Uchaguzi TLS : Wakili Fatma Karume aka Shangazi kutogombea tena Urais Wa TLS

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,516
Chama cha Wanasheria wa Tanganyika almaarufu kama TLS kinatarajia kufanya mkutano wake mkuu wa mwaka mwezi wa nne jijini Arusha. Moja kati ya masuala yatakayofanyika ni pamoja na uchaguzi katika nafasi za Urais, Makamu Wa Rais, Wajumbe wa Baraza na kadhalika.

Kwa mujibu wa taarifa toka TLS, Rais wa sasa wa TLS Wakili Msomi Fatma Karume huenda asigombee tena nafasi hiyo kwakuwa hadi sasa jina lake halijapendekezwa kama mgombea wa nafasi hiyo. Wagombea wa nafasi mbalimbali hupendekezwa na wanachama wa TLS au kujipendekeza wenyewe.

Hadi sasa, Wakili Msomi John Seka ndiye aliyependekezwa kama mgombea pekee Wa Urais wa TLS. Makamu wa Rais Wa sasa Wakili Msomi Dr. Rugemeleza Nshala amependekezwa kuwania tena nafasi hiyo.

Wakili Msomi John Seka ndiye aliyekuwa Rais wa TLS kabla ya Wakili Msomi Tundu Lissu. Napo alikuwa Ni mgombea pekee katika nafasi hiyo baada ya aliyekuwa mgombea mwingine Wakili Msomi Alex Mgongolwa kujiondoa.

Update: TLS imeongeza muda wa kupendekeza wagombea Wa nafasi mbalimbali za uongozi hadi tarehe 20/2/2019
 
Sidhani kama alikua na any impact, ushindi wake haukumaanisha kuwa alikuwa na ushawishi bali ilikua ni msimamo wa Mawakili wa kutoburuzwa wala kupangiwa mambo.
Ila sasa hivi hicho chama nacho pumzi inakwenda kukata and the only option left ni kuwa kama Channel 10, yaani wawe sehemu ya ile taasisi yenye mizizi iliyo jichimbia chini zaidi. TLS inakwenda kubaki historia tu.
 
Chama cha Wanasheria wa Tanganyika almaarufu kama TLS kinatarajia kufanya mkutano wake mkuu wa mwaka mwezi wa nne jijini Arusha. Moja kati ya masuala yatakayofanyika ni pamoja na uchaguzi katika nafasi za Urais, Makamu Wa Rais, Wajumbe wa Baraza na kadhalika.

Kwa mujibu wa taarifa toka TLS, Rais wa sasa wa TLS Wakili Fatma Karume huenda asigombee tena nafasi hiyo kwakuwa hadi sasa jina lake halijapendekezwa kama mgombea wa nafasi hiyo. Wagombea wa nafasi mbalimbali hupendekezwa na wanachama wa TLS au kujipendekeza wenyewe.

Hadi sasa, Wakili Msomi John Seka ndiye aliyependekezwa kama mgombea pekee Wa Urais wa TLS. Makamu wa Rais Wa sasa Wakili Msomi Dr. Rugemeleza Nshala amependekezwa kuwania tena nafasi hiyo.

Wakili Msomi John Seka ndiye aliyekuwa Rais wa TLS kabla ya Wakili Msomi Tundu Lissu. Napo alikuwa Ni mgombea pekee katika nafasi hiyo baada ya aliyekuwa mgombea mwingine Wakili Msomi Alex Mgongolwa kujiondoa.
Mwaka huu ntapiga kura kumchagua Rais wa TLS kama nilivyofanya mwaka 2016 na miaka iliyotangulia.Nawasihi ndugu zangu tusilete wahuni TLS.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom