Uchaguzi S/Mitaa 2019: Wagombea wa Upinzani asilimia kubwa wameenguliwa kugombea, CCM wengi wapitishwa

Uchaguzi huu utathibitisha ukweli kuwa Tanzania haina wapinzani na hawa waliopo ni Wajasiriasiasa......wanasaka fursa tu wapate kuishi!
Kuthibitisha kwamba hakuna wapinzani ni kuruhusu uchaguzi huru na kuwashinda , hili mnalolifanya litaleta vita

Yahya Jammeh baada kuchoka kubaka demokrasia alifikia ku kuanza kubaka wasichana wazuri wa nchini mwake , leo yuko wapi ?
mshahara wa dhambi ni mauti
 
Nilijua utani.

Nimekutana Na aliyekuwa mgombea uwenyekiti wa Chadema analalamika .Wanachofanya kati ya wale wajumbr njaa wa upande pinzani anashikwa mmoja mwenye njaa anasaini.Mgombea uwenyekiti anakuja tu kuambiwa bwana nimeshasaini Badala yako.

Hii Kali sana.

Mungu ingilia kati
 
Yaani nimecheka sana ila yote heri Mungu anawaona jinsi mnavyonyima haki halafu mkipata laana na familia zenu mnasema Mungu anipendi kumbe umevuna mwenyewe na anayewatuma katulia tuli na anataka apate lana na wengi.CCM mna akili sana
 
Fedha hizi za uchaguzi zingeweza kujenga barabara ya kwetu matombo walau kwa kiwango cha changarawe kutoka Bigwa Morogoro mpaka Kisaki.

Tunachezea hela kiseng sana
 
Kama hawakujitokeza kugombea inaweza kuwa haina tatizo. Lakini kama wamegombea na wamezuiwa hapo kuna kitu watu wanataka kukiona. Najaribu kujiuliza wale watu milioni 6 na point waliochagua wapinzani walienda wapi? Kama bado wapo hai naogopa sana.
Nadhani kuna vigezo viliwekwa...ili kuondoa utata...tupewe vigezo vilivyotumika kuwaondoa kwenye 'kuwania' nafasi walizoomba.

Na unaweza ukute hawa hawakutimiza vigezo makusudi ili waonekane wameenguliwa kwa 'uonevu' baada ya kusoma mchezo kuwa uwenda wasipate kura....

Maana nakumbuka kuna baadhi ya wanachama wa vyama fulani walihimizana kutokujihandikisha kupiga kura...hilo msilisahau.
 
Utaratibu wa kuwekana na kuondoana madarakani kwa kura ni wa wazungu lakini hata sisi waafrika pamoja na uduni wetu unaonekana ndio utaratibu sahihi na unatufaa. Hii ni kwa sababu utaratibu mbadala ni kuwa na mfumo wa kifalme ambapo kwa sasa ni ngumu ku-implement.

Kama mamlaka zinafikiri zinaweza kupata madaraka bila ridhaa ya wananchi basi wabuni mfumo sahihi na sio hivi viini macho maana sasa watu ni waelewa. Mbali na hapo wakitokea miongoni mwetu wakakubali kwamba mfumo wa upigianaji kura umefeli na kuamua kubuni wa kwao basi tumuombe Mungu wasije wakabuni kitu kibaya kitakacho haribu hata kidogo tulichokwisha kijenga. Tukumbuke miongo mitatu iliyopita Somalia ilikuwa nchi imara.

Maneno kuwa Haki huinu taifa hakuna hata mmoja wetu mwenye akili timamnu anayeyakataa!
 
Back
Top Bottom