Tabora mjini-CCM) na Aesh(MB-Sumbawanga-CCM).
  4. CCM wametumia RUSHWA kwenye Kampeni za Igunga. Wamehonga PESA na MAJI kuwarubuni wananchi wa Igunga wawape kura. Ushahidi upo kwamba MAJI yalikatwa mjini na yakaelekezwa VIJIJINI ili wanavijiji wapate maji na kuna gari la CCM lililokamatwa likiwa na Tshs.Milioni 20 siku ya Uchaguzi likigawa pesa kwa wapiga kura.
Haya ni mambo yako wazi kabisa CCM, NEC na MSAJILI WA VYAMA-John Tendwa knowa this. Kwa hiyo CHADEMA fanyeni haraka kufungua hiyo kesi mahakamani ili haki itendeke.
Mimi naona bora serikali ijenge mahakama mpya kwa ajili ya CDM lasivyo kesi zingine zote hazitasikilizwa. mpaka tufike 2015 sijui zitafika ngapi.
 
Jana usiku kupitia kipindi cha CHANNEL 10 ON MONDAY, MHE. mbowe asikika akijibu maswali kuhusu jinsi gani alivyopokea matokeo ya IGUNGA na kusema hawakubaliani na matokeo ktokana na sababu zifuatazo:

1) Tume ya uchaguzi siyo huru;

2)
CCM waligawa chakula na maji kwa wapiga kura kwa kisingizio kuwa ni serlikali ndo ilikuwa ikitekeleza majukumu yake;

3) CCM walitoa rushwa ya pesa tena hadharani;

4)
Baadhi ya wananchi walizuiliwa kupiga kura kwa madai kuwa hawana shahada;

5)
TAKUKURU na POLISI hawakuwasikiliza walipowasilisha malalamiko yao kuhusiana na ukeukwaji wa sheria za uchaguzi uliokuwa ukifanywa na CCM;

Mh. MBOWE tujibu maswali haya kabla hatujakuweka kwenye kundi linaloendesha siasa uchwara.

1)
Tume huru inakuwa siyo huru pale mnaposhindwa tu au hata pale mnaposhinda? Mbona mkishinda hamuendi mahakamani kuelezea mlivyoshinda kwa upendeleo wa tume?

2)
Kama vijana wa CHADEMA waliweza kumshambulia kiongozi wa SERIKSLI(D.C) , walishindwa nini kuwadhibiti vijana wa CCM walipoonekana kuwahonga wapiga kura maji, vyakula na hata pesa?

3)
CDM tunawaanini sana kwa vielelezo (documents), mliweza kuwatangaza mafisadi kule Mwembeyanga, Mkatoa vilelezo ya masanduku ya kura kule TUNDUMA, na hata TINDU LISSU pale Jangwani wakati wa kampeni mwaka jana alikua na barua ndeefu alivyonyanyaswa na JAKAYA KIKWETE sijui wapi huko na mengine mengi, Ziko wapi document mlizowawasilishia TAKUKURU, POLISI na TUME kuonesha jinsi CCM ilivyokeuka sheria ya Uchaguzi IGUNGA? Au nani ni wapishi wazuri wa data? Mnakwenda kuzipika kwanza?

4)
Je kukataa KUSAINI matokeo kila mtakaposhindwa ni kauli mbiu ya CDM sasa tujue?

5)
Je hizi propaganda za kufanya matukio mkasingizia wenzenu kuwa wamefanya wenyewe ni sera ya CDM sasa?

Mfano; kumwagia watu tindikali, kuchoma numba za wapinzani na hata kukununua Shahada za kupigia kura achilia mbali hili la kuwashawisi wanaume wawazuie wake zao wasiende kupiga kura kama mlivyofanya kule Tarime na mimi nilikua kule nilishudia wakati mh. WANGWE alipofariki.

Hakika propaganda za kiwango hicho si za binadamu wa Tanzania

6)
CDM mlikiri wenyewe kuwa mliingiza vijana zaidi ya 2000 kulinda kura IGUNGA. Je mlitaka TUME iruhusu watu wasio na shahada kupiga kura ili vijana wenu hao nao wapige?
subiria wanao wakianza kula nyasi ndo utajua unachokitetea. gabachori we!!!! Peoples........
 
Mzee Edwin Mtei wa Marangu Moshi anasikitika kutangaza kifo cha binti yake Mpendwa aitwaye CHADEMA kilicho tokea huko Igunga tarehe 2/10/2011 kwa Kupigwa na mume wake CCM kwa ugomvi wa Mapenzi akiwa na Kijana anaitwa Kashindye! Habari ziwafikie shangazi wa Marehemu wote akina Mbowe,Komu,Lyimo,Lema,Owenya,Kiwia,ndesamburo,mrema,masawe,kimaro,Urio! Mazishi yatafanyika baada ya Ndugu wote kumuangalia na kujua marehemu chanzo cha kifo chake! Ibada ya mazishi itaongozwa na Padri Mstaafu Dr Slaa wa Karatu! Habari ziwafikie Mr sugu,Msigwa,Shibuda,Zitto(mganga wa kienyeji wa marehemu),Mnyika akiwa dar,Mjomba wa Marehemu Selasini akiwa Rombo Mkuu,shoga wa marehe suzan kiwanga akiwa morogoro,mtoto wa marehemu Regia Mtema akiwa dar,shemeji wa marehemu Dr Kitila mkumbo! Ukisikia habari hizi mwambie mtu yeyote utakae muona amevaa gwanda!
 
  • Thanks
Reactions: Omr
UCHAGGA NA UKRISTO NDANI YA CHADEMA NI ZAO LA NDOTO ZA MCHANA ZA WALE WAVIVU WA KUFIKIRI

Wanasaikolojia siku zote hutufahamisha ya kwamba NI HULKA YA BINADAMU KUONA TU KILE ANACHOKIFIKIRIA akilini mwake.

Kwa mfano wewe ndugu Mkalagale, kama uko na washikaji wako hapo hivi sasa basi jaribu kufanya zoezi hili hapa simpo na utapata jibu kwa nini unafikiri jinsi unavyofikiri juu ya CHADEMA na hiyo dhana ya miaka nenda rudi ya UCHAGA:

1. Jiweke kwamba wewe ni refarii hivyo hutoshiriki kama mchezaji katika zoezi hili,

2. Jitahidi walau ukawapate kama watu wanne hivi kushiriki zoezi hili,

3. kama mku labda ndani ya nyumba hivi; nyumbani, ofisini, au hata ndani tu ya gari vile - hebu kawaambie kila mmoja wao aangalie nje kila mmoja kwa nafasi yake.

4. Wakimaliza kufanya zoezi hilo la kuangalia nje, sasa waambie kila mmoja akupe jibu juu ya KITU KIMOJA TU alichokiona wakati ule ulipompa nafasi ya kuangalia nje,

5. Kanuni mojawapo ili zoezi hili lifanikiwe ni kwamba MAREJESHO YOTE YA KITU GANI MTU ALIONA KWA KUCHUNGULIA nje kupitia dirisha au mlangoni NI SHARTI UPEWE KWA KUNONG'ONEZEWA MASIKIONI ili mtu mmoja asije akaamua kukupa tu jubu la wasemaji watakaomtanguia kukupa marejesho ya zoezi lenyewewe,

NB: Mwisho wa zoezi hili, amini usiamini, utastajaabishwa sana kugundua kwamba JAPO DIRISHA NI MOJA PA KUCHUNGULIA NA KULETA MAELEZO KWAMBA MSHIRIKI KAONA NINI NJE LAKINI AJABU NI KWAMBA KILA MMOJA ATAKUPA JIBU TOFAUTI TOFAUTI kulingana na kile kitu ambacho ndicho kinachomgusa zaidi kwenye ubongo wake na hivyo kupendezewa nayo na kutani kulisikia wakati wowote ule.

Kwa mfano:

a. Haitoshangaza sana kumsikia mwana dada binti mrembo atakuambia alipochungulia nje yeye aliona maua mazuri sana.

b. Kama kulikua na mtoto wa Rostam Aziz kwenye hilo kundi lako la mazoezi sana sana huenda akakuambia ama amemuona mtoto wa Robert Mugabe anapita au kaona Mercedez Benze SE 200 Model ikipita.

c. Pengine Tambwe Hizza kama alikwepo naye kwenye timu yako akakunong'onezea kwamba kamuona kijana mchuuza mkaa akipita na mzigo mzito sana wa magunia mawili akikokota kwenye baiskeli.

d. Tuseme zoezi hili lilifanyika mijini basi hapo utamsikia alosto mwenzangu na mimi yeye akikuambia kwamba alipochungulia kupitia dirisha la hoteli ya yule Mganda orofa ya 3 pale kwenye jengo la Benjamin Mkapa - Posta, kati ya vitu vyote pale nje yeye atakuambia ameona dala dala ya kwenda Mbagala Rangi Tatu express bila kugeuzia pale kwa Aziz Ali.

Kwa matiki ya zoezi hili ambalo halihitaji usomi wa zaidi ya darasa la pili tu, basi mwenzangu utagundua kwa nini mtu akipiga darubini ndani ya CHADEMA basi yeye huona tu sura za wanyama fulani wanaoitwa WACHAGGA wakipiga kura Igunga ha kufikia mtu wa elfu 23.

Nasema tangu mara baada ya zoezi hili hutokaa uwapende tena Mwana-CCM yeyote anayeshindwa kuona UTANZANIA ndani ya wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro na badala yake UCHAGGA wao ndio hujitokeza mbele zaidi hasa kitu uchaguzi unapoitishwa popote pale.

Na kama sikosei, sasa sasa mtu kama huyo hutochelewa kumuona kama Nape Nnauye anayetangazia umma wa Tanzania fungu la matokeo ambayo masikio yake yangependa kusikia, hata kama kufanya hivyo huenda ukampokonya Kafumu Ubunge wake huo geresha baada ya siku 180.

Ndio, nasema tangu sasa huenda Magwanda Orijino nitakua nimefanikiwa kukuelimisha taratibu humu mpaka kujihisi kama vile ulikua sawa tu na Tambwe Hizza wa kwenye mfano tu hapo juu aliyeona kijana na gunia la mkaa kulingana na mahitaji ya kule kwake Mbagalla (na hasa zama hizi za Umeme Ngeleja), wakati ulipokua unauanzisha uzi huu hapa chini, hata ukashindwa kuwaona WATANZANIA badala yake ukawaona tu WACHAGGA wakitia timu ndani ya nyumba ya CHADEMA ...

... poorBaba wa Taifa Mwalimu Nyerere hebu kamsikie huyu mjukuu wako alivyo na mdomo mchafu uliojaa ukabila!!!!!!!!!!!!

Nadhani baada ya kuelimika hapa Jamvini unajisikia kama vile umetua mzigo vile au sio?? Hebu jitofautishe basi na lile Genge la akina Mkigoma, FF, Rejao, Mbopo, Nape na wengine wa aina yao ambao hawakuwahi kuandika kitu humu zaidi ya kudondosha kimstari kimoja ama lenye tusi, kejeni, mashairi, uzabizabina (Rweyemamu et al 2011) na wengine wengi kama hao.

Mpaka hapo naomba ukajipime wewe mwenyewe na ukajiamulie tu kwa moyo mkunjufu kabisa kama kweli leo hii uko kwenye mstari sahihi kuitwa JF GREAT THINKER au pengine utakua umeteleza kidogo kuungana na akina HAO kule katika ulimwengu wa JF GREAT STINCKERS.
 
Watu wa nchi ambayo ni moja kati ya mskini zaidi hapa ulimwenguni wanashangaza sana. Kuna watu wachache walioamua kujitoa kuleta mabadiliko katika nchi hii lakini wanabezwa. Kama watanzania wengi wangekuwa wanatumia akili zao vizuri na pia kuthubutu kuhakikisha maslahi yao yanatekelezwa na viongozi wanaowaweka madarakani sidhani kama kungekuwa na kitu kinaichoitwa CCM tena. Nakubaliana na hoja nyingi zinazosema huwezi kuwa na akili timamu na uadilifu ukaunga mkono CCM. Otherwise ni mwehu.
 
Mzee Edwin Mtei wa Marangu Moshi anasikitika kutangaza kifo cha binti yake Mpendwa aitwaye CHADEMA kilicho tokea huko Igunga kwa Kupigwa na mume wake CCM kwa ugomvi wa Mapenzi akiwa na Kijana anaitwa Kashindye! Habari ziwafikie shangazi wa Marehemu wote akina Mbowe,Komu,Lyimo,Lema,Owenya,Kiwia,ndesamburo,mrema,masawe,kimaro,Urio! Mazishi yatafanyika baada ya Dr Kafumu kumuangalia marehemu chanzo cha kifo chake! Ibada ya mazishi itaongozwa na Padri Mstaafu Dr Slaa wa Karatu! Habari ziwafikie Mr sugu,Msigwa,Shibuda,Zitto(mganga wa kienyeji wa marehemu),Mnyika akiwa dar,Mjomba wa Marehemu Selasini akiwa Rombo Mkuu,shoga wa marehe suzan kiwanga akiwa morogoro,mtoto wa marehemu Regia Mtema akiwa dar,shemeji wa marehemu Dr Kitila mkumbo! Ukisikia habari hizi mwambie mtu yeyote utakae muona amevaa gwanda!
Hahahahah mzee hapo umenimaliza. Hii ni kali ya mwaka
 
Watu wa nchi ambayo ni moja kati ya mskini zaidi hapa ulimwenguni wanashangaza sana. Kuna watu wachache walioamua kujitoa kuleta mabadiliko katika nchi hii lakini wanabezwa. Kama watanzania wengi wangekuwa wanatumia akili zao vizuri na pia kuthubutu kuhakikisha maslahi yao yanatekelezwa na viongozi wanaowaweka madarakani sidhani kama kungekuwa na kitu kinaichoitwa CCM tena. Nakubaliana na hoja nyingi zinazosema huwezi kuwa na akili timamu na uadilifu ukaunga mkono CCM. Otherwise ni mwehu.
Hao wachache hawataki kuleta mabadiliko, wanataka kuleta Uchief. Yani nchi ishikwe na familia moja, tena ya Kichaga...wewe unaumwa.
 
Mzee Edwin Mtei wa Marangu Moshi anasikitika kutangaza kifo cha binti yake Mpendwa aitwaye CHADEMA kilicho tokea huko Igunga tarehe 2/10/2011 kwa Kupigwa na mume wake CCM kwa ugomvi wa Mapenzi akiwa na Kijana anaitwa Kashindye! Habari ziwafikie shangazi wa Marehemu wote akina Mbowe,Komu,Lyimo,Lema,Owenya,Kiwia,ndesamburo,mrema,masawe,kimaro,Urio! Mazishi yatafanyika baada ya Ndugu wote kumuangalia na kujua marehemu chanzo cha kifo chake! Ibada ya mazishi itaongozwa na Padri Mstaafu Dr Slaa wa Karatu! Habari ziwafikie Mr sugu,Msigwa,Shibuda,Zitto(mganga wa kienyeji wa marehemu),Mnyika akiwa dar,Mjomba wa Marehemu Selasini akiwa Rombo Mkuu,shoga wa marehe suzan kiwanga akiwa morogoro,mtoto wa marehemu Regia Mtema akiwa dar,shemeji wa marehemu Dr Kitila mkumbo! Ukisikia habari hizi mwambie mtu yeyote utakae muona amevaa gwanda!
tupige vita malalia na hasa kwa watoto wadogo, vinginevyo watakuja kuwa na mitazamo ya hovyo hovyo ukubwani
 
Mbowe yuko right kwenda court maana serikal ilihamia igunga kwa kivul cha rais mstaafu,usalama wa taifa na mawazir.wananch wametishiwa aman kwa bunduk na akina rage na mengineyo meng.naunga mkono hoja.
 
kwa kitendo kama hicho walichokifanya wana igunga ni fundisho kubwa kwa wanajimbo wengine inaonesha kwa namna gani ccm inaweza kucheza na utapeli kwa wananchi wa hali ya chini kama wana igunga when you look at the other side ya uchaguzi ni ufisadi mkubwa unatendeka wakati igunga na umaskini wao wanashangilia kuingiza ufedhuli na wizi kwenye jimbo lao huku dowans malipo yanafanywa likiibuka tena wanajitetea kuwa mambo haya yalifanyika wakati wa uchaguzi mdogo wa igunga these pple know what they are doing na haya yote ni kutaka kurudisha fedha za uchaguzi kwenye chama. ni kweli wananchi hawaoni haya yote hata hivyo big up cdm mumeonesha ni ushindi wa dhati kama kwa miaka 18 hamkuwepo igunga leo kwa miezi 3 na kupata votes 23,000 this is good step nikiangalia hii ratio 2015 votes 170000
 
Thats just silly! Kama hawaendi mahakama kupinga matokeo kwa sababu uchaguzi haukuwa huru na wa haki wanaenda mahakamani kufanya nini? Kwa kutopinga matokeo Mahakamani kunatuambiua kuwa wamekubali kuwa ni matokeo halali na ya haki. Kama kulikuwa na uvunjwaji mkubwa wa haki huko Igunga njia pekee ya kudai haki ni mahakamani. Sasa unaweza vipi kusema "uchaguzi haukuwa huru na wa haki" halafu ukakataa kupinga matokeo yake mahakamani? Unless you really don't believe what you are claiming au hauna ushahidi wa kuweza kuusimamisha mahakamani.

No Mwanakijiji hapo hukuwapata sawasawa. Hawakumaanisha kuwa hawatayapinga matokeo, hilo lipo. Isipokuwa what they mainly want to achieve siyo kubatilisha ule uchaguzi bali kurekebisha mambo ya jinsi uchaguzi unavyosimamiwa nchini. Pamoja na hii tume ya tumbili kusimamia uchaguzi juu ya miti iliyojaa nyani. Kuna mtu ameiweka bayana zaidi aliposema kwa kifupi ni mwendo wa kudai Katiba mpya!
 
Kwa kifupi uchaguzi haukuwa huru na haki. Serikali nzima ilihamia Igunga hata watu wa mbagala walipata matatizo ya kuezuliwa mapaa serkali imeenda baada ya siku 2.
Ila iko siku tutatoka utumwani kama wana wa Israel. Tuendelee kuomba kila mtu na imani yake Mungu atajibu maombi
 
Mbewe atambue mahakama ndo haohao kwahiyo ajue matokeo yatakua ndo hayohayo. Ilobaki ni kupigania katiba ibadilishwe
 
subiria wanao wakianza kula nyasi ndo utajua unachokitetea. gabachori we!!!! Peoples........

Hee! tayari wanakula nyasi we unafikiri ana nini! Unajua kama upo vizuri kidogo kiuchumi na kifikra huwezi kushabikia upuuzi kabisa! we fanya utafiti uone... wale wooote wanaoshabikia nchi kuliwa na mafisadi au chama cha mafisadi ni duni kifikra na kiuchumi pia! sababu uchumi mzuri kwa yeyote yule au katika jamii fulani unamfanya mtu au jamii husika kuwa na fikra nzuri na muda wote ujijua yeye ni nani na anataka nini katika maisha yake!
 
Thats just silly! Kama hawaendi mahakama kupinga matokeo kwa sababu uchaguzi haukuwa huru na wa haki wanaenda mahakamani kufanya nini? Kwa kutopinga matokeo Mahakamani kunatuambiua kuwa wamekubali kuwa ni matokeo halali na ya haki. Kama kulikuwa na uvunjwaji mkubwa wa haki huko Igunga njia pekee ya kudai haki ni mahakamani. Sasa unaweza vipi kusema "uchaguzi haukuwa huru na wa haki" halafu ukakataa kupinga matokeo yake mahakamani? Unless you really don't believe what you are claiming au hauna ushahidi wa kuweza kuusimamisha mahakamani.

Mzee Mwanakijiji! Mbowe alikuwa lini mwanasiasa? Ruzuku ikiondolewa atajiuzulu uenyekiti. Huwezi kupingana na mtu anayekuandikia hundi ya zaidi milioni 100 kwa mwezi. Mabadiliko ya kweli yatapatikana siku watakapopatikana viongozi wa kweli kwenye vyama vya upinzani, hesabu hii ni ndogo sana kuifafanua MBOWE +SLAA = MSHIKO (RUZUKU) + MATAPISHI YA CCM ; Chadema itaishia kuwa kama CUF.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Wana igunga wanaombea uchaguzi mwingine utokee haraka ili nao wafaidi ufisadi wa ccm kwa njia ya kampeni kwa kupata japo pilau na pombe za kienyeji................hii ndiyo ccm bwana yenye uwezo mkuwbwa wa kutumia umaikini wa watz
 
Waheshiwa Mbowe, Ndesamburo, Dr Slaa walikwepo kwanza CHADEMA ndipo ka-ruzuku hako kakafuata - njoosha rekodi hizi mzee.

Ila anachokizungumzia Mwanakijiji alichokibtiza jina 'Silly' kweli ni zaidi ya hilo neno kwa sabu mantiki yanapotelea moja kwa moja tangia hapo.

Ukosefu wa uchaguzi kuwa FREE AND FAIR ni pale Igunga hivyo kesi ni sharti ipate mizizi yake pale pale ndipo mambo mengine hufuata.

Cha msingi subiri uje uone CCM itakavyokua ikihangaika mara baada 2015 pindi baada ya kuwapiga chini wabunge wake wa hivi sasa kwa 75% na ruzuku yake ya sasa nayo kunywea kwa kipimo kama hicho hicho ndipo watakapojua kwa nini CUF hivi sasa usfiri ni wa kukokotwa na Punda na kesho yake kuniga tai kwenye helikpta ya hawara Igunga.

Lakini kimsingi mimi nimemuelewa vema; alikusudia kuwapiga tik-taka hawa wazembe wa kufikiri kama huyu ajiitaye CHAMA ili waendelee kukodolea macho kivuli hata baada ya jua kuzama kuhu mwenye kizuli chake akiondoka kivingine mbali kuleeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!

We kasherekee 'ushindi' wa Kafumu sasa hivi kabla mambo hayajarudishwa kwenye mstari stahiki na wale Wapambanaji wa uhakika.

Mzee Mwanakijiji! Mbowe alikuwa lini mwanasiasa? Ruzuku ikiondolewa atajiuzulu uenyekiti. Huwezi kupingana na mtu anayekuandikia hundi ya zaidi milioni 100 kwa mwezi. Mabadiliko ya kweli yatapatikana siku watakapopatikana viongozi wa kweli kwenye vyama vya upinzani, hesabu hii ni ndogo sana kuifafanua MBOWE +SLAA = MSHIKO (RUZUKU) + MATAPISHI YA CCM ; Chadema itaishia kuwa kama CUF.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Nimepitia thread na post mbali mbali hapa JF naona kipigo cha Igunga kimewachanganya sana magwanda! Nawashauri mnywe maji mengi na kukaa sehemu yenye utulivu ili akili iwarudie vizuri!
 
Back
Top Bottom