Uchaguzi Tanzania haukuwa na "dosari" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi Tanzania haukuwa na "dosari"

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzito Kabwela, Nov 3, 2010.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Wachunguzi wa uchaguzi nchini Tanzania wamesema hakuna taarifa yoyote kuu ya dosari iliyojitokeza inayoweza kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili.
  [​IMG] Uchaguzi Tanzania haukuwa na dosari  Kiongozi wa jopo la wachunguzi kutoka Jumuiya ya Madola Bw Paul East, amesema uchaguzi huo uliendeshwa vyema ikilinganishwa na ya miaka mitano iliyopita.
  Hata hivyo East amesema kuchapishwa kwa matokeo ya uchaguzi huo kumecheleweshwa sana.
  Amesema kutokana na kuwepo teknolojia ya kisasa, haipaswi matokeo hayo ya uchaguzi kuchukua siku nne hata tano kuweza kujulikana.
  Wakati huo huo Mawaziri kadhaa tayari wamepoteza viti vyao vya ubunge katika uchaguzi huo.

  BBC Swahili - Habari - Uchaguzi Tanzania haukuwa na "dosari"
   
 2. K

  King kingo JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Angejiuliza kwanza kwanini matokeo yamechelewesha ndio aseme kuwa uchaguzi ulikuwa huru na haki
   
 3. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  :smile-big::smile-big: PALIONDOKEA CHANJAGAA KAJENGA NYUMBA KAKAA....:smile-big: Ni hadithi taaaaamu kusikilza UCHAFUZI Ooops UCHAGUZI wa taifa letu unavyofanyika na kufanywa:A S angry: katiba mpya, tume mpya ndio dawa.:tape:
   
 4. B

  Biro JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 331
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  uchaguzi ni mpaka matokeo, sasa matokeo hayajatoka unasema hayana dosari? watu wakipiga kula kisha usitoe matokeo kutokana na kula zile ukatoa ya uchakachuaji utasema hayana dosari? maswali mengi kuliko majibu.
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Nov 3, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Matokeo ya masaa machache mara baada ya uchaguzi yalikuwa yanaonesha hali halisi, Slaa na JK walikuwa hawaachani sana, lakini siku iliyofuata upepo ulibadilika ghafla ukionesha eti JK akiongoza kwa kishindo!
   
 6. m

  msasa Member

  #6
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  (WAISLAM WATAKUWA NA BUSARA WATAKAPOANZA KULA KITIMOTO )

  Mheshimiwa HAPA UMEUGUSA UISLAM SWALA KITIMOTO NI KATAZO KUTOKA KWENYE VITABU VYETI KWA WEWE KUONGEA MANENO HAYO MEANS UNAKIKOSOA, UMEKIKOSEA UMETUKOSEA TAFADHALI KAMA UNA BUSARA TUTAKE RADHI WAISLAM NA UISLAM. NITASHUKURU KAMA UTAKUWA UMENIELEWA. NIMETIMIZA WAJIBU WANGU KAMA MUISLAM
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Labda katika report yao matokeo hayawahusu na unaweza kuta mwisho wa coverage ilikuwa jumapili usiku
   
 8. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Dosari zipo kibao wewe soma Respect poll outcome for peace - EU: C`wealth, AU: Poll peaceful, results handling poor http://www.ippmedia.com
   
Loading...