Uchaguzi wa 2010 hautakuwa Lelemama - Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi wa 2010 hautakuwa Lelemama - Kikwete

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Boflo, Aug 21, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Jijini Dar es salaam, mgombea urais wa CCM, Kikwete ndiye aliyekuwa wa kwanza kurejesha fomu na alisindikizwa na mamia ya wafuasi wa chama hicho waliokuwa wamevalia nguo za rangi ya kijani na njano, wakiimba nyimbo za kumsifia mtetezi huyo wa kiti cha urais.

  Lakini Kikwete, ambaye alipata ushindi wa zaidi ya asilimia 90 mwaka 2005, alionekana dhahiri kutobweteka na rekodi hiyo pamoja na uwingi huo wa wafuasi wake na shangwe zao na akaonya kuwa ushindi wa safari hii hautakuwa lelemama

  SOURCE: Mwananchi 20 August..

  My Intake
  Wadau hii kauli nimeshamsikia mara nyingi Rais wetu akisisitiza, hii inatokana na nini????
  1- Hofu ya Chadema?
  2-Ameongoza nchi kisanii na anajua sasa wananchi wameshashtuka?
  3-Anataka kuweka mikakati ya uchakachuaji wa matokeo?
  4-Hali ngumu ya maisha inayowakabili wananchi?
  5-.................

  ...toa mawazo yako


   
 2. M

  Mutu JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  anamaanisha kushinda mpaka kuchakachua
   
 3. mrefu36

  mrefu36 Member

  #3
  Aug 21, 2010
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  quote maisha bora yapo mgongoni tuyaonaje?
   
 4. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,449
  Likes Received: 781
  Trophy Points: 280
  1.Mweshimiwa hakutegemea Dr Slaa kugombea nafasi hiyo.
  2. CCM chama kikongwe kiligubikwa na rushwa,fitina,majungu,ubabaishaji,maandalizi hafifu, usimamizi mbovu wakati wa mchakato wa kura za maoni.
  3. Wanachama hawakuridhika na mchakato wa kuwaengua baadhi wanachama waliokuwa wameshinda.
  4.Majibu ya wasemaji wakuu wa CCM yaliwakera wananchi na kuongeza mvutano ndani ya chama.
  5. Chama tawala kimekuwa kikishinda huko nyuma kwa mazoea wala si kwa kazi nzuri.
  6. Chama kilichokuwa ni kimbilio la wanyonge kimewatema na kukumbatia matajiri.
  7. Serikali na Taasisi au Mashirika ya serikali yamekumbwa na kashfa nyingi tu,na imeshindwa kuyatolea maamuzi ya uhakika.
  8 Mwenye chama chake hayati Dr Julius Kambarage Nyerere hayupo tena kuuza sera za chama na mgombea uraisi kama alivyofanya 1995.
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Nadhani changamoto si Dr Slaa pekee hata professor Ibrahim Lipumba anamuumiza kichwa kuliko mnanyofikiri.Nitajaribu kutoa sababu chache kwanini Dr Slaa na Professor watampeleka puta Muungwana.

  [1] CCM wanajaribu kupunguza kura za Dr Slaa kwa kutumia sababu za kidini zaidi.watapenda kuwachuuza wapiga kura kwamba Dr ni Padre hafai kuongoza nchi.Mbinu hii itafanikiwa kuwanasa baadhi ya waislamu wasiopenda kufikiri.Tayari tunaona baadhi ya Radio na magazeti yenye mwelekeo wa kidini [Islamu] yakimwandama Dr Slaa kwa kutumia mbinu chafu ili kumdhoufisha.Mbinu hii imewahi kutumiwa na CCM mara nyingi wanapoona mgombea wa upinzani anakubalika zaidi ya mgombea wao.Mwaka 1995 wakati Mzee wa Kiraracha anawasumbua sana CCM ziliandaliwa kanda karibu misikiti yote Tanzania bara kumchafua Mrema kwamba ni adui wa waislamu kiasi fulani baadhi ya wapiga kura waislamu waliingia kwenye mtego wa CCM.Uchaguzi huu tena CCM wanakuja na mkakati wa mwaka 1995 sasa sijui Dr Slaa alivunja lini maasndamano ya waIslamu kama Bwana mrema aliekuw akitekeleza majukumu yake kama Waziri wa mambo ya ndani.

  [2] CCM wanajua wakiendelea kutumia sababu za kidini kumwangamiza Dr Slaa kura za waIslamu zinaweza kwenda CUF hivyo kumnufaisha zaidi Professor Lipumba ambae uchaguzi mkuu uliopita alishika nafasi ya pili.Professor Lipumba anauzoefu wa masula ya uchaguzi ingawa baadhi ya watu wanadhani si jambo zuri mwaka 2005 alishika nafasi ya pili huku Mbowe akiambulia nafasi ya tatu pamoja na kutumia Helicopter kwa mara ya kwanza katika uchaguzi Tanzania.CUF ilifumika Dar wakati wa kurejesha fomu kitu ambacho hakijawahi kutokea.CUF inakosa covarage ya kutosha kwenye vyombo vya habari ukilinganisha na CCM na CHADEMA,ukitegemea vyombo vya habari Tanzania kupata picha halisi uchaguzi utakavyokuwa uenda utakuwa unajidanganya kwa kudhani mpambano ni kati ya CCM na CHADEMA.

  Hakuna ubishi uchaguzi wa 2010 utakuwa ni uchaguzi utakao toa picha halisi jinsi Tanzania itakavyokuwa siku za usoni.CCM,CUF na CHADEMA ni vyama vitakavyotoa nafasi nzuri kwa wapiga kura kuchagua chama kitakachowaongoza miaka mitano ijayo.

   
 6. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ...WELL SAID!!...... mkuu wewe ni g.t wa ukweli
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Anamuogopa MGAWA pilau wa TUCTA sorry, ni Mgaya wa TUCTA na ile pilau aliyoikataaa
   
 8. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2010
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ]
  anahofia kauli yake aliyowatolea wafanyakazi
   
 9. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Najua anajutia sana maneno yake hayooo, sio uliona T-shirt zile zilizoandikwa " Sitaki Kura zenu" ?? Kile kisu cha kuwamaliza CCM
   
 10. Bourgeoisie

  Bourgeoisie JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hakuna ubishi kauli yake hii imemuumiza sana, maana anatafuta kila namna ya kuifuta lakini anshindwa. Oh! mara anaongeza mishahara kimya kimya! Oh! Mara anasema ule ulikuwa ni utani kati yake na Mgaya na mengineyo chungu nzima. Na hapo ifahamike kuwa Kutamka neno SAMAHANI kwa kiongozi asiye mwadilifu ni Ngumu Mnooooo!
   
 11. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  CCM ndio inamtisha....nadhani leo imeonekana wazi...
   
 12. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Anajaribu kutumia kila njia kukanusha kwamba hakusema hataki kura za wafanyakazi uzuri wa zama zetu tekelinalokujia litamuumbua kilaatakapojaribu kukanusha
   
Loading...