Uchaguzi ni muhimu, viongozi bora ni muhimu, ila... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi ni muhimu, viongozi bora ni muhimu, ila...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Natty Bongoman, Oct 26, 2010.

 1. Natty Bongoman

  Natty Bongoman JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Uchaguzi waja, kura ni muhimu... Lakini wananchi wenzangu - hata ka tulikuwa na viongozi wabaya miakani ilopita na mola forbid, labda miakani ijayo... Lawama si zote kwao, wakati wengi tuliketi tukingojea miujiza tokea kwao... Tafadhali chunguzeni maofisini - makazini... Wengi wakazana kuiba, kujivimbisha, kukata konaz, kufanya kazi kivivu, kutoheshimu kazi... Nchi ama kampuni itajengeka vipi tukiendelea na tabia hizi ?????????? sote twahitajika kujenga nchi, si viongozi tu...

  Pia jamani, Sirikali itaendelea kuwa sirikali, ka wananchi hatuungani kupiga makelele - wachache wanaopiga makelele wataendelea kunyamazishwa ka hawaungwi na wananchi wengi makeleleni - Sirikali haiwezi kunyamazisha ama kufunga wananchi mia kadhaa ama elfu kadhaa bila kustusa nchi na dunia, lakini wanaweza kunyamazisha na kufunga wachache ka wananchi wengi wanabakia kimya...


  Nchi yetu inaendelea vizuri (ila si haraka) bila kutumia 'uhuni'... Lakini wahuni wengi wanatajirishwa na nchi yetu bila kunufaisha wananchi... sisi wengi si wajinga, ila sisi wengi hatuunganiki kulalamika... mfano, uchimbaji wa madini yetu, hakuna transparency tokea sirikalini, hakuna muungano mkuu wa kuilalamikia sirikali, sijui ka viongozi 'wanaotuwakilisha' wanalalamika kwa niaba yetu? ... kwani hatuna ruhusa ya kujua manufaa kwetu ???

  Mungu ibariki Tanzania na watoto wake.
   
Loading...