Uchaguzi wa 2015 -Nini kifanyike kusiwe na wizi wa kura

Kingdom Finder

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
1,119
1,387
Wana JF ninawaombeni tusaidiane kujadili jinsi ya kufanya katika uchaguzi wa mwaka 2015 ambao unakaribia angalau wizi wa kura kama siyo kwisha kabisa uweze angalau kuwa kidogo maana inavyoelekea kama wizi ukiendelea kuna janga la kuuana sisi kwa sisi kitu ambacho hatutaki kitokee. Je Katiba mpya itaweza kuwa suluhisho. Sina tatizo chama kitakachotawala kama kitapewa kihalali na raia.
 
Tatizo sio wizi wa kura tu, ila Daftari la Tume ya Uchanguzi. Watu wengi majina yetu yaliondolewa yakawekwa ya watu waliokufa miaka mingi ili mradi wasipige kura kwa wingi.
 
Daftari la kupigia Kura liboreshe na Tume ya Uchaguzi iwe huru sio hii ya sasa.
 
kwani vibaka wakiiba mtaani tuna wafanya nini? kwasababu mtu akiisha iba kura, serikali humpitisha, basi jukumu la kumnyoosha liko mikoni mwa raia wenye uchungu na kura zao. kura yako ni mali yako isimamie. na kama watu mtaungana kwa pamoja basi mambo yatakuwa shwari!

kusema ukweli sheria zetu hazimbani vizuri uchakachuaji maana hii ni kwafaida kwa serikali. uchungu wa kuibiwa kura anao mwananchi, hivyo ni kufanya makubaliano kati ya wapiga kura na wanaogombea kwamba kama kutafanyika jaribu la kuiba au kfanikiwa kuiba kura, basi watu watakushughulikia kama kibaka wa kuku maana mwizi ni mwiz tu, na ni bora mwizi wa kuku kuliko mwizi wa kura maana baada ya hapo anakunyonya tena miaka mitano zaidi
 
Introduction of electronic voters registration would be the best solution. It will give politicians other way of rigging vote
 
Tume Huru ya Uchaguzi itachangia kwa asilimia zaidi ya 50 uchaguzi kuwa huru na haki. Polisi na usalama wa taifa kuacha vitisho na ubabe kwa wapiga kura kabla na wakati wa kupiga kura.
 
Uwazi uongezwe katika vituo vya kupigia kura wakati wa kutoa matokeo, matokea ya kila kituo yawekwe wazi iwe ya urais,ubunge na hata madiwani. Pia mtu yeyote aruhusiwe kujumlisha matokeo katika jimbo zima kwa kukusanya vituoni!
 
Wana JF ninawaombeni tusaidiane kujadili jinsi ya kufanya katika uchaguzi wa mwaka 2015 ambao unakaribia angalau wizi wa kura kama siyo kwisha kabisa uweze angalau kuwa kidogo maana inavyoelekea kama wizi ukiendelea kuna janga la kuuana sisi kwa sisi kitu ambacho hatutaki kitokee. Je Katiba mpya itaweza kuwa suluhisho. Sina tatizo chama kitakachotawala kama kitapewa kihalali na raia.
Hakuna cha kufanyika... kwa kuwa hapakuwa na wizi wa kura!!! nikuulize kwenye uchaguzi wa viti 29!!! Kulifanyika nini? Mbona hakuna tuhuma za wizi wa Kura?
 
Back
Top Bottom