Uchaguzi unakuja, pombe, pilau, kanga na fulana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi unakuja, pombe, pilau, kanga na fulana!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by BAK, Aug 13, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,640
  Likes Received: 82,265
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi unakuja, pombe, pilau, kanga na fulana!​  Ayub Rioba
  Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo
  Agosti 5, 2009
  [​IMG]

  TUNAHITAJI fikra mbadala katika siasa zetu. Hili ni dhahiri. Nilijaribu kujadili hali halisi ilivyo katika chaguzi zetu na hasa za wabunge. Nikaeleza changamoto na matatizo muhimu yanayotukabili kama taifa.

  Kitu cha msingi ambacho kwa fikra mbadala tunatakiwa kukijadili sasa ni maana ya chaguzi zetu na kama tunaamini ndizo njia ya kutupatia viongozi tunaowastahili na maendeleo tunayoyataka sana.

  Nimejaribu kuonyesha katika udadisi wangu huko nyuma kuwa biashara ya uchaguzi (na ni biashara kweli ukizingatia hongo, fulana, kofia, pilau, pombe, usafiri, n.k. vinavyotawala wakati wa uchaguzi) haiwahakikishii wapigakura kwamba watapata wanachokistahili.

  Katika kampeni, wapiga kura wanapewa ahadi za kitapeli, zikiwamo zisizotekelezeka, au wanapewa fulana, kanga, pombe, pilau, na wao wanampigia kura aliyewanunua. Kinachofanyika leo hakina tofauti na wafanyabiashara ya utumwa kutoka ng'ambo walivyokuwa wakija na kuwapatia machifu na wafanyabiashara wetu shanga, kanzu, kofia, bangili na goroli na wao kupewa binadamu kadhaa kama watumwa.

  Wakati ule; walau bangili iliweza kukaa mkononi miaka kadhaa kuliko fulana ya "chagua fulani" ambayo huwa ni kauka nikuvae na huchakaa ndani ya mwaka au miwili.

  Miaka ya kwanza ya ujenzi wa taifa hili mfumo wa uchaguzi ulilenga kuwapata wawakilishi wa watu. Kama anavyosisitiza Professa Issa Shivji na wanamapinduzi wengine kuhusu jambo hili, wawakilishi wa watu hupatikana kutokana na watu wenyewe na bila kuwepo shinikizo au ushawishi wa rushwa.

  Wawakilishi wa watu hawanyeshi tu kama mvua. Hawashuki tu ghafla kutoka juu na kuwanyeshea watu walio chini na baadaye kuwaacha wakikimbizana kijikinga au kukwepa athari za mafuriko.

  Wawakilishi wa watu ni kama umande. Hainyeshi mvua, hakuna mafuriko, lakini majani yanakuwa na unyevu wake.
  Wawakilishi wa watu unawaona wakiwa na watu wao, wakishirikiana nao, wakisaidiana nao, wakifikiri nao, wakila nao, wakihangaika nao, wakianguka nao na kuamka nao.

  Mfano ninaoutumia sina maana kuwa wawakilishi wa watu ni lazima wawe wanaishi katika nyumba za nyasi kule kijijini na kuendesha maisha yao kama kila mtu pale kijijini. Maana kubwa ya mfano huu ni kwamba wawakilishi wa watu maana yake wanakwenda bungeni kuwakilisha mawazo, changamoto, dukuduku na matarajio ya wale wanaowawakilisha. Lakini pia wanashirikiana na wapigakura wao kukabili changamoto zao pamoja.

  Wawakilishi wa watu wanatakiwa kusikia maumivu wanayoyapata wapiga kura wao na kuchukua hatua za dhati za kuwashirikisha wananchi katika kuyashughulikia.

  Leo hii tunapoelekea katika uchaguzi wa 2,010 hatuna budi kuanzisha na kukuza mijadala itakayowasaidia watu wetu kujua ni nini au nani wanamchagua kuwa kiongozi wao.
  Pamoja na kwamba mijadala hii inawaogopesha baadhi ya watu, njia pekee tuliyo nayo ya kutusaidia kubakia salama kama taifa ni kuhakikisha wananchi wanachukua hatua kama waajiri wakuu wa viongozi hapa nchini kuchagua watu makini na wenye kuitakia heri nchi hii na watu wake wote.

  Nitaeleza kwa ufupi yanayoweza kutokea katika uchaguzi mkuu ujao: Kwanza, wapiga kura wanaweza kuendelea na tabia yao ya kuendekeza tamaa ya vijisenti vya msimu, kanga au fulana. Wanaweza kuendekeza kiu yao ya pombe au soda na njaa ya siku moja wakashiba kwa siku moja na kuchagua kiongozi wa kukaa madarakani miaka mitano.

  Na wapiga kura wetu wanaweza kufanya makosa hayo na kudhani wanaweza kuishi kwa matumaini (kama walivyozoea) hadi uchaguzi mwingine unapokuja wakahongwa tena pilau, pombe, fulana na kanga.
  Wanapofanya hivyo wanakuwa wamehalalisha mambo makuu mawili. Kwanza, wanakuwa wamehalalisha sababu za wao kuonekana majuha kwa sababu hakuna shinikizo la mwakilishi wao kuwajibika ipasavyo.

  La pili, wanakuwa wamehalalisha kuwa na viongozi wanaoweza kuuza nchi na kuwauza hata wapiga kura wenyewe bila wao kujua. Iko hivi. Fursa ya uchaguzi ilikuja kwa wapigakura baada ya miaka mitano. Wao badala ya kuitumia fursa ya uchaguzi kwa umakini na kwa kufikiri vizuri, wakaongozwa na tamaa ya pilau, pombe na vijisenti vya kutumia kwa siku moja au wakahadaika na ahadi hewa.
  Kwa sababu ya kuhadaika, watachagua matapeli, wauza bangi na wenye tamaa ya kujitajirisha wao binafsi. Wakichagua matapeli, basi, wawe tayari kuongozwa kitapeli na wasilalamike. Wajue kuwa wao wenyewe wapiga kura ndio walichagua utapeli.

  Lakini kwa upande wa pili, ni kwamba wapiga kura wa Tanzania wanaweza kuamua kuamka. Wakachukua rungu wanalopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakakaa nalo kipindi cha kampeni hadi siku ya uchaguzi. Wakalitumia kuchagua viongozi kwa umakini wa kipekee. Na ili kujiridhisha kuwa wanachokichagua wanakijua wajiulize maswali yafuatayo:

  Mosi, huyu anayeomba tumchague ni nani? Katokea wapi? Ni mvua au umande? Je historia yake ikoje? Je, ni kwa nini anatuomba tumchague yeye? Je anaahidi nini? Je kinatekelezeka?
  Je, anaamini katika mambo gani kitaifa na ameonyeshaje kuyasimamia kwa dhati hata pale maslahi yake binafsi yalipokuwa hatarini? Je ana msimamo kwa anayoyaamini au ni mtu wa kuyumbayumba kutegemea na maslahi yalipo?

  Pili, huyu anayeomba kura ameifanyia nini nchi yetu au ameufanyia nini ubinadamu kwa ujumla? Je ni wapi na lini katuonyesha kuwa anaweza kuwa kiongozi? Je rekodi yake ya uongozi huko alikotoka ikoje?

  Tatu, huyu anayeomba kura kwetu anatumia njia gani kufanya hivyo? Je anajaribu kutushawishi kwa rekodi yake au na yeye anatutupia vijisenti vya kula leo, fulana, kanga na pilau ili tumchague?
  Je tuna ushahidi gani kuwa huyu anayetuomba kura leo anatuthamini sisi kama watu, kama binadamu, kama wananchi na hatutumii tu kama ngazi ya kupandia kuelekea katika "ulaji" wake binafsi? Je anazifahamu vyema changamoto zetu na jinsi ya kuzikabili au naye pia ana mlolongo tu wa ahadi za kutafutia kura?

  Nne, je ni vigezo gani tutakavyotumia kupima utendaji wake tokea siku ya kwanza tutakapokuwa tumemchagua kuwa kiongozi ili, ikiwezekana, hata kama hajatimiza kipindi chake cha miaka mitano tumuite tumweleze kuwa hatufai na huko anakotupeleka (au asikotupeleka) siko tulikokubaliana kwenda wakati wa uchaguzi?

  Tano, je ni mtu anayejitegemea kimawazo au ni yule tegemezi anayesukumwa na wenye mitaji na maslahi binafsi ili aje agombee ubunge kisha aingie bungeni kutetea maslahi ya waliomtuma?

  Hili la mwisho ni la kujihadhari nalo kupita mengine yote. Leo hii nchi yetu inaelekea pahala ambapo watu wanaweza kutengeneza fedha kupitia ujuha wa wananchi na kisha wakazitumia fedha zile zile kudandia uongozi wa nchi na hatimaye kujihakikishia wao, familia zao na kikundi kidogo wanaendelea kushikilia uchumi na rasilmali za nchi.

  Ujuha wa wapigakura unaweza kutoa uhalali kwa kikundi cha matapeli wachache kuteka nchi halafu kikaanza kuiuza nchi na hatimaye wananchi wenywe. Ipo nchi ya jirani yetu, katika Bahari ya Hindi, ambayo hivi karibuni ilikuwa karibu iuze sehemu kubwa ya ardhi yake kwa nchi moja tajiri eti kwa ajili ya kilimo. Rais wa nchi hiyo alishtuka dakika za mwisho akasitisha uuzwaji ule.

  Huko tunakoelekea, ambako kuna nyang'au wa nje wanaotaka sana kushirikiana na nyang'au wa ndani, tusijeshangaa ikitokea kwamba fedha za kununulia wapigakura wapenda pilau, pombe, kanga na fulana zinapatikana kirahisi na kugawiwa ovyo kwa kila ****. Na baadaye nchi ikajikuta iko rehani au chini ya himaya ya wageni waliotukopesha ili tushinde uchaguzi kwa kununua wapigakura wetu na baadaye tukashindwa kuwalipa.

  Leo hii nchi yetu inashuhudia kujitokeza kwa makundi mbalimbali yanayotoa madai mbalimbali yanayopaswa kushughulikiwa. Mengi ya madai yanayotolewa yana maana na pengine nia nzuri tu. Lakini zipo dalili kwamba baadhi ya madai haya yanaweza kutekwa na matapeli wa kisiasa na wakayatumia katika uchaguzi ujao kuhakikisha wanashinda.

  Na matapeli hao wachache wanaweza hata kuyaombea madai hayo fedha nje ya nchi ili zitumike kununua kura. Ole wao wapiga kura wanaosubiri pilau, pombe, kanga na fulana!
  [​IMG]
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Asante BAK kuweka hii kitu!

  Ayub Rioba uandishi wake ni mzuri, nadhani nakala kama hizi wale wapiga kura wa vijijini ni muhimu sana kujua. Wale waja na pilau ni kuzila na kuwa nyima kura, hasa pale wanapoonekana wanasukumwa na Fisadis ili wakiingia Bungeni watetee maslahi yao.
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kule kwetu unyaluni ni ULANZI,KIMPUMU,komoni na mahindi ya kuchoma
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,640
  Likes Received: 82,265
  Trophy Points: 280
  Masanilo, hiyo signature yako nimeipenda sana. Ahsante sana.
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Watani zangu nyie kumbe ni ovyo kabisa, Mahindi ya kuchoma mnauza shahada za kupigia kura? Kazi kubwa tunayo wapenda mabadiliko
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Unajua wabunge wa kule?? Akina Mwakweta, Yono, Mungai, Galinoma,Makinda uliza wameufanyia nini mkoa wa Iringa watajiuma uma tu hawa kipindi cha uchaguzi iwa wanapita kiulainiiiiiiiiiiiii hakuna upinzani kule.
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hawa ''bwana-shemeji'' ni wahuni sana!

  Siku moja Makambako hapa Makweta aliulizwa na wapiga kura wake ''MBONA UNAKAA MUDA MREFU SANA MADARAKANI HADI UNAZEEKA?KWA NINI USIWAACHIE VIJANA UKAWA MSHAURI?''

  akawajibu-HAKUNA WA KUMUACHIA HADI SASA,WABENA WOOOTE WA NJOMBE HAWAJASOMA!watu wakanuna sana,wakaapa kutompitisha(ndani ya chama)!mzee alisoma alama za nyakati.akauza nyumba moja pale ramadhani AKANUNUA WANACHAMA,wakampitisha!

  tukabaki na maswali tu pale!
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Geoff hivi nikija na container mbili za mahindi ya kuchoma na Ulanzi wa kutosha nakamata Jimbo?
   
 9. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Hapana. Muulize Mwakyembe ana chinja ng'ombe ....
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Teh teh teh mpwa ukitaka upite chinja ng'ombe unyaluni kila kijiji kicha shusha semi trailer la mchele umemaliza kazi baada ya kampeni nunu madebe ya ulanzi na common mapipa kama kumi hivi mzee huna huja yakufanya kampeni rejea we unasonga mbele. Jimbo lako tu.
   
 11. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Geoff;

  Sio Victor Bout ni Marlon Brando kwenye The God father.

  Please rekebisha
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Usiharibu mjadala hapa kijana......unanifatilia kila post vipi umetumwa? .... by the way I do not do men....sorry!
   
 13. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135

  Sasa ina maana kule Bukoba na Moshi wale wasomi na Inshomile kuliko yeyote Tanzania wao wanarubuniwa kwa ndizi??
  Wanyakyusa wa TKY na wangone wa kule PELA MIHO na PELU MUTIMA je wao wanarubuniwa kwa nini maembe?

  Uchovu wa kukubali kula wali ili uliwe kura yako ni tatizo la kitaifa, tatizo siyo ulanzi kimpuni wanzuki, kangara au togwa! Hivyo ni vyakula. Tatizo ni upeo wetu kama Watanzania.

  Amen.
   
 14. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Unajua ukishaishiwa hoja unaleta vioja. kwani sio kweli kuwa Mwakyembe hachinji ng'ombe?

  Sasa matusi ya nini?.

  Huwezi kumwazia mwenzio mwizi kama wewe sio mwizi! mbona tunasikia unaishi kwa namna hiyo USA?, unafikiri ni siri?
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  This is a second warning! Keep on....

  Its my life in Texas nipe heshima yangu, kila ninachopost lazima usome vipi wewe mara ubadili ID utukane nakupa thanks bado.....unakuwaje ndugu ....!
   
 16. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Madela wa madilu;

  Mzee ES aliwahi kusema viongozi wetu ni reflection ya sisi wenyewe. Wa Tanzania tunaendekeza njaa kweli. Toka CCM ilipokubali TAKRIMA itolewe watu (viongozi) wanaitumia vibaya sana. Kwa kweli mie sioni kwanini kiongozi AFANYIWE SHEREHE lakini NG'OMBE WA KULIWA anunue yeye.

  Hapo ndo nachanganyikiwa na wa TZ. Hiyo sio Takrima ni Rushwa kwa mtazamo wangu especially unapoitoa kwa wananchi ambao sio wa UKOO wako wala ndugu wala marafiki zako.

  Ni mtizamo wangu tu.
   
 17. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kizazi kiwazacho kujenga familia, jamii na taifa kwa kupokea na kutoa rushwa kamwe hakiwezi kuvunja nguvu za mtandao wa rushwa.
  Rushwa si tatizo la viongozi au watu wa kabila au watokao sehemu fulani kama kusini kaskazini mashariki au magharibi.
  Rushwa Tanzania ni tatizo la watanzania wote, wale wpingao rushwa na wale waikumbatiao rushwa.
  Kupinga rushwa bila kuvunja msingi wa utamaduni wake , mapokeo na mazingira yake ni kazi bure. Rushwa iko katika kila kilenge cha maisha. Rushwa ipo hata miongoni mwa wachunga kondoo wa bwana, wanasiasa na hata mashabiki wa soka.
  Rushwa ina sura nyingi zenye ukinyonga wa kuwarubuni hata wale wajifanyao wako mstari wa mbele kuipinga.

  Kwanza tukubali kwamba rushwa ni tatizo letu Watanzania wote, lakini huonekana zaidi kwa viongozi kuliko kwetu wananchi wa kawaida.
  Pili lazima tukubali kwamba Rushwa ni tatizo la kiutamaduni na kimapokeo" mkono mtupu haulambwi".
  Tatu ni lazima tukubali kwamba kwa namna moja au nyingine maisha yetu ya kila siku yanathiriwa na rushwa iliyotokea mahali fulani miongoni mwa ndugu au marafiki wetu wa karibu, na kinachoitwa mafanikio katika maisha yetu kwa namna fulani msingi wake umejaa matofari na mawe ya rushwa.
   
 18. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Sababu kubwa ya rushwa kutoisha ni viongozi wenyewe wa juu, waliingia madarakani na rushwa; watamaliza vipi rushwa?
   
 19. E

  Edwin Mtei JF Gold Member

  #19
  Aug 15, 2009
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nimeamua kuchangia mawazo kuhusu Uchaguzi Mkuu ujao, na naanza kwa kuwapongeza kwa dhati wazalendo wenzangu, Bubu Ataka Kusema na Ayub Rioba, kwa kuibua masuala la rushwa na takrima ya kupindukia, yaliyokithiri katika Uchaguzi Mkuu uliopita na chaguzi ndogo zote zilizofanyika baadaye. Nahofia kwa dhati kwamba chaguzi za aina hii zisipokoma, maendeleo yetu yataathirika sana.

  Natambua kwamba wanaharakati wa demokrasia ya kweli tulifaulu kuifanya Mahakama Kuu kutamka kwamba takrima ile ilikiuka Katiba ya Tanzania na ni marufuku kuitumia katika uchaguzi. Licha ya kwamba Katiba haikuweza kutumika kutengua uchaguzi wa wale waliochaguliwa kinyume na Katiba, nilitegemea kwamba Serikali na Bunge wangeandaa mabadiliko ya sheria na taratibu ili kudhibiti na kuzuia takrima na rushwa za aina zilizopigwa marufuku.

  Ninachotaka kupendekeza sasa ni kwamba Serikali na Bunge, kwa kujiandaa kwa uchaguzi ujao, wapitishe sheria na taratibu hizo. Najua kwamba Rais hivi karibuni, ametangaza kwamba Sheria ya kutenganisha "siasa na biashara" inaandaliwa. Lakini hili ni suala tofauti na suala la wanasiasa kuhonga wapiga kura. Bado wananchi wenye upendo na nchi yao ya Tanzania, tunasubiri sheria kali na taratibu za wazi, kupiga marufuku na kuzuia hongo na takrima katika uchaguzi.

  Jambo ambalo linahusiana sana na uchaguzi huru na wa kidemokrasia, ni kuundwa upya Tume huru ya Uchaguzi taifa (National Electoral Commission). Hii imepigiwa kelele na wanaharakati kwa muda mrefu. Lakini, sio tu wajumbe wa NEC ni wale wale wanaendelea. bali hata Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wameipiku Serikali ya Muungano kwa kuwa na Tume (ZEC) inayoshirikisha wajumbe toka CUF na CCM.

  Tume ya Muungano, NEC, imeendelea kuonesha upendeleo wa wazi kwa wagombea wa chama tawala ktk chaguzi ndogo. Mifano ya Tarime, Busanda na Biharamulo Magharibi kulikofanyika chaguzi ndogo hivi karibuni, ilidhihirisha haja ya mabadiliko.

  Pendekezo ninalotaka WanaJF walifikirie na kulivalia njuga, sio tu kwamba NEC iundwe upya, bali taratibu za kusimamia uchaguzi katika majimbo zihakikishe kwamba zina wasimamizi huru na wasiopendelea upande wowote (neutral and independent).

  Inavyofahamika, sasa NEC hutumia Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya, miji au manispaa kama ndio wasimamizi wa uchaguzi (Returning Officers). Hawa ni watumishi wa Serikali na mara nyingi ni wakereketwa wa chama tawala.

  Hata pale Returning Officers wanapojaribu kuonyesha kutekeleza matakwa ya sheria ya uchaguzi kwa kutopendelea upande wowote, mabingwa wa siasa wang'ang'anizi wa madaraka huwatisha kwamba watawafukuza kazi au kuwaadhibu endapo hawahakikishi ushindi kwa wateule wao. Mifano ni ile ya Busanda na Biharamulo Magharibi ambapo viongozi wa CCM waliwatisha hadharani wale wasimamizi.

  Kwa hiyo pendekezo langu ni kwamba NEC iajiri wasimamizi wapya kila tunapokuwa na Uchaguzi. Tume ihakikishe ni watu neutral and independent, wasioweza kupendelea upande wowote. Watumishi hao wa muda wapewe mafunzo juu ya Sheria na taratibu za uchaguzi (intensive orietation course) na watakapo kamilisha zoezi la uchaguzi waachishwe kazi au warudie mashughuli yao ya awali.

  Natarajia kwamba NEC huru na mpya itaweza kuajiri temporarily, baada ya proper interview, watu waadilifu na huru ambao hawatazidi 1000 ambao watatukwamua kutoka tatizo hili la kuwa na wasimamizi wa uchaguzi wanaopendelea au wasioaminika. Hakuna tatizo la fedha za kuwalipa kwa vile hata kwa mpangilio wa sasa hawa Wakurugenzi wa Halmashauri hulipwa na Tume kwa kipindi cha uchaguzi.

  Watu waadilifu wanaweza kupatikana miongoni mwa watumishi wa dini au wanafunzi wa vyuoni wanaotarajia kuingia katika fani kama hizo. WanaJF wanaweza kupendekeza taratibu nyingine za kupata watu wanaofaa kwa kazi hii.

  Hata kukitokea ulazima wa kuwa na uchaguzi mdogo, NEC inaweza kuajiri watumishi wa muda ambao wataaminika. Hawa Wakurugenzi wa Halmashauri waendelee na majukumu yao ya kawaida na kamwe wasihusishwe na uchaguzi wa kisiasa.

  Edwin Mtei
   
  Last edited: Aug 15, 2009
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Aug 16, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,640
  Likes Received: 82,265
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana Mzee Mtei kwa pongezi zako. Pia nakuomba sana pamoja na shughuli zako nyingi ujitahidi kuchangia katika mijadala mbali mbali hapa ukumbini hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi wa 2010.

  CCM sasa hivi wanajua fika bila kutumia rushwa za pilau, pesa, pombe, fulana, kanga, magodoro n.k. pamoja na vyombo vya dola kuwanyanyasa kwa namna moja au nyingine wanachama wa vyama vya upinzani na Viongozi wao basi hawawezi kushinda katika majimbo mengi sana Tanzania.

  Nakubaliana nawe kuhusu kuwatumia Wakurugenzi wa halmashauri za Wilaya, Miji na Manispaa kwamba hawa wote siku zote maamuzi yao yatakuwa yanaegemea zaidi upande wa CCM tu.

  Kwa maoni yangu NEC ni kama kitengo cha CCM hawako huru kabisa katika maamuzi yao hasa pale ambapo taratibu za uchaguzi zinapokiukwa. Kulikuwa na ushahidi wa kutosha kabisa kuhusu taratibu mbali mbali zilizokiukwa za kutoa rushwa za aina mbali mbali kule Tarime, Busanda na Biharamulo na pia kutimika kwa vyombo vya dola kuwanyanyasa wanachama wa vyama vya upinzani na viongizi wao, lakini NEC iliamua kufumba macho kabisa na kutokukemea kabisa kasoto hizo.

  Kuna haja ya vyama vya upinzani kuhakikisha wanakuwa na sauti moja katika kuishinikiza Serikali ili NEC iundwe upya kabla ya 2010 na kuhakikisha inakuwa huru katika maamuzi yake vinginevyo pamoja na kasoro kubwa zitakazojitokeza katika uchaguzi wa 2010 lakini NEC wataangalia pembeni na kusema kwamba uchaguli ulikuwa huru na hivyo uongozi wa nchi yetu kuendelea kuwa mikononi mwa mafisadi.
   
Loading...