Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,394
- 31,345
- Thread starter
- #81
Marekani sheria inafuata mkondo na haki inalindwa. Trump ana haki na anatuimia. Sijui kama una habari alitoa madai ya wizi wa kura kabla ya kupigwa kura. Alisema '' namna pekee atakayoshindwa ni kwa wizi wa kura''Na kwa kuwa hakuna kura zilizoibiwa, hata akikagua kwa magnifying glass, hatopata kitu. Kwa hiyo tumwachie aangalie wee mpaka achoke; hapati ushahidi. Isn't it then kinda premature kusema hana ushahidi wakati ndio michakato ya kupitia upya kura inafanyika? Tuache mpaka mwisho tuone kama ushahidi upo au la.
Matokeo yalipotangazwa kasema kura zimeibwa. Hakuwa na ushahidi. Kamtuma AG Barr kutafuta kura zilizoibwa.
Yaani nikutuhumu kwa wizi na kisha kwenda kutafuta ushahidi.
Kule Arizona na Georgia alisema hakuna wizi, baada ya kushindwa kuna wizi!
Nina uhakika wakati wa Gore-Bush kuna haya; ima ulikuwa hujazaliwa, au ulikuwa mdogo au ulikuwa mkubwa usielewa au hukuelewa kabisa. Kuna upande wa pili, umejitahidi kusoma na kupata uelewa. Sina uhakika kama umamalize kitabu au kusoma kingineUchaguzi huu mazingira yake "ya kawaida" ni ya kulinganisha na ya Gore-Bush saga. Gore aliconcede lini? [Disemba 13]; Lini Bush Jr alitambuliwa Rasmi kwamba ni rais mteule?
Tofauti ya kura za Bush na Gore ilikuwa 500 (mia tano). Gore ali ' concede' kabla ya ku-retract.
Kura 500 si sawa na tofauti ya kura milioni 5 iliyiopo leo kati ya Trump na Biden.
Katika Gore-Bush kesi ilikwenda mahakamani kwasababu ilikuwa ''too close to call'', kura 500
Trump- Hillary, tofauti ya kura za electoral college ilikuwa chini ya 80,000. Hillaru ali concede usiku ule ule hata pale alipokuwa na tofauti ya kura 10,000 katika state moja.
Mfano wa Gore-Bush !
Please kuna tatizo gani ukinukuu mtu kwa usahihi? Nilichosema ni hiviWaliosema uchaguzi umeibiwa mwaka 2016 walikuwa Democrats, na stori za udukuzi wa Urusi, ambazo uchunguzi rasmi nadhani ulifanyika na kuonekana madai hayakuwa ya kweli.
Madai ya kwamba uchaguzi umeibwa si mageni. Mwaka 2016 alikuwa na madai kama hayo kabla ya uchaguzi.
Maana yake ni kuwa kabla ya uchaguzi 2016 Trump alisema kuna wizi wa kura unafanyika.
Hapa ni kabla ya kura hata moja kupigwa.
Unachosema wewe ni kuhusu Russia investigation. Hakuna Democrats aliyesema kuna wizi wa kura, kilichosemwa ni kuwa kulikuwa na interference kutoka Russia. Hili lipo katika taarifa ya Mueller ambayo AG Barr ameificha lakini itapatikana tu baada ya January 20.
Pili, kamati ya senate ikiongozwa na Chuck Grassley ambaye leo hii ana Corona katika umri wa 87, ilisema wazi kuwa Russia iliingilia uchaguzi wa 2016. Haya ni kwa uchache. Kwahiyo, tofautisha kuiba kura na ku influence uchaguzi, ni vitu viwili tofauti. Kubwa zaidi umeninukuu kwa jazba ukajibu kisichoulizwa, na watu wengi hufeli mitihani kwa kutoelewa hoja au kuvamia bila kujua msingi wa hoja
Siyo Joe Biden. Kumbe alikuwa mwandamizi tu hilo ni tofauti na PEOTUS au POTUSNa ndivyo pia kwa Team Biden: "Whatever happens, do not concede", alisikika Mdemokrati mwandamizi akimwambia Biden.
Sijui kama una taarifa Dir Kreb amefukuzwa kwa tweet jana kwa kosa la kusema ''uchaguzi huu umekuwa salama zaidi katika historia ya Marekani''. Una taarifa hiyo?Trump alichukua hatua kwa kuanzisha CISA. Na kuweka executive order ya kuhakikisha chaguzi zijazo (ukiwemo huu) uchunguzwe na vyombo vya usalama ili kuzuia au kubaini kuvurugwa uchaguzi na mataifa ya nje.
Katika miaka 20 fraud ya uchaguzi Marekani haiafikia hata 0.01% ni katika kiwango cha chini sanaPili, hiyo kauli ya hakuna fraud kubwa kiasi cha kubadili matokeo inasigana na hoja kuu ya kwamba hakuna fraud.
Katika milioni zaidi ya 140 na ushee huwezi kukosa watu wawili au watatu waliofanya tofauti.
kuna kitu kinaitwa widespread voter fraud. Kule Carolina Trump aliwahi kusema kuna wizi wa kura mwaka 2016 kwa Reprsentative. Uchunguzi ulibaini Republican walifanya hivyo hadi mshindi akaamua mwenyewe kuachia ngazi na kukiri hilo.
Eeh Mungu wangu!Tatu, mfumo wa shirikisho unatoa mamlaka ngazi za chini ambako kunaleta fursa za wizi kufanyika. Trump alishinda uchaguzi huu kwa kura nyingi, viti vingi vya Seneti na Congress, kwa kiwango ambacho hakikuwahi kuonekana toka 1776. Sema tu, wizi wa kura ulizipunguza sana. Hata hivyo, siku ya uchaguzi bado Trump alikuwa anashinda, ikabidi wasitishe kuhesabu ili waibe kura za Urais tu, tena bila haya wala kujificha kivile (the end justifies the means); panga pangua Trump asipewe awamu ya pili.
Nimejiuliza niendelee au niache, jibu likawa rahisi, sina uzoefu katika level hii