Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,037
- 22,728
Ha ha haa ! I am here, Mkuu.
Ila mkuu sijajua ni kwa nini hauoni mimi ninachokiona, kuwa kwa kiasi kikubwa, kuna madukuduku mengi juu ya hicho kinachohubiriwa cha ubora wa liberty na demokrasia huko US. Matukio ya hivi karibuni huko US ukweli yananitoa kwenye reli ya kuamini kuna liberty na demokrasia ya uhakika huko Marekani. Ngoja niendelee kuzibugia popcorn .
Republican Rep. Marjorie Taylor Greene vows to IMPEACH Biden on his first day in office, says she’ll be ‘voice of ignored voters’
Freshman Congresswoman Marjorie Taylor Greene (R-Georgia) has pledged to bring articles of impeachment against Joe Biden on his very first day in office, mirroring a similar move by Democrats early on in Trump’s presidency.www.rt.com
TUJITEGEMEE, wakati ukibugia popcorn, jitahidi pia kusoma vitabu vya historia. Soma historia inatufundisha nini hatari ya kuweka madaraka makubwa yasiyo na mipaka mikononi mwa binadamu moja! Wamarekani wengi walizikimbia nchi zao za asili kukwepa kuwa chini ya binadamu ambao ama walikabidhiwa madaraka makubwa yasiyo na kikomo au waliojitwalia kwa nguvu na kujikabidhi madaraka kama hayo.
Cha ajabu ni kwamba binadamu hao wote waliwezeshwa na binadamu wenzao kama wewe na mimi. Binadamu tunatofautiana kulingana na mazingira na mazingara tuliyokulia. Kwa bahati nzuri historia iliweza kutuzindua mapema kidogo baadhi yetu na kutufungua macho. Hivyo ninyi wengine pia endeleeni kuzibugia popcorn mkifuatilia matukio kama haya labda iko siku nanyi mtapata bahati kama hiyo...usiku mwema.