Uchaguzi umekwisha- igunga wamemchagua au wamechaguliwa mbunge?????


kinepi_nepi

kinepi_nepi

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2007
Messages
870
Likes
5
Points
0
kinepi_nepi

kinepi_nepi

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2007
870 5 0
Uchaguzi ni demokrasia mwanadamu anayoitumia kumchagua kiongozi anayempenda. Demokrasia hii imekuwepo tangia zama za kale. Pale pasipo na kuchagua kwa uhuru tunaita udikteta ambapo viongozi wote wa jamii wanatoka kwa kauli ya mtu au kikundi kichache cha watu.

Uchaguzi Igunga umekwisha mbunge aliyetangazwa na NEC ni wa upande wa chama cha mapinduzi, hivyo ndivyo imekuwa tunapenda hatupendi, ni haki si haki, kachaguliwa au kateuliwa ndiye aliyetangazwa kwa mujibu wa sheria zetu. Manung'uniko yetu wala vilio vyetu haviwezi kumtoa pale alipo isipokuwa kwa mahakama tu.

Wakati wa kampeni tumekuwa tukilalamika kwamba taratibu na kanuni za uchaguzi zimevunjwa na wapiga debe, mgombea au wapambe wa CCM. Kanuni hizi ni zile za maadili ya uchaguzi, sheria za uchaguzi na nchi, uvunjifu wa katiba.

Ninaamini muda wa lkulalamika kila mwaka ufike mwisho, tuanze kupeleka malalamiko yetu mahakamani, hata tukishindwa hata kama tunawasiwasi na mfumo wa kimahakama, wakati umefika wa kupeleka kila lalamiko letu mbele ya sheria ili mahakama zitafsiri sheria nasi tujue sheria zinavyotafsiriwa na mahakama hizi.

Wote waliopigania haki, demokrasia ya kisiasa na kiuchumi kamwe hawakuchoka kwenda mbele ya mahakama kushita na kufungua kesi. Historia inaonyesha siku moja kutatokea majaji wasiopenda dhuluma na uonevu watakubali kutafsiri sheria kama inavyotakiwa. Hatuwezi kupata haki kwenye sanduku la kura ambalo kila mwaka linamazingaumbwe.

Wakati umefika wa kuchangisha fedha nyingi kwa ajili ya kufungua kesi zote ambazo watawala, au wapambe au washika pembe wao wanapovunja sheria kwa makusudi. Tuwe tayari kupambana na sheria huku tukiendeleza siasa za kuelimisha umma. Lazima utawala zalimu ubanwe kila kono.

Igunga kulikuwa na malalamiko na matumizi mabaya ya fedha, vyeo, mamlaka na utawala ili kushinda. Tukinyamazia haya mambo hizi zitaonekana kelele za kila siku mwisho wa siku zitakuwa zinapuuzwa. Kama hakuna la kupeleka mahakamni hakuna haja ya kulalamika kwani ni fair game. Upande wa pili na watatu wanalalamika, CDM wanalalamika lazima mmoja awe tofauti.

Nawaomba Viongozi wangu wa CDM wawe tayari kutumia mahakama hata kama kuna wasiwasi wa kuegemea upande wa CCM kama polisi wanavyojidhihirisha. Tukipeleka kesi zenye mashiko na ushahidi usio na mashaka hata hao majaji wa kijani wataona aibu. Ila kulalamika na kujiona mnyonge haisadii wala sio uajsiri wa kupigana vita na mkolono mweusi. Ikumbukwe kuna majaji nao hawapendi kupindisha sheria sio wote wamewekwa mfukoni mwa CCM.

Tuanze na Igunga kila alikiuka taratibu au maadili apelekwe mbele ya sheria.
 
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
81
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 81 145
hawajaweza kusema kuwa kura 171,000 zimekwenda wapi? sababu ndizo zilizo watu waliojiandikisha na kura 50,300 ndizo zilizopigwa

kwahiyo CCM iliishida Chadema kura 3,000 tu kweli ni kura zilizopigwa au ni hizo kura zilizopotea? CCM wajanja wanakila kitu

No DEMOCRACY...
 
Vin Diesel

Vin Diesel

JF Gold Member
Joined
Mar 1, 2011
Messages
8,671
Likes
1,182
Points
280
Vin Diesel

Vin Diesel

JF Gold Member
Joined Mar 1, 2011
8,671 1,182 280
Kazi zikikosekana watu wanaanza andika upupu tu...
 

Forum statistics

Threads 1,236,300
Members 475,050
Posts 29,253,365