Uchaguzi ukiitishwa leo, je mbunge wako atarejea bungeni kukuwakilisha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi ukiitishwa leo, je mbunge wako atarejea bungeni kukuwakilisha?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Karibuni masijala, Sep 24, 2012.

 1. K

  Karibuni masijala JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wadau hebu kwa nafasi yako katika jimbo lako mbunge anastahili kurejea Bungeni kuendelea kukuwakilisha kama ukiitishwa uchaguzi. Tuwe wa kweli kwa kuwachambua jinsi wametumika kwa miaka miwili itawasaidia kwa miaka mitatu iliyosalia kujitadhimini na wewe kunufaika kwa uwajibikaji wao kwa jinsi ulivyo jenga hoja kwenye maoni yako. Taja jina la mbunge na jinsi na maoni yako ya jinsi amelitumikia jimbo. Mimi mbunge wangu ni Nasari kwa kipindi kifupi sijaridhishwa na utendaji wake jimboni kwani mpaka sasa kata ya Ngarenanyuki na nyingine sijaona utekelezaji wa Ilani na ushiriki wake kutatua changamoto au kuhamasisha maendeleo jimboni kwa mkakati kama Watanzania wangekuwa wanampigia kura angeshinda kwani michango yake kwa mtazamo wa kitaifanaikubali bali katika ngazi ya jimbo hajatambua ni mtihani kwa kipindi kifupi alichopewa angejihusisha sana na shughuli za jimbo kwani watakaomtadhimini ni wanajimbo. Je wa kwako kijimbo unasemaje mwambie asisahishe na kama mchapa kazi mtiye moyo. Ahsante kwa hoja makini na za ukweli.
   
 2. K

  Karibuni masijala JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Changamoto za majimbo zinatatulika pia kwa kuwa na viongozi ambao wanajua kuongoza ni kuonyesha njia. Wangea ndaa mipango (Progamme) za jinsi ya kutatua matatizo ya kimitaa, kata na jimbo. Kwa mfano leo wanambezi wanalalamika uharibifu wa wazingira hasa mto mbezi, Mbunge angetumia fedha za mfuko wa jimbo kuandaa program itakayowashirikisha wanambezi wa maeneo yaliyokando kando ya mto kupanda miti inayozuia mmomonyoko wa udongo, wakazi hao wangeilinda na kuenzi mchango huo huku mbunge akiweka alama mioyoni mwao haitafutika miaka na miaka wameshindwa kununua hata miti 500 wakahamashisha walengwa kujitoa. Nilifurahishwa sana siku niliona taarifa chama cha Chadema ngazi ya Tawi kuwakusanya wanachama wakatatua matatizo ya mtaa siku hiyo waliamua kusafisha mazingira kufukua mitaro iliyoziba. Hebu kila mbunge atembelee matawi washirikiane na wanachama wa mitaa kubainisha changamoto za mitaa hiyo na kuona namna wanaweza kuzitatua kwa kuwashirikisha wanamtaa. Hebu fanyeni mambo ambayo serikali haijaona au inasua sua kwenye mitaa, kata na jimbo yaliyokwenye uwezo wenu yasiyotatulika yanahitaji nguvu ya Serikali mjumbe ajulishwe akaseme bungeni. Mmekuwa watu wa kuwalisha sana watu waneno badala ya kuonyesha njia kwa matendo katika nyanja ya mazingira, uchumi, kijamii. Mbunge atakayedhaminika miaka ijayo ni yule atakayefanya nuia kuweka historia kwenye jimbo kwa ukuandaa mikakati ya kutatua kero za wanajimbo wengi wametafuta historia kwa maneno yao bungeni vyombo vya habari na mikutano wachukue hatua kuwa wa kimatendo zaidi kwenye mitaa, kata na jimbo.
   
 3. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Wangu keshapiogwa chini tunasubiri tume ya uchaguzi iitishe uchaguzi jimbo letu
   
Loading...