bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,667
Je nani asiyeona Maendeleo ya nchi yetu yanayosababishwa na Rais wetu anayetawala kupitia Chama Kikongwe barani Afrika na Dunia Chama cha Mapinduzi?kama huoni basi siwezi kukulaamu.ila uhalisia ni Rais aliyeleta maendeleo kwa Muda mfupi nani alikua na ndoto ya Kuona Airbus Ikimilikiwa na serikali yetu tena sio Moja nani alikua anajua ipo Siku Treni Ya umeme itajengwa Tanzania, Nani alikua na Ndoto ya Kuona Ujenzi wa Bwawa kubwa la Kufua umeme likijengwa Tanzania Likishindana na Aswan Dam, inga Dam, Kabora Bassa, Zambezi Dam..Nk haya ni Matunda ya Serikali ya awamu ya Tano chini ya Mtawala JPM.
Kwa sasa Upinzani wa Tanzania Upo ICU mashine zikichomolewa muda wowote wanazimika wamebaki Kulumbana wao kwa Wao kifupi hawana jipya mwisho wao umefika kwa kifupi wamekata Pumzi na Mbio ndio kwanza zipo mzunguko wa kwanza.Wamebaki wakisema Hakuna Demokrasia sio kweli wao demokrasia ya kweli ipo Sema wao wenyewe ndio watajifuta/watapoteana wenyewe, wamebaki na sera nyepesi Nyepesi ambazo hazina mashiko kwa mtu yeyote yule msomi yani wanafanya Cheap Politics.
Wamebaki Kulia wakisema ohoo tunaonewa wakati sio kweli wao wenyewe wamekosa mipango madhubuti ya kuwateka Watanzania wamekosa Sera madhubuti wanasubiri Kukosoa tu kifupi hawana Jipya.
Basi Tutarajie nini?Anguko kubwa sana la Wapinzani kwenye Uchaguzi wa 2020 kuna hatari wasipate Mwakilishi hata Mmoja, Wawakilishi wote wakatoka CCm na kushuhudia maendeleo makubwa sana ndani ya nchi yetu kama vile China au hata Cuba.
Kwa heri Upinzani Tanzania.