Uchaguzi UWT moto;Mpambanaji wa ufisadi agawa fedha kwa makatibu; Mgombea Urais 2015 amfadhili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi UWT moto;Mpambanaji wa ufisadi agawa fedha kwa makatibu; Mgombea Urais 2015 amfadhili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 16, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145  JUMAPILI, SEPTEMBA 16, 2012 08:21 NA MWANDISHI WETU, TANGA

  *Mpambanaji wa ufisadi agawa fedha kwa makatibu
  *Afadhiliwa na mmoja wa wagombea urais 2015
  *Adaiwa kutoa rushwa ya Sh 200,000 hadi Sh 500,000
  HALI ya siasa ndani ya Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) imezidi kuchafuka baada ya mmoja wanachama wanaowania nafasi ya uenyekiti wa umoja huo kutuhumiwa kugawa fedha kwa makatibu wa wilaya wa umoja huo.

  Mgombea huyo ambaye pia ni mpambanaji wa ufisadi, anadaiwa amekuwa akigawa fedha kwa makatibu hao kama njia ya kushawishi achaguliwe katika nafasi hiyo nyeti na ya juu ndani ya jumuiya hiyo.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya UWT, mgombea huyo ambaye pia ni mbunge, amekuwa akifanya vitendo hivyo vya kugawa hongo kwa makatibu hao wa UWT sambamba na kuwalisha viapo wapambe wake.

  Chanzo hicho kilisema kuwa tangu yalipopitishwa majina ya wagombea wa nafasi hiyo mjini Dodoma na vikao vya UWT, mgombea huyo aliwakusanya baadhi ya makatibu wa UWT wilayani Korogwe kwa lengo la kuweka mikakati huku akimwaga fedha kuanzia Sh 200,000 hadi Sh 500,000 kwa kila aliyehudhuria kikao hicho.

  Kikao hicho ambacho kilifanyika katika hoteli ya Transit kilitoa na azimio huku mgombea huyo akiweka mikakati yake ya kuhakikisha anatumia mikutano ya uchaguzi kupitia mgongo wa makatibu hao.

  Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa mpambanaji huyo wa ufisadi alimtumia Katibu wa UWT Wilaya moja mkoani Kilimanjaro kufanikisha mkakati wake huo.

  Katibu huyo wa UWT, alipewa kazi hiyo pamoja na fungu la fedha ambako alitakiwa kugawa kwa kila wilaya Sh 500,000 lakini hakufanya hivyo na kulazimika kugawa Sh 200,000.

  "Unajua ndugu yangu kwa muda mrefu UWT ilikuwa na utulivu mkubwa lakini katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka huu fedha zimekuwa zikimwaga mno tofauti na miaka iliyopita.

  "Mimi pamoja na makatibu wenzangu wa wilaya wa UWT kutoka katika mkoa wa Kilimanjrao tumepewa kila mtu Sh 200,000 badala ya Sh 500,000 tuliyokuwa tumekubaliana tangu awali.

  "…, hata hivyo bado fedha tulizopewa sisi ni tofauti na wenzetu wa mkoa wa Arusha ambao kila mmoja amepewa Sh 500,000.

  "Tunajua wazi tunachukua hizi fedha kuna kundi la mgombea mmoja wa urais amekuwa akimpa fedha huyu mama aweze kupambana katika uchaguzi Mkuu wa UWT.

  "Kwa hali hizi Sh 200,000 tulipopewa tuliahidiwa kumaliziwa kiasi kilichobaki kama tulivyokubaliana pamoja na kwa hali hii sasa ninakiomba chama changu cha CCM kifanye uchunguzi ya kina katika hili," alisema na kuhoji mtoa habari huyo ambaye pia ni Katibu wa UWT katika moja ya wilaya za mkoa wa Kilimanjaro.

  Inaelezwa kuwa mgombea huyo wa UWT mbaye pia ni Mbunge amesoma alama za nyakati baada ya kuona hali ya siasa imebadilika katika jimbo lake hali inayoonyesha huenda asirejee bungeni mwaka 2015.

  "Jimbo lake huyu mgombea hivi sasa lina upinzani mkali kwa sababu upepo wa siasa umebadilika, CHADEMA waliingilia na kufanya kazi ya ushawishi hivyo kuna hatihati ya kutorejea tena mjengoni mpambanaji huyo.

  "….hivi sasa hata anapoitisha mikutano ya wananchi amekuwa akitumia lugha za ubabe dhidi ya wapinzania wake wa ndani ya chama na nje ya chama hali inayodhihirisha wazi kuwa na wakati mgumu," analisema mtoa habari huyo na kuongeza:

  "Kwa muda mrefu UWT imekuwa ni injini kubwa ndani ya CCM hasa kila inapofika uchaguzi mkuu wa nchi au wa majimbo ambako huwa na kazi ya kuomba kura za chama kwa wanawake.

  "Na katika kipindi chote tulikuwa na utulivu wa hali ya juu ndani ya UWT lakini uchaguzi wa mwaka huu umekuwa na fujo na fitina za kila aina hasa kutoka kwa mmoja wa wagombea wa uenyekiti wa taifa."

  Alipotafutwa Katibu wa UWT wa anayetuhumiwa, alikana akisema jambo hilo halina ukweli wowote huku akimtaka mwandishi wa habari hizi kwenda ofisi kwake.

  "Duh! ndugu yangu ninakuomba uje ofisini kutokana na jambo hilo kuwa kubwa. Binafsi niseme katika wilaya yangu sijapewa fedha na mgombea yoyote ila ninakuomba uje ofisini tuzungumze zaidi.

  "Pamoja na hali hiyo lakini napenda kusema ….Sina uhusiano na fedha zilizokuja ndani ya wilaya yangu zilitoka makao makuu ya chama ndugu yangu," alisema.

  MTANZANIA Jumapili ilipomtafua Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kujua namna chama hicho kinavyopambana na wagombea wanaotoa rushwa, alisema katu chama hicho hakiwezi kuvumilia vitendo vya rushwa.

  Aliweka wazi kuwa ikiwa kuna wagombea watabainika wanafanya hivyo watachukuliwa hatua hata kama watafanikiwa kushinda katika uchaguzi.

  Katika vikao vya Baraza Kuu la UWT ililofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni, majina matatu yalipitishwa kuwania uenyekiti wa UWT.

  Hao ni Mwenyekiti wa sasa anayetetea nafasi yake, Sophia Simba, Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango na Meryrose Magige.

  Hata hivyo upinzani mkali unatarajiwa kuwa kati ya Sophia Simba ambaye anaonekana kuungwa mkono na kundi kubwa la wajumbe wa mkutano mkuu kwa kusimamia sera yake ya viti maalum kuwekewa kikomo ili kila mwanamke aweze kupata nafasi ya ubunge huku Anne Kilango, akisimami sera yake ya kuondoa ukomo katika ubunge wa Viti Maalum ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]

  WALIOTOSWA WALALAMIKA RUSHWA, UPENDELEO


  na Mwandishi wetu

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]MAPENDEKEZO ya Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) wa CCM ya majina ya wagombea nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo ngazi ya taifa, yameibua mlolongo wa tuhuma kuwa yalifikiwa kwa upendeleo, rushwa na woga.


  Tuhuma hizo zimetolewa na baadhi ya walioomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo, ambao majina yao hayakupendekezwa na kamati wanayodai kuwa ilifanya kazi kwa woga na kuwapendelea baadhi ya wagombea baada ya kushawishiwa kwa rushwa.

  Mbali ya malalamiko ya wagombea, taarifa kutoka ndani ya UWT zinaeleza kuwa, uteuzi wa majina yaliyopendekezwa na kamati ya utekelezaji na kupelekwa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM umeibua ufa baina ya wanajumuiya hiyo kwa kile kinachoelezwa baadhi yao kujiona wanatengwa kwa sababu hawana watu wa kuwapigania dhidi ya wake wa vigogo wanaodaiwa kuogopwa na kutetewa na waume zao.


  Mmoja wa wagombea ambaye jina lake halikupendekezwa, Hamida Thabit, katika mahojiano yake na gazeti hili kuhusu mwenendo wa mchakato wa uteuzi alisema ulikuwa wa hovyo kwa sababu haukuzingatia sifa na uwezo wa waombaji.


  Alisema waombaji wenye sifa majina yao hayakupendekezwa kwa sababu hawakuwa na pesa za kuwafurahisha wajumbe, na majina ya waombaji ambao waume zao wana sauti ndani ya chama yalipitishwa kwa woga.


  "Sijaridhika na mapendekezo ya kamati. Siyo kwamba nina uchu wa madaraka, lakini wakati mwingine ukiona mambo yanakwenda kombo kiasi cha kutisha ni lazima kusema. Na ninasema ili NEC ilione hili, itende haki kwa sababu UWT ni waoga.


  "Baadhi yetu majina yetu hayakupendekezwa kwa sababu hatuna pesa, hatuna watu wa kututetea, hatuna wanaume wenye nyadhifa au sauti ndani ya chama. Ni aibu kwa jumuiya iliyokomaa kama UWT kuchagua watu kwa kuwaogopa, eti wasipochaguliwa watapiga kelele.


  "Wabunge wenye majimbo, wana kazi za kila siku za kusimamia majimbo yao, bado wanataka na kazi ngumu ya kuongoza umoja huu na majina yao yanapitishwa, hiyo maana yake nini? Wanaachwa watu wenye sifa, wanaoijua UWT," alisema Hamida.


  Alisema mwenendo wa sasa wa CCM unaonekana kuwa wa kifamilia zaidi kwa sababu licha ya kuwa na wanachama wengi wenye sifa na uwezo wa kushika nafasi za uongozi, bado nafasi hizo zinatolewa kwa kujuana na hasa kwa kuangalia wake wa vigogo.


  Alitolea mfano wa Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, kuwa ni mbunge wa jimbo ambaye ana jukumu la kuwatumikia wapiga kura wake, hivyo hapaswi kukabidhiwa jukumu lingine la kuongoza UWT kwa sababu majukumu yote ni mazito.


  Pia alisema Maryrose Majinge hakupaswa kupendekezwa kwa sababu hana sifa zinazostahili kuwa kiongozi wa juu wa umoja huo.


  "Anne Kilango ni mbunge wa jimbo, anawajibika kwa karibu sana kwa wananchi wa jimbo lake, lakini bado anataka uenyekiti wa jumuiya. Majukumu yote ni mazito, kwanini yeye tu majukumu hayo?


  "Sophia Simba ni sawa kwa sababu yeye ni mwenyekiti hivyo anatetea kiti chake na anao uzoefu wa uongozi ndani ya jumuiya, lakini hata huyu Maryrose, ametokea umoja wa vijana moja kwa moja amerushwa hadi kwenye uenyekiti, aanzie chini ajifunze na kupata uzoefu.


  "Huu ni upendeleo wa wazi kabisa, unajua ukiwa na watoto watatu halafu ukawa unampendelea mmoja tu, wengine lazima watalalamika na itafika mahali watapachukia nyumbani, huko ndiko tunakokwenda.


  "Kwa sababu lazima ieleweke kuwa kujua kupiga kelele siyo ujuzi wa kiutendaji, kupiga kelele bungeni siyo kigezo cha kuwa kiongozi bora," alisema.


  Alipoulizwa kama ana mpango wa kukata rufaa kupinga mapendekezo hayo, alisema hana mpango huo kwa sababu anaamini hakuna kitakachofanyika isipokuwa anabaki na matumaini NEC itatenda haki.


  Mgombea mwingine aliyelalamikia mapendekezo ya kamati ya utekelezaji ya UWT ni Hilder Kitana, ambaye alisema ingawa anayaheshimu maamuzi ya kamati hiyo, amesikitishwa na kitendo chake cha woga.


  Kitana alisema kamati hiyo imewaacha baadhi ya waombaji wenye sifa na kuchukua majina ya watu ambao hawana rekodi ya uongozi ndani ya jumuiya, lakini pia wenye majukumu ya kila siku kwa nafasi ambazo tayari wanazo.


  "Wameamua wamependekeza majina hayo sawa, nayaheshimu. Lakini nimesikitishwa na woga wa kamati hii. Tukienda kwa kuogopana kama walivyokuwa wanasema ndani ya kamati hiyo hatutafika, tunaiua jumuiya.


  "Mimi nimekuwa Mjumbe Kamati Kuu ya UWT, nimekuwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, ninaijua jumuiya, sina jukumu kwa sasa linalonibana moja kwa moja zaidi ya biashara zangu, halafu jina langu linakatwa kwa sababu wanasema wakimuacha Kilango, anaongea sana na mke wa mtu mkubwa itakuwa matatizo, atapiga kelele hadi kwenye vyombo vya habari, huu ni udhaifu mkubwa," alisema Kitana.


  Kwa upande wake, Maryrose Majinge, alisema licha ya jina lake kupendekezwa, anasubiri maamuzi ya NEC.


  Alisema nafasi za uongozi ndani ya CCM zinapaswa kuzingatia uwezo wa utendaji badala ya kuchagua watu kwa sifa ya kuzungumza au kwa majina ya wenzi wao.


  Wiki iliyopita, kamati ya utekelezaji ya UWT iliyoketi mjini Dodoma ilipendekeza majina ya wanachama wake watatu kwenda NEC ya CCM kwa ajili ya kuwania uenyekiti wa jumuiya hiyo.

  Waliopendekezwa ni Mwenyekiti wa sasa, Sophia Simba, Anne Kilango na Maryrose Majinge.


  Wagombea katika kinyang'anyiro hicho walikuwa tisa ambao ni Halima Mamuya, Teresia Huvisa, Ritha Mlaki, Raya Safari, Simba, Majinge, Kilango, Thabit na Kitana.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Oh, Kwahiyo huyo mtoa hongo ni Anne Kilango? na Support ya Mgombea Urais 2015 ni Edward Lowassa?

  How nice... Sophia Simba lazima basi ana baraka za Mgombea Urais 2015 naye ni MEMBE; Sababu PRINCE anataka Umoja Wa Vijana

  Sera ya Kumkubali MEMBE...
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna faida gani tangible za kuwa mwenyekiti wa UWT?
  Nazingatia usemi wa Mwl Nyerere, kuwa ukiona watu wanakimbilia uongozi ujue iko namna. Uongozi ni mzigo, very demanding and stressful. Nielimisheni na mie nichangamke.
   
 4. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,654
  Likes Received: 3,301
  Trophy Points: 280
  Anne kilango huyo anajidanganya!!muda wake wa kutudanganya umekwisha!of course bora amekuja na cash!vinginevyo tusingemsikiliza kabisaa.
   
 5. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Mwenyekiti wa UWT hagombei ubunge wa Viti maalum, anapitishwa moja kwa moja na jina lake linapelekwa tume ya uchaguzi (la kwanza). Pili ni mjumbe wa Kamati kuu (CC) ambayo hufanya maamuzi mazito ya chama. Na faida nyinginezo kadhaa ikiwemo ushawaishi kwa mgombea Urais ajaye............Nafasi hii ni muhimu wakati huu hasa kwa kuangalia 2015
   
 6. C

  Concrete JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Wote ni wachafu tu, hakuna wa maana hapo.

  Inakuwaje tena Kilango awe anaungwa mkono na Lowassa?

  CCM ina mambo ya ajabu sana kama wachawi vile.
   
 7. d

  dmwinuka Member

  #7
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mimi binafsi naona sasa uongozi katika nchi hii ni biashara ambayo inachuuzwa kwa pesa na rasilimali zinginezo kwa kuwa mtu hazingatii uongozi ni "kuonyesha njia na dhamani anayopewa mtu kwa ajili ya wenzake" Hata hivyo tumefika hapa kwa ajili ya watu wasio na uwezo stahiki kukimbilia ikulu, kuna biashara gani huko? Hawa wanaonunua uongozi wanategemea kurudisha fedha walizotumia kwa namna gani kama sio kwa ufisadi na rushwa.
   
 8. p

  politiki JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  hapo ndio maana niliwapenda sana chadema kwa sababu ya kukataa guarantee ya kupewa vyeo hata kama hunauwezo
  mama mmoja alikuwa mwenyekiti wa BAVICHA TAIFA lakini ilipofika wakati wa viti maalum aligombea kama wananchama wengine wa kawaida na kushindwa hiyo ndio demokrasia hakuna mambo ya kupeana vyeo eti kwa kuwa wewe m-kiti.
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi nakumbuka kuwa Simba alikuwa kwenye kambi ya Lowassa na Kilango alikuwa akipiga vita ufisadi akiwa miongoni mwa wale makamanda waliojipambanua katika vita dhidi ya ufisadi. Yote yanawezekana kwa kuwa katika siasa hakuna adui wa kudumu. Nadhani wale makamanda wa vita dhidi ya ufisadi wamesambaratika na sasa inabidi wajisalimishe tu mmoja baada ya mwingine.
   
 10. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Anawezeshwa na Membe siyo Lowassa. Binafsi nawashangaa kupigana vikumbo kwa chama-mfu! Hawajielewi!
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,219
  Trophy Points: 280
  nyinyiemu usipohonga hupati nafasi..... Kinanuka rushwa
   
 12. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Hapa sidhani...Anna Kilango yupo kwenye lile kundi ambalo lili ibuka CCM kupinga vita ufisadi- Mengi,Mwakyembe,Sitta na wengine majina yamenitoka.Pia Membe na Nape walikuwa kwenye ili kundi ingawa Membe kwenye mikutano yao hakujitokeza.

  Ukishaona mwanamke anatamka hadharani fulani ni DUME LA MBEGU ni vigumu kumbadilisha msimamo wake dhidi ya huyo mwanaume.Sofia Simba aliyatamka hayo kuwajibu wakina Kilango na kundi lake na inawezeka wazo la kumngoa Sofia Simba ndio lilianzia hapa

  Lakini kwenye siasa za Tanzania chochote kinawezekana,Anna Kilango kwenda against bwana wake ( Mzee Malecela) ambaye ni adui ya Lowassa na vile vile kuamua kupoke pesa kutoka kwa Lowassa ambaye alikuwa anampiga vijembe kuhusu malipo ya Richmond.
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Oh, Yeah Hapo naona Unasema kuhusu Uhusiano wa Anne Kilango na Mzee Malecela labda sababu ya Lowassa na Kikwete campaign na kumtupa CHINI

  Lakini Ukiangalia Anne Kilango hawezi kwenda kwenye Team ya Membe na Prince (Rithwani) sababu ya JK ? Au Anaweza akawa kundi hili

  Lakini, Mama Simba yeye cheo chake kimetokea SAIGON sidhani Anne anaweza kuwa kundi hili; Na Unakumbuka Mama Simba anamsema Anne ni FISADI

  Sababu ya Kiwanda cha Tangawizi Same... Kikwete alialikwa kwenye Harambee Miaka 3 iliyopita pesa zikachangwa up to 4 bill Shillings...

  Kiwanda Kikwete alikuwa akifungue Mwezi May or June 2012; Wanasema kiwanda hakipo pesa Mama Kilango kaziweka kibindoni...

  Ukiona alichopiga nacho PICHA kwa Sh. 4 bill hakuna Mashine zinazofanya kazi kila kitu hand-work... SHAME Kikwete hajaitwa kufungua...
   
 14. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  watapambanaaaaaaaaaaaa lakini hawatamshinda chama kubwa S.S a.k.a SOPHIA SIMBA
   
 15. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  mama kilango ni tapeli wa kisiasa tu hana lolote. atashindwa kama walivyoshindwa wengine,
   
 16. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  kilango mwongo wa kimataifa.
  juzi kwenye caucus ya wabunge wa chama amelia hadharani kuwa anamwomba radhi lowassa kuwa hakujua kuwa alikuwa anaonewa. mnafiki tu huyu wala hawezi kujisimamia kamwe. waliwaacha solemba watanzania hawa yeye na wenzake kina sitta kwenye sakata la dowans, kisa kunusuru vyeo vyao...
  hana ubavu wa kumshinda sophia simba.
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Hee kumbe alishajisalimisha? Sasa wale makamanda waliojipambanua dhidi ya ufisadi wamebaki wangapi? Naona Kimaro alishughulikiwa, Sitta naye akashughulikiwa, Shelukindo alishajisalimisha, Eng. Stellah Manyanya alishasalimishwa, Selelii naye alipata haki yake, Lembeli hasikiki tena manake Mgeja kamuwekea police marking. Dr. Mwakyembe bado anapigana lakini kama yupo peke yake
   
 18. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ngoja ya Ngoswe nimwachie Ngoswe.
  I'm out.
   
 19. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Chama cha mapindizi kama vile kina rahana. Hivi hawa watu walipiataje katika kamati zote? Watu wanaogawa chama, watu walio ua chama wanakuwaje wagombea?

  Mama Kilango si ndo yule shabiki wa Supika Sitta aka standard aliyekuwa anataka kugombea kupiatia Chadema baada ya kuuwa chama cha mapinduzi? Nafikiri ianabidi ajiulize alikuwaje mpiganaji wakati haamini katika kupigana?
   
 20. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2014
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  KUMEKUCHA. Naona Mama Maryrose Majinge Anajipigia "CHAPUO" ITV kumepambazuka na RADIO ONE Kumepambazuka! Ila anaongea facts sana angefaa kuwepo CHADEMA kwani anatofauti sana na mafisadi!
   
Loading...