Uchaguzi Tarime kusimamishwa?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Kama mambo yanaenda jinsi yanavyoenda hasa kuelekea hizi siku chache za mwisho za uchaguzi kuna dalili za kutaka kusitisha uchaguzi huo mdogo hadi hali ya "usalama na utulivu" itakapotengemaa.

Hili linawezekana kutokea kwa mujibu wa "ka nzi" baada ya safu ya viongozi wa upinzani kuwasili na CCM na serikali yake kupima mwelekeo wa ushindi huko Tarime.

Kama kutatokea jambo lolote ambalo litasababisha vurugu kwa viongozi wa CCM au kuharibu mikutano ya kampeni yao basi uchaguzi utaahirishwa. Lakini the tipping point itakuwa ni kipimo kuwa CCM itashindwa kwa asilimia 60 na hilo halikubaliki kwao.

Vyanzo hivyo vinadokeza kuwa kama uamuzi wa kusitisha uchaguzi hautatolewa within the next 8 days (hadi Jumatano ijayo) basi uchaguzi utaendelea. Vinginevyo tuangalie siku hizi chache hadi Jumapili kwa habari za kushtua kutoka Tarime zitakazosababisha uchaguzi kusitishwa kwa muda na kupangiwa siku nyingine.
 
Kaka Mwanakijiji,

Nakkamini kainzi kanakokuletea habari, kwani kwa asili mia kubwa huwa hakakosei. Ila kama itakuwa hivyo, na kwa shinikizo la kufikirika, itasikitisha. Yetu macho na masikio kwani katika Bara letu all the Impossibles Do Happen!!!! .
 
Sasa wakuu,hapo ndipo tutakapoipima CCM kwenye kung'ang'ania madaraka.Tarime mapinduzi daima.

Na ikiwa iatatokea hivyo,vyama vya upinzani visikubali kuburuzwa,inabidi kuchukua hatua.kupambana na CCM inabidi sometimes nawe uwe reckless
 
Kaka Mwanakijiji,
Asante kwa taarifa, naamini kainzi kana uhakika kwani kila kakikuletea habari huwa kwa asilimia kubwa za kweli. Ila kama uchaguzi ukiahirishwa kwa shinikizo tu au kwa fujo za kufikirika / za kutengenezwa, itasikitisha sana.
 
Au Masatu unasemaje? Maanake huchelewi kulrta mzaha kwenye hoja muhimu,ngoja tuone
 
Tarime niliona mpango wao mapema .Tossi kupelekwa kwa jina la machafuko then they support and instigate basi nikaongea na wana Tarime wakasema wako Iraq ndogo nikakata tamaa .Kwa kweli nimeshangaa Serikali kuhamia Tarime , na gharama kubwa hadi kuwa imetumika kisa Jimbo la uchaguzi na Mbunge mmoja wa CCM .JK hana la kujivunia baadaye katika kukuza demokrasia Tanzania .
 
Kama mambo yanaenda jinsi yanavyoenda hasa kuelekea hizi siku chache za mwisho za uchaguzi kuna dalili za kutaka kusitisha uchaguzi huo mdogo hadi hali ya "usalama na utulivu" itakapotengemaa.

Hili linawezekana kutokea kwa mujibu wa "ka nzi" baada ya safu ya viongozi wa upinzani kuwasili na CCM na serikali yake kupima mwelekeo wa ushindi huko Tarime.

Kama kutatokea jambo lolote ambalo litasababisha vurugu kwa viongozi wa CCM au kuharibu mikutano ya kampeni yao basi uchaguzi utaahirishwa. Lakini the tipping point itakuwa ni kipimo kuwa CCM itashindwa kwa asilimia 60 na hilo halikubaliki kwao.

Vyanzo hivyo vinadokeza kuwa kama uamuzi wa kusitisha uchaguzi hautatolewa within the next 8 days (hadi Jumatano ijayo) basi uchaguzi utaendelea. Vinginevyo tuangalie siku hizi chache hadi Jumapili kwa habari za kushtua kutoka Tarime zitakazosababisha uchaguzi kusitishwa kwa muda na kupangiwa siku nyingine.

Nakuaminia kwa uganga huo wa kutoa ramli... haya ndugu
 
Serikali wameshindwa kusimamisha chaguzi za Zanzibar ndio iwe Tarime?

Uchaguzi utafanyika ila ndio hivyo tena, mali za watu zitaendelea kuharibiwa na watu kupigana/kupigwa bila sababu za maana.

Hizo zote ni dalili za taifa lenye wajinga wengi kuanzia kwenye uongozi wa juu mpaka kwa walala hoi.

Tarime kazi mnayo kweli kweli, uchaguzi utaisha na mtaachwa Soremba hapo hapo, huku wenzenu wanaenda kulewa Dar wakati nyie mnaomboleza.
 
wameshaseti stage leo baada ya Mwenyekiti wa tume kupiga mkwara vyama vyote leo. Na amesema kuanzia wiki ijayo Tume ya Uchaguzi itakuwa Tarime??? Sikujua kumbe muda wote huu tume ya uchaguzi haikuwepo Tarime.

Kama hali itakuwa ya utulivu kama alivyotanaibisha Lewis leo basi uchaguzi utaendelea lakini kama amesema ili kutengeneza preconditions za kusitisha uchaguzi basi tarajieni mambo toka Tarime kuanzia kesho Jumatano baada ya final strech ya kampeni kupamba moto.
 
Tume ya uchaguzi ingekuwa serious ilipaswa kuwa huko Tarime na ku-monitor activities zote za uchaguzi, inachekesha kuwa tume inaenda zikiwa zimebaki siku nane so ndio wanaenda na hizo ballot box au walisha zituma huko! du kweli watu wanajua kuwajibika, LOL
 
Mkakati uliopangwa kusababisha uchaguzi usitishwe ni ama Polisi na FFU kuwashambulia wananchi ili wananchi warudishe na hatimaye kusema kuna vurugu. Au watu wasiojulikana kumpiga risasi kiongozi mmoja wa upinzani na hivyo NEC kutangaza kwamba mazingira ya uchaguzi ni hatari. Hii nimeipata toka kwa chanzo changu kimoja kwenye vikao vya kamati ya ulinzi na usalama

PM
 
Tumeshaliweka hapa hadharani, ili litakapotokea tusitafute udhuru. Soma makala yangu ya kesho pia... nimelifafanua kwa kina!
 
Sasa niemamini demokrasia hakuna tena tanzania
tume ya ccm ikiongozwa na bwana makame leo hii`
wametangaza kuairisha uchaguzi wakati wowote
kama hali ya kampei itaendelea hivi
na hili ni baada ya kuona hali inakuwa ngumu siku
zinazoyoyoma .......kazi kweli kweli.........
 
Hizo zote ni dalili za taifa lenye wajinga wengi kuanzia kwenye uongozi wa juu mpaka kwa walala hoi.QUOTE]

Mkuu,

You can do better than this.Ya nini kutukana taifa zima mkuu.Yaani huwezi kutoa hoja zako kwa uangalifu bila kulitukana taifa,eti ni dalili za sisi wananchi pamoja na viongozi wetu kuwa wajinga? No,please give me a break!
Kuwa kwako huko majuu mkuu,haimaanishi kwamba wewe ndiwe mwenye akili kuliko wote kule Tanzania mkuu,jenga hoja acha kulidhalilisha taifa mkuu.Kwa mara nyingine nakuomba ukanushe kauli yako.

Btw: wanaochochea vurugu huko Tarime ni CCM na jeshi la polisi pamoja na Mtikila.Kwanini mtikila asikamatwe kwa uchochezi? Kama kweli wanataka uchaguzi kuwa huru na wa haki?
 
Hizo zote ni dalili za taifa lenye wajinga wengi kuanzia kwenye uongozi wa juu mpaka kwa walala hoi.QUOTE]

Mkuu,

You can do better than this.Ya nini kutukana taifa zima mkuu.Yaani huwezi kutoa hoja zako kwa uangalifu bila kulitukana taifa,eti ni dalili za sisi wananchi pamoja na viongozi wetu kuwa wajinga? No,please give me a break!
Kuwa kwako huko majuu mkuu,haimaanishi kwamba wewe ndiwe mwenye akili kuliko wote kule Tanzania mkuu,jenga hoja acha kulidhalilisha taifa mkuu.Kwa mara nyingine nakuomba ukanushe kauli yako.

Btw: wanaochochea vurugu huko Tarime ni CCM na jeshi la polisi pamoja na Mtikila.Kwanini mtikila asikamatwe kwa uchochezi? Kama kweli wanataka uchaguzi kuwa
huru na wa haki?

Ben
Mtanzania yuko sahihi kabisa. Tanzania ni taifa la wajinga. In fact mimi hupenda kusema Tz ni taifa la majuha(idi0ts), kuanzia raisi mpaka wafagizi wa barabarani. Mimi siko huko ughaibuni. Lakini ninaona wazi wazi jinsi fikra zetu zilivyo finyu. How do you relate vast wealth versus abject poverty among Tz citizens?
__________________
 
Mkuu,I beg to differ,kosa ni la viongozi kutokubali hata kutoa elimu ya uraia kwa watu wetu.Halafu mazingira ya hofu yanapojengwa na watawala dhidi ya wananchi.Still naamini kabisa watanzania wote na au si viongozi wote wajinga mkuu.
 
Back
Top Bottom