Uchaguzi Serikali za Mitaa CCM imepoteza mwelekeo Arusha

12STONE

JF-Expert Member
Mar 16, 2013
1,109
1,475
Kuelekea Uchuguzi wa Serikali za Mitaa 14.12.2014 naona CCM wamechanganyikiwa,hawana Tumaini na bila kutafuna tafuna maneno na thubutu kusema CHAMA CHA MAPINDUZI kadri tunapokaribia sana kupiga KURA ndivyo Kinavyopoteza mwelekeo kabisa.

Jana kwa macho yangu nimewaona Vijana wawili wakifutilia waendesha boda boda na tayari walikuwa na baadhi yao Wakiwahonga 10,000/= hadi 15,000/= ili kuwakabidhi Bendera ya CCM ifungwe kwenye Piki piki na kuzunguka nazo.

Kijana mmoja wa CCM kwa kujiamini alijaribu kumwita mtoto mdogo wa miaka 3 au 4 hivi,akafanya jaribio la kumwuuliza swali huku akimwonyesha Bendera ya ccm iliyokuwa imefungwa kwenye Pikipiki na Bendera ya CHADEMA ilikuwa juu ya bati,KATI YA HIZO BENDERA mbili anapenda ipi???
MTOTO kwa ujasiri kabisa akasema anaipenda CHADEMA huku ameinyoshea kidole BENDERA YA CHADEMA.

Ni aibu kubwa kuona watu wanatoa Rushwa na kujaribu kuwalaghai UMMA kwa pikipki zenye bendera za CCM huku mkijua wazi CCM imepoteza mwelekeo na kukataliwa kabisa Arusha.
HIO NDIO HALI HALISI.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom