Uchaguzi mwaka huu ni kati ya mafisadi na wapinga ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi mwaka huu ni kati ya mafisadi na wapinga ufisadi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Masauni, Sep 22, 2010.

 1. M

  Masauni JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uchaguzi wa mwaka huu ni muhimu sana kwa watanzania, lakini pia ni mtego mkubwa sana kwa watanzania. Sababu uchaguzi huu ni kati ya Mafisadi na wapigania uhuru wa wanyonge. Ukifuatilia kampeni za CCM si raisi wala mbunge anayeongea jinsi gani atapambana na ufisadi, ni swala ambalo wamelikubali na kwa upande mwingine Dr. Slaa na Chadema wanasema ni jinsi gani watapambana na ufisadi. Ndugu mtanzania hata kama CCM itatoa ahadi 1000, kama swala la kupinga ufisadi halitapewa kipaumbele hizo ahadi ni kazi bure maisha yataendelea kuwa magumu tu, (Naomba usome kwa undani kilichotokea zimbabwe, utaamini ninachosema). Nimalizie kwa kusema hivi mtego mkubwa uliopo mbele yetu ni kuwa KUICHAGUA CCM IENDELEE KUTAWALA NI KURUHUSU MAFISADI KUENDELEA KUIFISADI NCHI YETU(Tusije lalamika katika hilo, si tumetaka wenyewe) na KURUHUSU CHADEMA KUONGOZA NCHI NI KUSEMA TUMECHOKA NA UFISADI NA TUNATAKA UHURU WA WANYONGE
   
 2. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  True 100%, Toka kampeni zianze hakuna hata mkutano mmoja JK kishakemea Ufisadi zaidi ya kuwakumbatia wahusika wakuu, hakika kuichagua CCM ni sawa na kuua watoto wako, kaka zako, dada zako, ndugu zako, wazazi wako kwa shoka lako mwenyewe na wewe ukabaki hai na msongo wa mawazo ukiwa gerezani Ukonga ukisubiri faili litoke kwa DPP 2015
   
Loading...