Uchaguzi Viti Maalum Chadema Wakwama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi Viti Maalum Chadema Wakwama

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Masonjo, Aug 12, 2010.

 1. M

  Masonjo JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2010
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 2,725
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  UKIONA kwa mwenzio kunaungua ujue kwako kunateketea. Hiyo ni kauli iliyodhihiri jana baada ya uchaguzi wa wabunge wa viti maalumu wa Chadema, kufutwa baada ya kutokea vurugu zilizohusisha utoaji wa rushwa na upendeleo kwa baadhi ya wagombea.

  Uchaguzi huo ambao ulikuwa ufanyike juzi, ulisitishwa usiku wa kuamkia jana baada ya wajumbe zaidi ya 25 wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), kuzuiwa kupiga kura kwa madai kuwa walikuwa wanatoka mikoa na wilaya mpya zilizotangazwa hivi karibuni.

  Aidha, vurugu hizo zinadaiwa kusababisha madhara zaidi baada ya mjumbe mjamzito kujifungulia njiani na mwingine mimba kuharibika.

  Mjumbe anayedaiwa kujifungulia njiani, alikuwa akitoka Kigoma kwenda katika uchaguzi huo na alijifungua baada ya kushtuka kutokana na kusikia kutokea kwa vurugu hizo.

  Mwingine ni mjumbe kutoka Pemba ambaye alikuwa ukumbini katika Viwanja vya maonesho ya biashara Sabasaba, Dar es Salaam ambapo inadaiwa ujauzito wake uliharibika alipotolewa nje ya mkutano na kuzuiwa kushiriki kuchagua wabunge, jambo lililosababisha
  kukimbizwa katika zahanati moja jijini Dar es Salaam.

  Kutokana na vurugu hizo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, alifika saa 2.15 usiku eneo la tukio kwa lengo la kusimamia uchaguzi ndipo alipogundua kuwapo kasoro hizo.

  Ilidaiwa kuwa wajumbe waliohesabiwa walikuwa 182 huku idadi iliyokuwa ikitakiwa ikiwa ni wajumbe 139, jambo lililosababisha vurugu baada ya baadhi yao kuanza kutolewa katika ukumbi wa mkutano.

  Karatasi zilianza kugawiwa kwa wajumbe saa 3.15 usiku na baadhi ya wajumbe kukosa na waliotolewa nje kulazimisha kuingia jambo lililosababisha Kabwe aingilie kati ili haki itendeke.

  Hata hivyo Zitto alikiri kuwapo matatizo na kuwaarifu wagombea kuwa uchaguzi hauwezi kuendelea hadi atakaposikiliza wanachama wake.

  Baada ya vurugu za juzi, mkutano huo ulihamishiwa Mbezi Beach katika ukumbi wa Kiramuu, ambako hadi jana jioni wajumbe walikuwa hawajaanza kupiga kura kutokana na wasimamizi wa uchaguzi huo kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu ya Chadema.

  Ilipofika jioni, wajumbe hao wa Kamati Kuu waliwasili mkutanoni akiwamo Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe na waandishi wa habari kutakiwa kutoka nje ya mkutano ili kutoa nafasi ya kujadili mambo yao kwa siri.

  Mwandishi wa habari hizi, alilazimika kuzungumza na wajumbe waliokuwa wakienda msalani na kupata habari kuwa mkutano huo umefutwa na Mbowe.

  Wajumbe hao walidai kuwa Mbowe alituhumu kuwa uchaguzi huo ulinuka rushwa. Hata hivyo, baada ya kumalizika kwa mkutano huo saa moja usiku jana, Mbowe alitoka na hakutaka kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu kilichokuwa kikijadiliwa.

  Msimamizi wa uchaguzi huo, Dk. Kitila Mkumbo, alikiri kuvunjwa kwa mkutano huo na kuongeza kuwa hatima ya uteuzi wa wabunge wa viti maalumu itajadiliwa kesho katika kikao cha Kamati Kuu na Baraza Kuu la Chadema na katika Mkutano Mkuu keshokutwa.

  Aidha wajumbe wote ambao si wa Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, walitakiwa kurudi majumbani kwa kuwa mkutano wa Bawacha hautafanyika tena wala hautakuwa na nguvu ya kuchagua wabunge wa viti maalumu.

  Habari zilizopatikana baadaye jana kutoka miongoni mwa wajumbe wa mkutano wa Bawacha, zilisema kuna watu wanaopendelewa na viongozi wa kitaifa na hali yao ya kukubalika ni mbaya na ndiyo maana ya kufuta uchaguzi huo ili kupanga jinsi ya kuwabeba.

  Hii ni mara ya pili kwa Chadema kuahirisha mikutano ya Bawacha na ya vijana - Bavicha, ambapo mwaka jana, kulitokea mvutano kati ya kambi za Mbowe na Zitto na hivyo uchaguzi kuahirishwa.

  Source: HabariLeo | Chadema hakieleweki
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Source: HabariLeo....mhariri Michuzi
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kitila, tuhabarishe bwana. Wewe ndiye uliekuwa unasimamia uchaguzi huu. Kwani wale viti maalum mwaka 2005 mliwapataje? Hatukusikia haya wakati ule.
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mhariri msadizi Malaria sugu
   
 5. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,498
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red: WHAT IS THIS MAN ACTUALLY DOING IN CHADEMA? DO CHADEMA PEOPLE REALLY KNOW THE INSIDE OF HIM? ANYWAY, FROM TODAY ONWARDS, I WONT UTTER A SINGLE WORD ON HIM, BUT TIME WILL TELL! KNOWING THE INSIDE OF A MAN IS VERY IMPORTANT, NOT HIS/HER WORDS!
   
 6. M

  Masonjo JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2010
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 2,725
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Na Elizabeth Suleyman

  MKUTANO wa kuwachagua wabunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chadema jana ulivunjika tena kutokana na maadalizi mabovu na kuibuka kwa mapungufu kadhaa.

  Msimamizi wa uchaguzi huo, Dk Kitila Mkumbo aliliambia gazeti hili kuwa mapungufu yaliyojitokeza ni kuwa hakukuwepo na muongozo wa uchaguzi wa Chadema."Kukosekana kwa muongozo wa uchaguzi, kulisababisha, wagombea kutofuata maadili ya chama,'' alisema Dk Mkumbo.

  Hata hivyo, Dk Mkumbo alisema uamuzi wa jinsi ya kuwapata wabunge wa viti maalumu utategemeana na maamuzi yatakayotolewa na katibu mkuu wa chama hicho, Dk Willbrod Slaa ambaye pia ni mgombea urais, katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

  Katika hatua nyingine, leo Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) linakutana kujadili kiini cha kuvunjika kwa mkutano wa kuchagua wabunge wanawake wa viti maalumu.

  Hali haikuwa shwari kwenye uteuzi huo tangu juzi. Siku hiyo, naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe aliahirisha uchaguzi kutokana na kujitokeza malalamiko mengi, ikiwemo baadhi ya wagombea wasio na wajumbe kupewa fursa ya kujipigia kura na wengine kutoruhusiwa.

  Sababu nyingine ya kusitishwa kwa uchaguzi huo ni kitendo cha baadhi ya wajumbe zaidi ya 25 kutoka wilaya mpya zilizoanzishwa karibuni kuondolewa ukumbini na hivyo kunyimwa fursa ya kupiga kura, kuibuka kwa mamluki pamoja na makundi ambayo yanaonekana yanatokana na tofauti za viongozi wa ngazi za juu.

  Uamuzi wa kuvunjwa kwa mkutano huo kuliwafanya baadhi ya wagombea kuingiwa hofu ya kuhisi kuwa huenda kamati kuu ya Chadema inaweza kuteua wagombea inaowataka na kuacha wengine wenye sifa.

  Zitto alifafanua kuwa wameamua kusitisha mchakato huo na kwamba kamati kuu ya Chadema pamoja na viongozi wa Bawacha itakutana na kutoa maamuzi ya kurudiwa kwa uchaguzi na kwamba uko uwezekana wa kufanya uchaguzi leo. Aliongeza kuwa malalamiko ya kupungua kwa karatasi za uchaguzi, ni jambo ambalo halipaswi kujitokeza tena na kwamba ni vyema likafanyiwa marekebisho mapema.

  "Isije ikaonekana Chadema ni chama ambacho hakina demokrasia ya kweli ya kuwajali wanachama wake," alisema Zitto. "Hatuwezi kuwaacha wajumbe waliotoka mikoani kwenye wilaya hizo mpya wasipige kura na pia wagombea ambao wasiokuwa na wajumbea walioruhusiwa kukaa ndani kupiga kura wapige na wengine wenye wajumbe kufungiwa nje," alisema. "Haitakuwa picha nzuri, kwani tutakuwa tunawanyima haki yao ya msingi ya kupiga kura," alisisitiza.

  Source: Mwananchi

   
 7. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Mhamasishaji Mkuu: ROSTAM A..
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160

  OMG.... WTF.... KMA!!!!!

  Kitila na wenzako, this is not good aisee, hebu wekeni mambo sawa na muwe organized; chadema sasa ni another level kwahiyo wekeni vitu sawa. Ikibidi ajirini full time people wawafanyie protocol and procedure management na kama mnao watoeni muweke wengine hao wamefeli!! hatujasahau ya kule kusini mlivyotolewa kwenye uchaguzi, fomu imechukuliwa kabla ya confirmation ya mgombea

  WE LOOK TO YOU FOR QUALITY, CHANGE NOW!!!
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Read the literal contents of both papers and judge your self...my insistance in red
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mmmh chama hakina muongozo wa namna ya kuchagua wabunge wake? kweli tutafika kwa namna hii?!
   
 11. Tuntu

  Tuntu JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2010
  Joined: Jan 28, 2009
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kulikuwa na ukiukaji wa taratibu sio vibaya kufutwa kwa uchaguzi, lakini ni vizuri uchaguzi urudiwe na wajumbe wote wapate nafasi ya kuchagua na kuchaguliwa kwa haki.

  Katu wakulu wa chama wasijichague majina kivyao kama ilivyokuwa 2005.
   
 12. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  JF kuna mambo
   
 13. R

  Ramos JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Imekuwa vyema kuufuta...
   
 14. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Jamani kwanini kwenye ukweli tusiseme ukweli?
   
 15. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Huyu bundi alikuwepo siku nyingi sana.


  ......Katika hatua nyingine, mvutano mkubwa umeibuka ndani ya Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema.
  Mvutano huo umeibuka kutokana na kundi la Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na lile la Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe kutofautiana kuhusu wagombea wa viti maalum.

  Wakati kundi la Mbowe linataka wabunge wa sasa wa viti maalum wachaguliwe, wakati kundi la Zitto linataka wateuliwe wapya kutoka maeneo mbalimbali kwa lengo la kusambaza chama.


  Uchaguzi wa Viti Maalum Chadema uliingia dosari juzi baada ya baadhi ya wagombea kudaiwa kutoa rushwa ili wachaguliwe.

  Tuhuma hizo na nyingine zilisababisha, wasimamizi wa uchaguzi kuvunja uchaguzi huo.

  Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zinadai kwamba Mbowe alikemea vikali vitendo vya rushwa ndani ya Chadema kwa wagombea hao.


  Miongoni mwa wagombea ambao walionekana kukataliwa ni pamoja na wabunge watatu wa viti maalum waliomaliza muda wao.
   
 16. Mwanamosi

  Mwanamosi Member

  #16
  Aug 12, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee msekwa aliposema rushwa haiko CCM tu iko kila mahali alionekana mwehu..nadhani hii ni changamoto kama nilivyokwishachangia suala hilo.......hizo ndio politiks za bongo rushwa ipo na itachukua muda mrefu kuitokomeza...nilisema Miiko na Maadili ya Uongozi ianze kufatwa sasa na kizazi kipya ili kiikomboe nchi.
   
 17. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  CHADEMA kama wanadhamira ya kweli kupata suluhisho la hili suala wanawake wapige kura kuchagua wawakilishi wao bungeni wanaume msijipe jukumu la kuwachagulia mtu ondokeni kwenye mfumo DUME , mnataka kuonyesha kuwa wanawake wenyewe hawawezi si kweli na si sahihi
   
 18. F

  Froida JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  CHADEMA mumefanya vizuri kualisha uchaguzi ili kutafuta njia bora zaidi ya kupata uwakilishi wa wanawake wekeni mipango mizuri na muitishe uchaguzi haraka iwezekanavyo ili isije ikaleta gumzo lisilo la lazima lakini kwa maamuzi yenu ni ditto
   
 19. n

  njori Member

  #19
  Aug 12, 2010
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwakweli ktk hili mmetuaibisha,m/kiti kuingilia uchaguzi wa wanawake si umwachie mkeo bac ashughulikie?lazima uende wewe?tumeamini CHADEMA bila uchaga haiwezekani!
   
 20. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Kama alivyosema Dr Slaa marupurupu ya wabunge ni makubwa sana, wekeni kanuni mbunge wa CHADEMA atoe 50% ya marupurupu yake kwa ajili ya shughuli za uhai wa chama tuone ni wangapi bado watataka huo ubunge.
   
Loading...