maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,344
Kwa namna hali ilivyo na inavyoonekana uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge wa 28 Oktoba 2020 kwa namna unavyoonekana utakuwa ni uchaguzi ambao wapiga kura wataongozwa na mambo makubwa mawili wakati wa kupiga kura yao.
1. Kuna wapiga kura watakaopiga kura yao kwa chuki ya kuuadhibu utawala ulioko madarakani kutokana na uonevu na maovu waliyofanyiwa. Hawa ni wale;
√ waliotumbuliwa, kuachishwa na kufukuzwa kazi kwa uonevu.
√ wanaochukizwa na utungwaji wa sheria za kujipendelea na upendeleo kwa watawala. Wanaoona Kama sheria ya kinga ya viongozi ilikuwa njia ya kujihami kwa watakayofanya.
√ waliokutwa na majanga wakapuuzwa, wakakejeliwa na wakanyimwa misaada walliyochangiwa na watanzania ndugu zao.
√ wale waliojitolea kuwasaidia wahanga wa matukio na majanga mbali mbali lakini misaada yao haikuwafikia wale waliokusudiwa.
√ watumishi waliofukuzwa kazi au KUNYIMWA mishahara yao kwa sababu walienda kugombea uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kitu ambacho hakijawahi kuwepo.
√ wafugaji waliouziwa mifugo yao kwa sababu mbali mbali na wakulima walionyang'anywa mazao au ambao walichukuliwa mazao yao lakini hawakulipwa.
√ waliobambikizwa kesi na kutakiwa kwenda kutubu kwa DPP walikolipa mamilioni na mabilioni ya fedha bila kufikishwa mahakamani.
√ ambao walikamatwa wakateswa, wakapotea na hata kuuawa na watu wanaoitwa "wasiojulikana"
√ kuna watanzania watakaopiga kura kama huruma na faraja kwa Tundu Lissu wanaomwona kama ni mtetezi wao aliyeonewa na kutaka kuuawa kwa sababu ya misimamo yake ya kutetea haki na uhuru wa watanzania na raslimali zao.
√ walionyimwa fursa ya kufanya siasa katika nchi yao wakati ni haki yao ya kidemokrasia.
Wahanga hao wote wanao makumi, mamia na maelfu ya jamaa, ndugu na watanzania chungu nzima nyuma yao ambao kura yao itakuwa ngumu sana kuitoa kwa CCM.