Uchaguzi uliofanywa na CUF haukuzingatia vigezo, wamepeana tuu.

Manjii

New Member
Nov 6, 2016
3
0
Kwa masikitiko makubwa mno nimesikitishwa kwa namna Baraza la cuf lilivyoteua majina ya wabunge wa viti maalum waliochukua nafasi ya waliotenguliwa bila ya kujali ya kuwa wapo wagombea wanaostahili kupewa nafasi kwa ajili ya maslahi ya Taifa na chama kwa ujumla.

Nimeshangazwa kuwaona baadhi ya walioteuliwa wasio na vigezo na wengine walishawahi kutumika kwa nafasi hii bila faida yoyote tena kwa awamu 2 mfululizo.

Hiki ni kitu kibaya chenye kukatisha tamaa na mapenzi kwa chama, maana ipo wazi ya kwamba majina yalioteuliwa wamejipa nafasi wenyewe. Eti viti maakum wawili watoke kwenye Kanda moja( mkoa) ina maana hakuna wagombea wengine wenye sifa kutoka kanda nyingine.

Ki ukweli tunakipenda chama chetu lakini walio wengi wanajali maslahi binafsi na sio chama na Taifa.
NEC nayo imeshindwa kujadili kwa umakini juu ya majina ya wagombea kabla ya kuwatangaza. Wapo wagombea wenye kustahili katika nafasi hii na wale ambao walishatumika kwenye nafasi hi wangepisha wenzao kuweza kupata changamoto na hamasa ya maendeleo.

Uteuzi uliopitishwa ni wauonevu wa wazi wazi kabisa na wenye kuchochea upotevu wa imani juu ya uongozi na Baraza lililopo.

Rai yangu ni kuwaomba NEC kuzingatia Sana vigezo kwa wagombea na chama kizingatie wagombea wapya walio na mapenzi ya dhati na chama chetu na Taifa kwa ujumla wapewe nafasi ya kutuongoza na sio kuwapa watu waliotumika.

Watu wanapoteza imani sasa na kuona kuwa hawashindwi ila wanaondolewa maana vigezo wanavyo na wamekuwa wakigombea mara kadha wakadha bila ya mafanikio.

Tuitende ilio haki katika chaguzi zetu bila ya upendeleo wowote kwa manufaa ya chama na Taifa kwa ujumla Kama ilivyo sera yetu ya HAKI KWA WOTE, maana bado naona Giza kubwa limetanda ndani CUF.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majina sahihi ya Wateule:-
1. Alfredina Kahigi----Bukoba
2. Zainabu Mdolwa--Handeni Tanga
3.Nuru Awadh Bafadhili-Tanga mjini 4.Sonia Jumaa-------DSM.
5.Hindu Hamisi Mwenda-Tbra 6.Shamsia Azizi---------Mtwara 7.KizaHussein Ahmed-Kigoma
8.Rukia Kassim-------ZnZ.

Majina ni hayo kanda kati hakuna.
Jina namba 3. Nuru lilishatumika awamu zilizopita kwa miaka 10 pia ni mjumbe wa baraza kuu.

Jina la 2 na 3 wanatoka Kanda moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa masikitiko makubwa mno nimesikitishwa kwa namna Baraza la cuf lilivyoteua majina ya wabunge wa viti maalum waliochukua nafasi ya waliotenguliwa bila ya kujali ya kuwa wapo wagombea wanaostahili kupewa nafasi kwa ajili ya maslahi ya Taifa na chama kwa ujumla.

Nimeshangazwa kuwaona baadhi ya walioteuliwa wasio na vigezo na wengine walishawahi kutumika kwa nafasi hii bila faida yoyote tena kwa awamu 2 mfululizo.

Hiki ni kitu kibaya chenye kukatisha tamaa na mapenzi kwa chama, maana ipo wazi ya kwamba majina yalioteuliwa wamejipa nafasi wenyewe. Eti viti maakum wawili watoke kwenye Kanda moja( mkoa) ina maana hakuna wagombea wengine wenye sifa kutoka kanda nyingine.

Ki ukweli tunakipenda chama chetu lakini walio wengi wanajali maslahi binafsi na sio chama na Taifa.
NEC nayo imeshindwa kujadili kwa umakini juu ya majina ya wagombea kabla ya kuwatangaza. Wapo wagombea wenye kustahili katika nafasi hii na wale ambao walishatumika kwenye nafasi hi wangepisha wenzao kuweza kupata changamoto na hamasa ya maendeleo.

Uteuzi uliopitishwa ni wauonevu wa wazi wazi kabisa na wenye kuchochea upotevu wa imani juu ya uongozi na Baraza lililopo.

Rai yangu ni kuwaomba NEC kuzingatia Sana vigezo kwa wagombea na chama kizingatie wagombea wapya walio na mapenzi ya dhati na chama chetu na Taifa kwa ujumla wapewe nafasi ya kutuongoza na sio kuwapa watu waliotumika.

Watu wanapoteza imani sasa na kuona kuwa hawashindwi ila wanaondolewa maana vigezo wanavyo na wamekuwa wakigombea mara kadha wakadha bila ya mafanikio.

Tuitende ilio haki katika chaguzi zetu bila ya upendeleo wowote kwa manufaa ya chama na Taifa kwa ujumla Kama ilivyo sera yetu ya HAKI KWA WOTE, maana bado naona Giza kubwa limetanda ndani CUF.

Sent using Jamii Forums mobile app

Pia ni vyema ukajua kuwa uteuzi wao uko Kisheria, na NEC inaangalia kama wamekidhi Sifa za kuwa wabunge Viti maalum hili jambo lisiwekewe ushabiki, tusome Katiba na Sheria zetu kwani na hilo nalo ni gumu?
 
Wale walioteuliwa na le propesa ni wanachama wa CCM si CUF...
tunawatambua kwa mioyo yao si miili yao Mkuu alitufahamisha namna ya kuwatambua kama yule mbunge wa Kalimaua
 
Back
Top Bottom