Elections 2010 Uchaguzi Tanzania haukuwa na "dosari"

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,615
Wachunguzi wa uchaguzi nchini Tanzania wamesema hakuna taarifa yoyote kuu ya dosari iliyojitokeza inayoweza kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili.
101101151840_tanzania_election_386x217_nocredit.jpg
Uchaguzi Tanzania haukuwa na dosari

Kiongozi wa jopo la wachunguzi kutoka Jumuiya ya Madola Bw Paul East, amesema uchaguzi huo uliendeshwa vyema ikilinganishwa na ya miaka mitano iliyopita.
Hata hivyo East amesema kuchapishwa kwa matokeo ya uchaguzi huo kumecheleweshwa sana.
Amesema kutokana na kuwepo teknolojia ya kisasa, haipaswi matokeo hayo ya uchaguzi kuchukua siku nne hata tano kuweza kujulikana.
Wakati huo huo Mawaziri kadhaa tayari wamepoteza viti vyao vya ubunge katika uchaguzi huo.

BBC Swahili - Habari - Uchaguzi Tanzania haukuwa na "dosari"
 
Angejiuliza kwanza kwanini matokeo yamechelewesha ndio aseme kuwa uchaguzi ulikuwa huru na haki
 
:smile-big::smile-big: PALIONDOKEA CHANJAGAA KAJENGA NYUMBA KAKAA....:smile-big: Ni hadithi taaaaamu kusikilza UCHAFUZI Ooops UCHAGUZI wa taifa letu unavyofanyika na kufanywa:A S angry: katiba mpya, tume mpya ndio dawa.:tape:
 
uchaguzi ni mpaka matokeo, sasa matokeo hayajatoka unasema hayana dosari? watu wakipiga kula kisha usitoe matokeo kutokana na kula zile ukatoa ya uchakachuaji utasema hayana dosari? maswali mengi kuliko majibu.
 
Matokeo ya masaa machache mara baada ya uchaguzi yalikuwa yanaonesha hali halisi, Slaa na JK walikuwa hawaachani sana, lakini siku iliyofuata upepo ulibadilika ghafla ukionesha eti JK akiongoza kwa kishindo!
 
(WAISLAM WATAKUWA NA BUSARA WATAKAPOANZA KULA KITIMOTO )

Mheshimiwa HAPA UMEUGUSA UISLAM SWALA KITIMOTO NI KATAZO KUTOKA KWENYE VITABU VYETI KWA WEWE KUONGEA MANENO HAYO MEANS UNAKIKOSOA, UMEKIKOSEA UMETUKOSEA TAFADHALI KAMA UNA BUSARA TUTAKE RADHI WAISLAM NA UISLAM. NITASHUKURU KAMA UTAKUWA UMENIELEWA. NIMETIMIZA WAJIBU WANGU KAMA MUISLAM
 
Labda katika report yao matokeo hayawahusu na unaweza kuta mwisho wa coverage ilikuwa jumapili usiku
 
Wachunguzi wa uchaguzi nchini Tanzania wamesema hakuna taarifa yoyote kuu ya dosari iliyojitokeza inayoweza kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili.
101101151840_tanzania_election_386x217_nocredit.jpg
Uchaguzi Tanzania haukuwa na dosari

Kiongozi wa jopo la wachunguzi kutoka Jumuiya ya Madola Bw Paul East, amesema uchaguzi huo uliendeshwa vyema ikilinganishwa na ya miaka mitano iliyopita.
Hata hivyo East amesema kuchapishwa kwa matokeo ya uchaguzi huo kumecheleweshwa sana.
Amesema kutokana na kuwepo teknolojia ya kisasa, haipaswi matokeo hayo ya uchaguzi kuchukua siku nne hata tano kuweza kujulikana.
Wakati huo huo Mawaziri kadhaa tayari wamepoteza viti vyao vya ubunge katika uchaguzi huo.

BBC Swahili - Habari - Uchaguzi Tanzania haukuwa na "dosari"

Dosari zipo kibao wewe soma Respect poll outcome for peace - EU: C`wealth, AU: Poll peaceful, results handling poor http://www.ippmedia.com
 
Back
Top Bottom