sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 3,163
- 8,848
Tundu Lissu ni baba aambiliki nilimuonya hapa majuzi aache mission yake ya kukiua chama hajataka kusikia.
Sasa anaenda kufundishwa adabu na bingwa wa sayansi ya siasa za upinzani Aikael Mbowe.
Kelele ni nyingi mtandaoni lakini hazitomsaidia Lissu na kichapo cha mbwa mwizi toka kwa Mbowe.
Lissu ana wapiga kelele haswa wa mtandaoni, Mbowe ana wapiga kura. Mpaka hapo nani anaenda kushinda?
Uchaguzi wa Chadema una wajumbe wa mkutano mkuu wanakaribia 1300 ambao wana vigezo vya kupiga kura.
Mpaka hapo nafikiri mnaelewa kwa nini Lissu alikuwa anatoa milio mingi kwenye chaguzi zilizokuwa zinaendelea kwa sababu anajua Mbowe alikuwa anapanga safu yake ya kumpigia kura. Yani Mbowe mpaka sasa ana wapiga kura wa kutosha.
Kilichobaki ni Lissu kunyolewa bila maji then akimbie chama kwa hasira yeye na wapiga kelele wenzake.
Baada ya hapo Mbowe ataisuka upya Chadema yake na kurecruit damu mpya nyingi za vijana watiifu wafanya siasa sio harakati.
Lissu anasema uchawa kwenye chama haufai wakati yeye ndio alikuwa chawa namba moja wa Mbowe. Zitto na Kitila wanafukuzwa Lissu ndio kijumbe yupo pembeni ya Mbowe anatoa ushauri wa kisheria.
Dr Slaa anakimbia Chadema, Lissu yupo pale anamnyoosha Dr Slaa.
Yeye ndio alikuwa mastermind wa kuondoa ukomo wa uongozi kwa kuwa alikuwa ananufaika leo anawadanganya chama hakikuwa na watu.
Nasemaje Lissu anatakiwa apigwe vizuri mpaka hata hicho chama anachotaka kuanzisha aghairishe arudi kula pensheni ubeligiji.
Sababu ni moja ni TRAITOR.
Alimsaliti JPM mkamshangilia.
Amefanya kwa Mbowe kipenzi chenu.
Amesaliti watu wengi sana ili yeye ajenge jina lake kwamba anaipenda Tanzania kuliko kiumbe yoyote.
Mimi sio shabiki wa Mbowe ila watu kama Lissu wenye kelele nyingi na hekma sifuri hawatakiwi kuongoza taasisi yoyote. Chadema ipo hapo ilipo kwa vingi ikiwemo hekma za Mbowe. Mbowe ni Nigga ila ni kiongozi mara 200 kumzidi Lissu.