Uchaguzi nchi za Jumuia ya Ulaya ni fundisho kwa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki na Tanzania

mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
9,737
2,000
Matokeo ya chaguzi katika nchi mbalimbali huko Ulaya unaonyesha vyama vya mlengo wa kulia vimepata ushindi ambao haukutegemewa katika nchi na kiini cha ushindi huo ni wananchi wa hincho kuchoka na kuburuzwa na sera ambazo zinatungwa tofauti na matakwa yao huko kwenye makao makuu ya jumuia hiyo na kuwaacha wananchi wakiwa katika hali mbaya kiuchumi,pia wanataka mambo ya uhamiaji yawe ni maamuzi ya kila nchi.

Kwa sisi Tanzania tujifunze kuwa Jumuia ya Afrika Mashariki haitatusaidia kitu sisi Watanganyika ,kwani mambo ya uhamiaji /ajira na sarafu ya pamoja yatatuathiri zaidi tukiwa huko kuliko kama tusingekuwa kwenye jumuia.

Pia ni fundisho kwa Muungano wetu na hilo Bunge letu la Katiba kuwa pamoja na yote wananchi ndio wenye maamuzi kupitia kura.

Naamini kama CCM wangesikiliza wapinzani kule Bunge la Katiba kusingekuwa na kitu kinachoitwa UKAWA na sasa muda mwingi na raslimaliza taifa zinapotea bure ili kudhibiti UKAWA.

Uchaguzi wa EU uwe ni fundisho kwetu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom