Uchaguzi Umekwisha Sasa Twende Tukafanye Kazi


Ndallo

Ndallo

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Messages
7,294
Likes
1,415
Points
280
Ndallo

Ndallo

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2010
7,294 1,415 280
Watanzania ni watu wanaopenda saana kupiga soga. Na hakuna kipindi ambacho michapo huwa mingi mitaani kama kipindi cha uchaguzi. Kwa bahati nzuri, kampeni za kuwania uraisi,ubunge na udiwani hatimaye zimemalizika salama pamoja na kuwepo na rabsha za hapa na pale.

Nafahamu kwamba kuna mengi ya kunzungumza baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo. Hata hivyo tunapaswa kukaa tukikumbuka kazi iliyo mbele yetu. Kwa wenzetu wa nchi zilizoendelea mara kampeni zinapomalizika watu husahau haraka na kuendelea na mambo ya kujenga uchumi. Ningefurahi kama watanzani tungeiga mfano huu wa wenzetu wa nchi zilizoendelea. Uchaguzi unapokwisha, watu wanatakiwa kuyapa umuhimu mambo yanayosumbua nchi zao na maisha yao. Tupunguze muda wa kupiga soga maofisini kwetu na katika sehemu za kutafutia riziki. Hii ndio njia pekee ambayo nchi yetu inaweza kujikwamua kutoka katika umasikini.

Tupunguze kulalamika na kuzungumza tu bila ya kufanya kazi. Uchaguzi umekwisha, tufanye kazi kwa bidii na tujiandae na uchaguzi wa mwaka 2015.:thinking:
 

Forum statistics

Threads 1,236,906
Members 475,327
Posts 29,271,945