UCHAGUZI WA EALA: CCM inavyowanyanyapaa vijana.......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UCHAGUZI WA EALA: CCM inavyowanyanyapaa vijana..........

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Apr 18, 2012.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mr James Olle Millya


  CCM wanadai kuwa Millya kajitoa kisa alichujwa kugombea EALA
  .........hiii kauli ya wanamagamba inanifanya niangalie wale ambao kamati kuu ya ccm iliwapitisha........na nikabaini wengi wao ni wazee ambao wamevuruga sekta za umma walizopewa dhamana na sasa wanakwenda EALA kupumzika na kulinda ugali waliopora..........Vigogo wang'ara ubunge Afrika Mashariki........na vijana ambao ccm inaona wanafaa ni wale ambao wazazi wao walishika nyadhifa za juu ndani ya ccm na serikalini..........


  Nafasi tatu za bara................uteuzi wa Kimbisa, Murunya na Makongoro una walakini mkubwa..................Kiimbisa alilitafuna sana jiji la Dar, Murunya alitafuna Hifadhi ya Ngorongoro na watajwa hawa wawili walitumia kikamilifu pesa walizopora kwenye taasisi za umma kununua ubunge wa EALA...............na sasa wanaonekena kuwa mashujaa.................naye Makongoro hakuwa na cha kuhonga lakini kwa chama makini hakingeliweza kumpitisha mlevi huyu ambaye maisha yake yote hana mchango wa maana kwenye jamii..................yote haya yamefanyika kwa kuwaachia vijana maumivu..............makali sana.


  Nafasi za wanawake mbili zimenyakuliwa na akina Shyrose Bhanji na Angela Kizigha.................amabao umahiri wao hata wa kujieleza unatia shaka na wako wanawake wengineo wasomi na walijieleza vizuri lakini kwa sababu hawana mkate wa kuwahonga wabunge wa ccm hawakupewa nafasi ya kwenda kutuwakilisha................

  Waliofanya uteuzi mzuri ni NCCR-MAGEUZI pekee yao.....................na Bi. Dr. Nderakindo Perpetua Kessy ana upeo wa kuwazidi wateuliwa wote saba wa ccm na huyo ndiye ninamtarajia kung'ara kwenye bunge la EALA..............na Chadema mikakati yao ilikuwa aibu tupu........na inanipa wasiwasi wa ya kuwa kama hawatajirekebisha na kuajiri wataalamu wa kuwashauri vizuri basi wataanza kupoteza mwelekeo.........mgombea wao alikuwa dhaifu na sielewi kwa nini hawakuwa na majina mengine katika nafasi nyinginezo..........

  Ushauri kwa vijana
  .

  Kura zenu msizipoteze na kuwapa ccm kwa sababu hicho ni chama cha wazee hususani wastaafu na vijana ambao wazazi wao walikwishaula ndani ya hicho chama..........

  Kura zenu pelekeni vyama vya upinzani na kuhakikisha kiburi cha ccm kinafikia ukomo uchaguzi wa 2015 kwa kunyang'anywa Uraisi na uwingi wao Bungeni...........bila ya kufanya maamuzi haya magumu mtaendelea kuwasindikiza wachovu kwenda kukata kidali yao ya dhuluma tu.............

  Bunge la 2015 litusaidie kurekebisha utaratibu wa kuwateua wabunge wa EAC kwa kuwarudishia raia waifanye kazi hii moja kwa moja..............wabunge wa Bunge la Muungano kazi hii hawaiwezi zaidi ya kuitumia kuwajaza maswahiba wao ambao wanawahonga au wanaweza kuwatumia kufanikisha miradi yao ya kisiasa........
   
 2. n

  nyantella JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  hapo kwenye green, Unamtukana bure, Makongoro alijieleza mchango wake kwa jamii na Taifa zima la Tanzania. halafu kuhusu ushauri wako kwamba CCM ni chama cha wazee sii kweli kwani watu wote wanazeeka, hata kama sii wana CCM, halafu bila wazee vijana watatoka wapi? wazee ndio baba na mama wa hao vijana wako! pamoja na dharau zako kwa wazee kumbuka iko siku utazeeka tu. Tukana CCM kama chama kwa raha zako ila wazee tuwaheshimu! hata kama wazazi wako ni vijana!
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  tetea wazee kwa maana ya kuwa wale lakini ndiyo chimbuko la umasikini hapa nchini...............kuhusu Makongoro wewe jinyamazie tu.............kila mtu anayemfahamu Makongoro anajua ni mlevi tena wa kupindukia na kuna wakati hata anajikojolea mwenyewe......................labda ukweli wauma........mbona huongelei rushwa kama ndiyo sifa ya kuwa kiongozi ndani ya CCM ambayo hata wao wabunge wamekiri kuwa ilikuwa ikitembezwa waziwazi na hao walioibuka kideda?
   
 4. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Sio kweli kuwa Makongoro hakuhonga!! Kuna mkakati wa mafisadi unaothibitiwa na mmoja wao Mbunge Nimrod Mkono wa kumuondoa kwenye halmashauri kuu ya ccm ambako yeye ni mwiba sana kwao ili awe Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki; hivyo hawa mafisadi ndiyo waliotenga fungu la kuhonga kuhakikisha kuwa anaondoka kwenye uenyekiti wa ccm mkoa wa Mara!! Kwahiyo sio siri kuwa wagombea karibuni wote wa ccm wamepita kwa rushwa; walioshinda bila rushwa ni wale wawili wa upinzani tu!! Katika ccm bila kuhonga hupati nafasi ya uongozi na hiyo sio siri.
   
 5. L

  Lakuchumpa Member

  #5
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sawa its god
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  kwani akiondoka NEC wao wanapata faida gani?
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  you mean good?
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
 9. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Nauliza tena hivi mafisadi ndio wamemshawishi Mzee wa Saiti,kama jibu ni ndio basi naye atakuwa ni fisadi,na atakuwa hatufai kwenye saiti yetu,lakini kama ni utashi wake na mafisadi wametoa rushwa bila yeye kujua sintamulaumu ,lakini kama anajua atakuwa amelitia NAJISI jina la Nyerere
   
 10. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Akiondoka Makongoro Nec watakuwamempunguza mtu mmoja jasiri anaeweza kumkabili mwenyekiti wao dhaifu bila woga kuhusiana na azma yao ya kuvuana magamba!!
   
 11. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  UKWELI NI KWAMBA MKONO NDIO ALIYERATIBU KAMPENI YA MAKONGORO KUPATA HUO UBUNGE ; kama alijua au la hilo sina uhakika lakini kuwepo mkakati huo hilo ninahakika nalo. Nilikuwepo Dodoma na niliona Nimrod Mkono na wenzie walivyokuwa wanahangaika na kumbuka kwenye ccm preferential votes Makongoro ailtupwa mbali sana; Pasco aliwahi pia kuandika kuwa kuna mshiko wa kuua mtu unagawiwa kwa wabunge hata akadiriki kuandika kuwa hata wale ambao hakutegemea kuwa wangelambishwa walilambishwa!!
   
 12. k

  kaleb nikolai New Member

  #12
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ccm hawajachagua watu sahihi/bora wa kuliwakilisha taifa kwenye bunge la jumuia ya afrika mashariki, uzembe na mzaha wa namna hii utaligharimu taifa, na tutajuta kwa kutowakilishwa vema
   
 13. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,183
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Kuna sehemu umeongea ukweli mzuri,hasa uteuzi wa NCCR kwa yule mama Nderakindo kwa alivyojieleza vizuri na kwa maelezo yake huenda akawa mjenga hoja makini.
  Kuhusu Makongoro nyerere,hujamtendea haki ,
  *Maisha binafsi ya kila binadamu hubaki kuwa ni sehemu ya maumbile yake hadi siku ya kufa.ulevi wa makongoro huenda ulitokana na yeye kubaki bila kazi rasmi ya kufanya hasa baada ya kutoka vitani ambako alipigana bega kwa bega na askari wetu ili kumn'oa Nduli Idd amin dada wa uganda
  .
  Baada ya kurudi na kubaki bila kazi ulitegemea afanye nini zaidi ya kulewa na kujisahaulisha machungu yaliyomkuta vitani nk.kuna maboga wangapi wanaopeta leo ambao mchango wao au wa wazazi wao haukumsaidia chochote mtanzania.sembuse makongoro ambaye yeye na baba yake wote wameipigania nchi hii kila mtu kwa nafasi yake tena kwa dhati,nadhani wewe ni mmoja wea wale ambao mngetakiwa kumshukuru kwani alikuja kuwakomboa wahaya wakati idd amin akiwamwaga midomo.mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe.
  Kumbuka historia ya makongoro akiwa mbunge wa kwanza kuiangusha ccm katika jiji la arusha kupitia NCCR.

  Kuhusu kimbisa ni sawa kwani pamoja na umahiri wa kujieleza lakini sikuona chochote alichopaswa kujivunia katika uongozi wake kama meya wa jiji la DSM zaidi ya uchafu aliotuachia mabarabarani hadi ufisadi na uuzaji holela wa maeneo ya wazi bila aibu.

  Kuhusu vijana uko sawa ,lakini sikubaliani na wewe kwa hoja ya kuwakataa wazee kwa ujumla kwani bado baadhi yao ni wachapakazi wa kweli kuliko vijana wauza sura kama unavyofikiria.angalizo ni JK tulimpa kura zetu kwa kuamini damu changa kwa kizazi kipya ,yaliyotukuta hata wewe ni shahidi unayaona.labda kama na wewe ni mneemeka hapo sawa.

  Hata hao wabunge wa nchi jirani watakaoteuliwa huko subiri uone taswira utakazoziona huko.lazima wawe watu wazima.EALA sio bunge la kukamatana ufisadi bali ni bunge la kila mbunge kuwakilisha misimamo ya nchi yake na kutetea maslahi ya nchi yake zaidi.

  Nakubali ushauri wako kuwa vijana waamke sasa ili tupambane kuiondoa CCM madarakani kwa njia za kidemokrasia AHSANTE NA TUKO PAMOJA ....ALUTA CONTINUA,PAMBELI NE CHIMULENGE!
   
Loading...