Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Huu uchaguzi una maana kubwa sana kwa taifa la Tanzania. Ni uchaguzi unaoenda kui 'define' Tanzania kwa karne moja ijayo. Nchi hii iko katika njia panda, kuna hatma za aina mbili au tatu nchi inayoweza kuzifuata na yote hayo yanategemea mambo kadhaa. Ila ninachoweza kusema ni kuwa haijalishi nani atashinda kinyanganyiro cha Urais, haijalishi ni chama gani kitafanikiwa, jambo la muhimu kutambua ni kuwa huu uchaguzi ni 'referendum' ya sauti ya Mtanzania kutokana na hali ya nchi wanavyoiona.
Wakionyesha kwa sauti kuu kuwa hawajaridhishwa na muelekeo wa nchi hii itaonekana kuanzia katika kampeni hadi katika sanduku la kura na kama kutakuwa na mizengwe huko, wataionyesha kwa njia nyingine. Vivyo hivyo kama watataka waonyeshe kuwa wanaridhishwa na kila ambacho kimekuwa kinafanyika hasa katika nyanja zinazowagusa moja kwa moja, pia itaonekana.
Kwa msisitizo tu ni kuwa uchaguzi wowote wa kisiasa huwa unatoa fursa ya sauti na hoja ambazo huwa hazisikiki kusikika na kipimo cha uungwaji mkono wa hoja hizo huwa ni idadi ya kura, bila kujali kama wagombea wa sauti hizo wameshinda ama la. Hili jambo ndiyo linanifanya niamini kuwa uchaguzi huu si wa kawaida. Unaenda kuibadilisha Tanzania kwa namna ambayo wanahistoria wataikumbuka kwa sababu kuna hoja za msingi sana zinazolitambulisha ziko mezani huku kukiwa na mvutano mkali wa pande mbili zinazokinzana.
It is the best of times, it is the worst of times.