Uchaguzi Vijibweni; Zitto kukabiliana na kinana, CCM waanza rafu, rufaa ya CHADEMA yakataliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi Vijibweni; Zitto kukabiliana na kinana, CCM waanza rafu, rufaa ya CHADEMA yakataliwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, Mar 9, 2012.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Naibu katibu mkuu Chadema, Naibu kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, mkiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirka ya Umma na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ndo mgeni rasmi atakayezindua kampeni ya Chadema kata ya Vjibweni Leo.
  Wakati Zitto akisubiriwa kuzindua kampeni hizo leo mchana, atalazimika kukabiliana na hoja za ccm dhidi ya Chadema zilizotemwa na Abdulrahamani Kinana ambaye ndiye aliyezindua kampeni za Chama hicho jumatano wiki. Viongozi wa kata wameelekezwa kukusanya hoja hizo ambazo ataelezwa Zitto kabla hajasimama na kuzijibu zile zenye mantiki
  ZITTO pia tumempangia kuongea na wazee wa vijiwen kabla hajahutubia. Utaratibu huu unaandaliwa na viogozi wa kata.

  RAFU ZA CCM NI ZIPI?
  Kwa mujibu wa ratiba ya NEC, kampeni zinaanza leo nchi nzima. Hata hivyo, Kinana aliweza kufanya mkutano mkubwa wa Hadhara na kumnadi mgombea wa CCM tangu jumatano wiki HII, kinyume na utaratibu uliowekwa na NEC.
  Sisi tuliamua kukata rufaa kuhusu jambo hili. Cha kushangaza Mtendaji wa kata akasema kwamba hiyo ni ratiba ya vyama, kwa hiyo, haina tatizo.
  Pili, akasema nikipokea barua yenu, ina maanisha kuwa na ninyi hamtazindua kampeni yenu ijumaa hadi rufaa itakapoamuliwa. Tulipewa hilo sharti gumu ambalo kwa kweli halina msinigi wo wote WALA MANTIKI.
  Tulitafakari hilo, huku tukiwa hatuko tayari kuchelewesha kampeni, pili tunajua tunaweza tusimpate tena Zitto kwa sababu hatujui amepangiwa Kwenda wapi baada ya leo na CHAMA. Tukaamua kuachana na rufaa. Tulihisi wangeweza kujadili hiyo rufaa kwa wiki 2, kampeni ikawa wiki mmoja. CCM kila kitu kinawezekana.
  Zitto PIA amepangiwa kuongea na wazee wa Vibweni kabla ya kuhutubia mchana wa Leo. utaratibu huu unaandaliwa na viongozi wa kata.


  KATIKA HALI YA KUSHANGAZA.
  Wiki iliyopita, sikumbuki tarehe, kulikuwa na masuala ambayo tulitaka ufafanuzi kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi ambaye ndiye mtendaji wa Kata. Tulimpigia simu bila yeye kujua kwamba alipigiwa simu na nani na ana tatizo gani LA kiofisi? Akatuelekeza alipo. Tulimkuta yuko na vionogozi wa ccm kata ya vijibweni, Viongozi wa ccm ngazi ya wilaya na mfadhili wa ccm wa kata hiyo. Huyu mfadhili ni mhinidi aliyewekeza sana ktk fukwe za kata hiyo. Tukajiuliza, viongozi wa ccm, msimamizi wa uchaguzi na mfadhili wa ccm saa kumi mchana ndani ya Hotel wanakula au wanajadili nini? Mimi sitaki kuwa shehe Yahya, ila kuna utata.
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu Aweda kila la kheri.Mungu wetu ni mwaminifu yuko pamoja na nyie.
   
 3. escober

  escober JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 391
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hiyo vijibweni ni wapi?
   
 4. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,685
  Likes Received: 17,745
  Trophy Points: 280
  bila shaka ni Kigamboni
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Vijibweni ni wapi ?,uchaguzi wa nani kata,tarafa,wilaya,mkoa ?.
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hukusoma utafiti wa Aweda kuhusu ushindi wa 70% huko Vijibweni - Kigamboni wilaya ya Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam.
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu naona kuna hujuma nyingine kwa kuwa wazee wengi watakuwa Diamond Jubileee kumsikiliza Rais!!!!!
   
 8. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kazi kweli kweli,
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Mar 9, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kila la heri CDM
   
 10. p

  panadol JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kila la kheri CCM ,watalalamika sana tumeshawazoea ili wakishindwa waonekane wamefanyiwa rafu ata babu yao alisema hamtambuhi JK leo anamtambua baada ya umoja wa mabalozi kumtaka apeleke ushaidi wa kuibiwa kura na yeye kushindwa kufanya hivyo aibu imemshuka yeye na viongozi wengine wa chama chake wakati vyama vingine vyote vya upinzani vilikubaliana na ushindi wa JK ,Ebu fikirieni kwa akili ya kawaida umeshindwa kuing'oa CCM kwenye uchaguzi mkuu 2010 na wakati huo kulikuwa na kashfa za ufisadi kwa baadhi ya viongozi wake je leo hali imetulia viongozi wenye tuuma hizo kwa wale waliothibitika wamechukuliwa atua na wengine mafaili yao yako kwa mkurugenzi wa mashitaka wa serikali bado wanachunguzwa na watanzania wanajua hilo je leo utaweza kuing'oa CCM ? Mfano majimbo ya Igunga,Uzini na chaguzi mbali mbali za kata,vitongoji na vijiji zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika CCM inashinda kwa kishindo waulizeni vizuri viongozi wenu wawape takwimu za chaguzi zote zilizofanyika baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 na nawambieni tena kwa herufi kubwa ukiona panya analia ujue kabanwa mtegoni hana pa kutokea CCM itashinda Vijibweni na Arumeru Mashariki kwa kuwa ina sera nzuri zinazoeleweka na kutekelezeka,wapinzani mkipanda jukwaani hamna sera mnazungumzia ufisadi tu kapeni zinaanza mpaka zimakwisha nani atakuchagua kama hizo ndiyo sera mnafanya mipasho majukwaani ndiyo maana watanzania hawawaelewi na hawawachaguhi na wala si kufanyiwa rafu wala kuibiwa kura imekula kwenu mtabaki kulalamika kila chaguzi wenzenu washinda tu!
   
 11. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,719
  Likes Received: 1,628
  Trophy Points: 280
  vijbweni ziko nyingi tufafanulie mkuu
   
 12. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwenye Red highlight. sioni mantiki ya doubt yako hii. hivi wewe ukiwa mwanachadema wengine wote ni maadui? kuna wengine hata mke na mume (mf. will slaa na rose kamili) wa vyama tofauti walikuwa wanalala kitanda kimoja, sembuse hao waliokaa tu hoteli wakipata lunch. Simple kuwa na itikadi tofauti si uhasama, we mbulu vipi bana? Aghhh... boring.
   
 13. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hilo la kupata lunch pamoja kati ya msimamizi wa uchaguzi, viongozi wa ccm kata ya vijibweni, viongozi wa ccm wilaya na mfadhili wa ccm jimbo la kigamboni wakati huu ambapo kuna uchaguzi mdogo kata ya vijibweni ndipo utata wenyewe ulipo.
  Wamejianika hadharani mapema mno, mbinu zao zitadhibitiwa mapema.
   
 14. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  kama mungu akiwa upande wetu,nani huyo basi aliye kinyume chetu atakayeweza shnda nguvu za muumba HAKi haidhulumiki kwa vyovyote vile.Cha msingi fanyeni kampeni za
  kistaarabu dhibitin hujuma+wizi ushindi unakuja
   
 15. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe makalio, kwa mfano wewe una kesi halafu ukapita sehemu ukawakuta hakimu wa kesi na Mshtaki/ Mshtakiwa wako wapo sehemu wanapata Lunch, je utachukulia kwamba kuna hukumu ya haki atakayoitoa huyo hakimu hususan kama haki ipo upande wako?
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Vijibweni si mbali na Uzini.
   
 17. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,071
  Likes Received: 421
  Trophy Points: 180
  vijibweni ipo Kigamboni, jimbo la Temeke mkoa wa Dar es salaam.
   
 18. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jamani CCM hawaishi visa! Wanan'gan'gania madaraka kwanguvu wakati nchi imewashinda. No value addition hata kidogo. Naamini kamanda Zitto utawakilisha chama ipasavyo uko Kigamboni ili vijibweni iongezeke kambini.
   
 19. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #19
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nitahudhuria huko vijibweni kutoa tathmini ya ushindi.
   
Loading...