Uchaguzi u-NEC CCM Musoma vurugu; Bahasha za 'mshiko' zamwagwa kama njugu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi u-NEC CCM Musoma vurugu; Bahasha za 'mshiko' zamwagwa kama njugu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 29, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMAMOSI, SEPTEMBA 29, 2012 08:51 NA MWANDISHI WETU, MUSOMA

  *Mgombea aahidi kumwaga baiskeli
  *Bahasha za ‘mshiko’zamwagwa kama njugu

  UCHAGUZI wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma Mjini, unaotarajia kufanyika kesho, umeanza kughubikwa na vitendo vya rushwa.

  Habari za kuaminika zilizopatikana kutoka mjini Musoma, zinasema mmoja ya wagombea wa nafasi ya u-NEC anadaiwa kutoa posho kati ya Sh 50,000 hadi Sh 100,000 kwa kila mjumbe katika kata saba za Musoma mjini.

  Tukio hilo ambalo linadaiwa kuratibiwa na wapambe na mmoja ya watoto wa mgombea huyo,lilifanyika juzi kwa nyakati tofauti baada ya mgombea huyo kuzungumza na wajumbe hao.

  Habari za kuaminika ambazo, zimelifikia gazeti hili,zinasema mkutano wa kwanza ulifanyika juzi mchana katika Kata ya Nyakato, ambapo baada kumalizika tu wajumbe waliombwa kuonana na watu watatu, akiwemo mtoto mkubwa wa mgombea huyo kwa ajili ya kupewa posho.

  “Tulipewa fedha zikiwa kwenye bahasha, lakini nilipokwenda kufungua nilikuta zimo Sh 100,000, lakini mwenzangu alikuwa amewekewa Sh 50,000,inaonekana posho hizi zilitolewa kwa kuangalia sura”alisema mmoja ya wajumbe hao (jina tunalo).

  Alisema baada ya baadhi ya wajumbe kugundua wamelipwa fedha kidogo tofauti na wenzao, walishinikiza kuongezwa, kitendo ambacho hakikukubaliwa kwa maelezo kuwa watalipwa fedha nyingine usiku wa kuamkia Jumapili.

  Kwa mujibu wa habari hizo, baada ya kikao hicho kumalizika huku wajumbe wengine wakiondoka na kinyongo,kiliitishwa kikao kingine katika Kata ya Kitaji.

  Imedaiwa katika kikao hicho,mgombea huyo aliwaomba wajumbe kumchagua yeye kutokana na mchango wake katika chama, huku akitoa ahadi ya kutoa baiskeli kwa kila mjumbe kama akifanikiwa kuchaguliwa.

  “Mimi ni mwenzenu tumekuwa hapa wote,naomba msiniangushe, lakini nitawapa zawadi ya baiskeli kwa kila mjumbe,pikipiki kwa kila ofisi ya tawi kwa ajili ya viongozi wetu na kuimarisha chama”.

  Mgao huo,unadaiwa kufanyika katika kata za Nyosho,Iringo,Kigera,Kamnyonge,Bweri na Nyamatare.

  Hata hivyo, imedaiwa baada ya mgao huo wa fedha kwa kuangalia sura kumeleta mgawanyiko mkubwa kwa wajumbe, ambapo imemlazimu mgombea huyo usiku wa kuamkia jana, kurudi katika kata hizo kwa ajili ya kusawazisha hali ya hewa huku akitoa ahadi ya kutoa sehemu ya fedha hizo usiku wa kuamkia jumapili.

  Akizungumza na gazeti hili,mmoja ya watu ambao wako karibu na mgombea huyo,alisema wamepanga siku ya jumamosi kuamkia jumapili kugawa Sh 150,000 kwa wajumbe 200 tu ambao watakuwa na uhakika wa kuwapati ushindi huo.

  Kata 13 za Musoma Mjini, zinatajwa kuwa na wajumbe kuanzia 25 hadi 50 wa Mkutano Mkuu, ambao watarajia kupiga kura katika mkutano huo.

  Wagombea katika uchaguzi huo, ni Madari Kerenge,Dora Jama,Lenard Ismail Kitwala na Vedastus Mathayo anayetete nafasi hiyo.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Utamu wa MADARAKA ni KUTOA PESA na ZAWADI...

  Sasa hao Wajumbe Wnaogombea, ni wapi wanapata hizo PESA ? Wanaiba ? ni VIJANA Wajameni...

  Ukiangalia kwao Wana Nyumba za MAKUTI na Wazazi hawana MAJI safi na TAA.. Ni wapi wanapta hongo?

  Ndio, huyu kiongozi kijana wa KIKWETE ataongoza bila kuchota MALI???

  (
  SAMAKI HUKUNJWA ANGALI MBICHI) WIZI MTUPU!!!
   
 3. T

  TATOO Senior Member

  #3
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliekuwa mbunge wa musoma mjini VEDASTUS MATHAYO anatolewa jasho kwenye nafasi ya ujumbe wa NEC mkoa na aliyekuwa diwani wake kipindi cha ubunge wake ndugu MADALI aliyekuwa diwani wa kata ya mwigobero,,,kwa habari za uhakika ni kwamba Veda ana hali mbaya sana kwenye kampeni na uchaguzi ni kesho tutazidi kujuzana wana jamvi...............
   
 4. T

  TATOO Senior Member

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UCHAGUZI wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa CCM (NEC) na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma mjini, umeingia dosari baada ya mmoja wa wagombea kushutumiwa kutoa rushwa ya kati ya sh 50,000 na 100,000 kwa kila mjumbe katika kata saba za Musoma mjini.

  Tukio hilo ambalo linadaiwa kuratibiwa na wapambe na mmoja ya watoto wa mgombea huyo, lilitokea juzi baada ya mgombea huyo kuzungumza na wajumbe hao.

  Habari za kuminika ambazo zimelifikia gazeti hili zilidai mkutano wa kwanza ulifanyika juzi mchana katika kata ya Nyakato ambapo baada kumalizika wajumbe hao waliombwa kuonana na watu watatu akiwemo mtoto wa mgombea huyo kwa ajili ya kupewa fedha hizo kama posho.

  "Tulipewa fedha zikiwa kwenye bahasha na nilipofungua nilikuta sh. 100,000, lakini mwenzangu alikuwa amewekewa sh 50,000 sasa inaonekana zile posho zilitolewa kwa kuangalia sura," alisema mmoja ya wajumbe hao.

  Hata hivyo, alisema baadhi ya wajumbe waliopewa fedha ndogo tofauti na wenzao walishinikiza kuongezwa kitendo ambacho hakikubaliwa kwa maelezo kuwa watalipwa fedha nyingine usiku wa kuamkia Jumapili ya uchaguzi huo.

  Kwa mujibu wa habari hizo, baada ya kikao hicho kumalizika huku wajumbe wengine wakiondoka na kinyongo, kiliitishwa kikao kingine katika kata ya Kitaji.

  Imedaiwa katika kikao hicho, mgombea huyo aliwaomba wajumbe kumchagua yeye kutokana na mchango wake katika chama huku akitoa ahadi ya kutoa baiskeli kwa kila mjumbe baada ya uchaguzi.

  Mgombea huyo kupitia kwa vijana wake aliwapa wajumbe wa kikao hicho kile kilichoitwa posho kati ya sh 20,000 na 100,000.
  Mgao huo wa fedha pia ulifanyika katika kata za Nyosho, Iringo, Kigera, Kamnyonge, Bweri na Nyamatare.

  Hata hivyo, imedaiwa baada ya mgao huo fedha kwa kuangalia sura kuleta mgawanyiko mkubwa kwa wajumbe, imemlazimu mgombea huyo usiku kucha kuamkia jana kurudi katika kata hizo kwa ajili ya kusawazisha hali ya hewa huku akitoa ahadi ya kutoa sehemu ya fedha hizo usiku wa kuamkia Jumapili.

  Akizungumza na gazeti hili, mtu aliye karibu na mgombea huyo, alikiri kuwepo kwa fedha zilizoandaliwa kwa ajili ya kuwapa wapigakura wajumbe 200 tu ambao watakuwa na uhakika wa kuwapa ushindi huo.

  Wagombea wa nafasi hiyo katika wilaya ya Musoma Mjini ni Madari Kerenge, Dora Jama, Lenard Kitwala na Vedastus Mathayo anayetete nafasi hiyo.
   
 5. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  na minoti huyu?
   
 6. Nzenzu

  Nzenzu JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mapesa yake yanafanyakazi gani?
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,246
  Trophy Points: 280
  kumbe nec ni fweza yako tu? Angechukua mkopo bank, italipa mbele kwa mbele
   
 8. T

  TATOO Senior Member

  #8
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapa lazima aliye na not zake kwani 2010 hizo not hakuwa nazo?
   
 9. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Niko sebuleni naangalia taarifa ya habari itv kuna mgombea analalamika kutotendewa haki na mwingine analalamika kutekwa na wafuasi wa mgombea wa nec taifa.Najiuliza kama watoto wa familia moja wanafanyiana hivyo je inakuwaje kwa watoto wa familia nyingine inakuwaje?.
   
 10. commited

  commited JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hali imekuwa mbaya sana musoma, katika uchaguzi wa ccm, ambapo rushwa na ugawaji pesa ulifanyika waziwazi, na hakuna cha takukuru wala nini? Lakini kibaya zaidi hata silaha za moto zilitumika kumteka mmoja wa mgombea kabla ya muda mchache kupiga kura, na hatimaye mathayo david ametengazwa mshindi.. Hiyo ndiyo ccm source itv news saa 2.00 usiku leo
   
 11. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,737
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nimemsikia huyu jama na amelala mika sana kuwa alitekwa muda mrefu lakini hata polisi hawakwenda kumsaidia!

  Alisisitiza pamoja na ahadi za rais kumwaga watu wa kuzuia rushwa lakini hakuna Pccb aliyekuwepo na pesa ziligawiwa kama njugu!

  Hizi ndio siasa safi za sisiemu walizo zoea!
   
 12. j

  joyous Member

  #12
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  ligamba Tendwa liko wapi? mbona halitoi kauli ya kuifuta nyinyiem! au atasema ni vurugu ya ndani kwa ndani!! kumbe alikuwa anatafuta kibanzi kwa cdm wakati kuna bonge la boriti/banzi kwenye jicho la nyinyiem!!
   
 13. commited

  commited JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  ccm inasikitisha sana, na ndio maana hata wakina chenge na wenzake, ni mwendo wa rushwa tu na ndio waliochaguliwa nec... Mwalimu aliwahi kusema Rushwa ni adui wa haki.. lakini sijui ccm wanaakili gani,yaani sasa hivi ukiwa mwizi wa mabilions wewe ndiye mtu na wewe ndiye unatakiwa sisiemu.. NAPE SIJUI ATAKANUSHA NA HAYA, ATASEMA HAO WAGOMBEA WANAO LALAMIKA NI OIL CHAFU-, WANANCHI WANAJIONEA HAYA... RIP CCM, DEVIL AMEKUPENDA ZAIDI, KUFA CCM NA WAFUASI WAKO WOOTE;
   
 14. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Tendwa kawekwa pale karibia na magogoni na nani, chezea wakurya wewe
   
 15. b

  blueray JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hata mi nimeona ITV, inasikitisha sana. Nadhani hata Tendwa, Saidi Mwema na Hosea wameona au kusikia. Kama hawana taarifa wataambwiwa na Nape. Ngoja tusubiri watasemaje...
   
Loading...