Uchaguzi S/Mitaa 2019: Wagombea wa Upinzani asilimia kubwa wameenguliwa kugombea, CCM wengi wapitishwa

Chama hiki hakikujipanga kwaajili ya ushindani hii ni kutokana na udikteta wa viongozi wao kuendesha chama,kila agizo linatoka kwao tu hakunà kushirikisha wanachama,tangu2015 hakipendwi tena na wananchi.
Inakuaje taasisi kubwa hivi ikakosa interejinsia ya kung'amua kuwa serikali itatukatia majina ya wagombea wetu na je?tufanyaje sasa ili wasitukate?....hamkujipanga mlikurupuka kwenda vitani kwa kutegemea mtashinda bila kuwa na mbinu bora.
CCM ilishinda vita ndipo ikaingia vitani,nyie mmeingia kimachomacho tu bila kuwa na planiB,mnavuna mlichopanda2015.
First to reply
 
Yanayotokea sasa huku Tanganyika nikopi tu ya yale yaliotokea Zanzibar, kule Zenji ndugu zetu walipiga kelele sana tukawaona misukule tu, sasa yanatokea kwetu mchana kweupe. Baada ya miezi kadhaa tutaingia kwenye uchaguzi mkuu, na tutashuhudia makubwa Zaidi.
 
CCM ilishinda vita ndipo ikaingia vitani,nyie mmeingia kimachomacho tu bila kuwa na planiB,mnavuna mlichopanda2015.
Vita ya mwisho iliyoshinda ni ile ya 'Battle of CAG'. Nyingine ni 'Crash of the Oppositions'. "Surrender of the Parliament".., "Capturing of the Army" .., "A war Within CCM" na nyingine nyingi.
 
huyohuyo anasema unapopigana usimzingire adui mazima, acha upenyo wa kutorokea. Usimlazimishe apiganie uhai wake.
 
Hakuna afadhali yeyote ,kwani hata kuiba kura pia ni dhulma,tena nibora wametuonyesha mapema ufedhuli wao kuliko tungeenda kupigwa na jua na mvua for nothing.
Hakika CCM ni waoga kweli, ni bora wangewapitisha kisha waibe kura kuliko kuwakata juujuu. Haileti picha nzuri kabisa
 
Mkapige kura wapi wakati CCM imepita bila kupingwa nchi nzima!

Hivi uchaguzi maana yake ni nini? mimi nadhani ni kuchagua kutoka kwenye vitu kadhaa unachagua kimoja. sasa kama mgombea amebakia mmoja unachagua nini? This strange Tanzania!
 
Kwa mujibu wa John Mnyika in kuwa jimbo lake la Kibamba wagombea wote wa Chadema serikali za mitaa wameenguliwa. Pia asilimia 90 ya wagombea wa Chadema nchi nzima wameenguliwa.

Huu utoto wa serikali ya awamu hii haujawahi hata kuotwa ndoto ya mchana siku za nyuma. Kiukweli haya mambo ya hovyo anayofanya Magufuli na kisha tunayaona wazi wazi yanatupa uhakika kuwa katika utawala wake anafanya madudu mengine mengi sema hayajawa tu wazi ila muda utafika tu yatajulikana.
 
maelekezo toka kwa Jiwe;
inaonekana nchi nzima walipewa semina elekezi jinsi ya kuchakachua..

natamani ije siku Mikono ya jiwe ivishwe pingu, aonje joto la jiwe...
Wapewe maelekezo halafu yabaki siri vyama vingine visifahamu wakati wote tunaishi pamoja, tunakula sehemu moja; tunalewa sehemu moja; tunasali pamoja; tunaombeleza pamoja....wangewamegea wenzao tuu
 
Mnyika juzi kati vijana wa Kata ya msigwa wakamuweka kati kwa kuwadanganya na utapeli wa siasa ,viogozi kama mnyika wanao nenepa kama nguruwe na kutelekeza jimbo 2020watafute kazi ya kufanya

State agent
 
CCM wanazidi kuipaisha chadema kama chama kikuu kinachoogopwa, yaan nguvu yote hiyo bado chama kipo imara
 
Arafu tumekua waoga kweli Dunia inatushangaa kama kweli tuko sobar watu 55m wanapelekeshwa na watu 4 au 5. Humu kwenye million 55 kuna wasomi matajiri wakulima wakubwa Maraisi wastaafu watumishi wa Umma mapadiri ma sheikh nk.....hao watu wote wanaona ila wanaburuzwa na watu wawili tu kuna haja ya utafiti katika uelewa wa Watznia kwakweli wako normal na sense 5.
Inatushangaa kwa mengi. Taifa lenye mamilioni waliotamani Lowasa awe Rais wao linaweza kuwa taifa la watu aina gani?!
 
Mengi yamesemwa kuhusu maandalizi au mchakato wa uteuzi wa agombea. Na wale wa upinzani kuenguliwa ili wasishiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa mwezi huu tarehe 24.

Hali hii imewalazimisha CHADEMA kuamua kususia UCHAGUZI huo.

Mtiririko wa mambo tangu kupigwa marufuku shughuli halali za nyama vya upinzani, maelekezo ya Rais kwa wakurugenzi wa wilaya na mikoa kwamba wasiruhusu wapinzani kutangazwa washindi; na uteuzi wa haohao kuwa wasimamizi wa uchaguzi, na kufuatiwa na uamuzi wa Mahakama kubariki wateule hao kama wasimamizi wa uchaguzi eti ilimradi wataapishwa! Maana ya mlolongo huu wa mambo ni kuhalalisha kisheria mchakato feki usio wa haki na uhuru.

Kwahiyo kudai kwamba walioenguliwa wakate rufaa kwa Tume au Mahakama ni sawa na kupiga rangi upepo au "white washing".
 
Mnyika juzi kati vijana wa Kata ya msigwa wakamuweka kati kwa kuwadanganya na utapeli wa siasa ,viogozi kama mnyika wanao nenepa kama nguruwe na kutelekeza jimbo 2020watafute kazi ya kufanya

State agent
Mbna baba ako nae kanene kalio atusemi
 
Mkuu umesema kweli tupu..

Huyu jamaa ana madudu mengi tu ya ovyo muda ukifika waimba mapambio wake sijui wataweka wapi sura zao..

Kumbuka wakati akiwa Ujenzi kila ukaguzi wa CAG yalikuwa yanagundulika matumizi kibao ya utata..

He is the WORST Country Leader Tanzania has ever had in its history.
 
Yako maeneo watendaji wamelipwa kati ya 50000 Na 100000 kwa kukataa fomu za wagombea Wa upinzani.jaffo anatuzuga tu anajua yanayofanyika
 
Mnyika juzi kati vijana wa Kata ya msigwa wakamuweka kati kwa kuwadanganya na utapeli wa siasa ,viogozi kama mnyika wanao nenepa kama nguruwe na kutelekeza jimbo 2020watafute kazi ya kufanya

State agent
Unaona sifa mwenyewe kuongea upupu mbele ya watu wenye akili zao
 
Chama hiki hakikujipanga kwa ajili ya ushindani hii ni kutokana na udikteta wa viongozi wao kuendesha chama, kila agizo linatoka kwao tu hakunà kushirikisha wanachama, tangu 2015 hakipendwi tena na wananchi.

Inakuaje taasisi kubwa hivi ikakosa intelejinsia ya kung'amua kuwa serikali itatukatia majina ya wagombea wetu na je? tufanyaje sasa ili wasitukate?....Hamkujipanga mlikurupuka kwenda vitani kwa kutegemea mtashinda bila kuwa na mbinu bora.

CCM ilishinda vita ndipo ikaingia vitani, nyie mmeingia kimachomacho tu bila kuwa na plani B, mnavuna mlichopanda 2015.
Mkuu wakati mwingine ni busara kukaa kimya....''kwenya rangi nyekundu panakuhusu.'hapo juu''...sio kwa serikali hii ya awamu ya tano...umesahau wasiojulikana....
Halafu malalamiko sio ya chama kimoja...vyama karibia vyote vinalalamika.....Ujamsikia Profesa Lipumba...na Mzee wako Mrema......
Wape Plan B....
 
Kwa mujibu wa John Mnyika in kuwa jimbo lake la Kibamba wagombea wote wa Chadema serikali za mitaa wameenguliwa. Pia asilimia 90 ya wagombea wa Chadema nchi nzima wameenguliwa.

Huu utoto wa serikali ya awamu hii haujawahi hata kuotwa ndoto ya mchana siku za nyuma. Kiukweli haya mambo ya hovyo anayofanya Magufuli na kisha tunayaona wazi wazi yanatupa uhakika kuwa katika utawala wake anafanya madudu mengine mengi sema hayajawa tu wazi ila muda utafika tu yatajulikana.
Kiongozi fisadi hawezi kupenda demokrasia, anapiga hela nyingi kwenye miradi ya ndege, sgr, madini, bwawa nk na hakuna wa kuthubutu kulisema na kulikemea
 
White house ilitumika kama venue kupanga uhalifu dhidi ya katiba na demokrasia ya watanzania. Wasimamizi clearly walipewa maagizo nini wafanye na nn wajaze katika form ili kuwaondolea haki walizopewa watanzania kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa.
 
Back
Top Bottom