Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,394
- 31,345
- Thread starter
- #201
'AMEBANA AMEACHIA'
HATAKIRI KUSHINDWA , UKUU WA TAASISI ZA USA UNAONEKANA
Si mara moja mbili au tatu Rais anayeondoka madarakani Bw Trump amekataa kukiri makosa
Wala si mara moja au mbili au tatu, Rais Trump amekubali kuwajibika.
Mara zote tendo la kushindwa, kwake ni dhalili , atalitafutia sababu hata za kipuuzi ilimradi tu
Kama alivyokataa kukiri makosa ya 'Birtherism' au kuomba msamaha ndivyo ambavyo amekataa kukubali ameshindwa uchaguzi na wala hataki kuwajibika katika kumpongeza na kuachia madaraka kwa amani
Dhidi ya yote hayo, wiki hii amekiri kutaka kushiriki katika kukabidhi madaraka kwa amani.
Hili limekuja baada ya pressure kutokana na aibu iliyotokea kwa Trump kushawishi wafuasi wake kuvuruga mchakato wa Bunge katika kumuidhinisha Biden kama Rais ajaye.
Rais Trump alirudi DC akiacha shughuli za mwaka mpya kwa kile alichosema tukutane ' DC tarehe 6'
Katika hali isiyo ya kawaida Trump alidhani anaweza kushawishi Mabunge mawili ya US kutoidhinisha matokeo
Hii ilikuwa ndoto ya mchana na ya kipuuzi. Kwa mtu anayejua katiba ya Marekani hilo lisingewezekana.
Trump si wa kulaumiwa sana kwasababu ya uwezo wake wa kufikiri.
Wapambe wake kama Seneta Hawley na Ted Cruz ndio waliomtia mkenge wa kumfurahisha.
Trump alishawishi makundi ya white supremacists wakiwa na jina la proud boys kuvamia viwanja vya Bunge.
Kulikuwa na uzembe mkubwa katika usalama pengine kwa kudhani ni wazungu na huenda ni '' waelewa' tofauti na Black lives matter. Madhara yaliyotokea na picha za matukio yamebaki kuwa aibu kwa US
Pamoja na vurugu, Mabunge yalirejea na kukamilisha kazi ya kuthibitisha matokeo.
Mjadala uliopo ni kuhusu hali ya afya ya Rais Trump kiakili.
Wengi wanahofia siku 11 zinaweza kuwa na tatizo la usalama.
Inasemwa, Rais Trump alijaribu kushawishi kushambulia sehemu moja ya dunia.
Tumaini la Trump ni kuwa uwepo wa vita ungevuta muda wakati akitafuta mbinu za kubaki madarakani
Katika ukuu wa taasisi za Marekani uligomea mpango mzima
Jana, mwenyekiti wa majeshi amekutana na Spika wa Bunge mama Pelosi kujadili usalama
Kinachowatisha Wamarekani ni pale wanapofikiria kuwa iwapo Rais amefungiwa Instagram, Facebook na Tweeter, inawezekanaje basi mtu huyo akaaminiwa kudhibiti nuclear codes?
Taasisi zimeweka plan A, B, C.
Kwanza, shinikizo la Trump ajiuzulu katika siku 11 kuepusha madhara kutokana na mawenge wenge aliyo nayo
Pili, baraza la mawaziri litumie kifungu 25 cha katiba kutangaza Rais hana uwezo wa kuongoza
Tatu, Bunge limuondoea kwa mashtaka ''impeachment'
Plan A na B haiwezekani, Trump hawezi kukubali kujiuzulu na Baraza lake la mawaziri lina waoga hawawezi kumuondoa. Plan C inawezekana lakini pia ina kikwazo. Bunge (House of Rep) lina Dems wengi na linaweza kuunga mkono hoja wakiweno Republicans .
Seneti imemeguka na kuna uwezekana hata wa kupata maseneta 20 kuunga mkono.
Tatizo lipo sehemu moja, hadi sasa seneti inaongozwa na M.McConnel. ambaye amesema seneti italiifikiria suala hilo tarehe 19 ya siku moja kabla ya Trump kuondoka WH.
Kwa mtazamo wa haraka kuna 'chaos' zinazochagizwa na Trump. Kwa mtazamo wa kina taasisi zinafanya kazi na nchi inaendelea bila shaka. Mathalan, waliofanya vurugu wanasakwa na kuchukuliwa hatua.
Kwa Marekani hakuna 'asiyejulikana'' sheria inafuata mkondo. Viongozi wa Polisi katika eneo la Bunge wamewajibishwa tayari, wengine wakiachia ngazi kwa kupukutika. Wahuni wanasakwa hata Wasiojulikana watajulikana. Ni USA na ukuu wa Taasisi si kundi, makundi, mtu au watu. Ni Taasisi zinazoongoza nchi
Tusemezane