Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA: Kujiandaa kuongoza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA: Kujiandaa kuongoza?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 30, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Sijui ni lini uchaguzi Mkuu wa Chadema utafanyika japo nakumbuka ulikuwa ufanyike katikati ya mwaka huu. Kwa vile muda uliobakia kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010 ni kama mwaka mmoja na nusu tu, je:

  - CHADEMA chaweza kujipanga kuongoza taifa
  - Ni mabadiliko gani ya kisera na falsafa ambayo yatasababisha Chadema kuonekana kujiandaa kuongoza?
  - Ni mabadiliko gani ya kiuongozi yataashiria mwanzo mpya kuelekea kuongoza taifa?
  - Je, ni nani ndani ya Chadema leo hii anaweza kuwa mgombea wao wa Urais na kwanini? Kuna ulazima wa wao kumsimamisha mgombea wa Urais?
  - Kama Katiba haitabadilishwa na tume ya uchaguzi itakuwa ikiongozwa na sheria ile ile je Chadema washiriki wakijua kuwa bado wako kwenye upande ambao ni vigumu kushinda kama taratibu hazitabadilishwa na kuwa za haki zaidi na usawa?
  - Je, kuna umuhimu wa kuungana na chama kingine chochote au Chadema ijizatiti kusimama peke yake?
  - Kwa vile wamepata nafasi nyingi za kuvutia watu na hali ya kisiasa imekuwa upande wao sana ni kwa sababu gani wameshindwa kuiangusha CCM kwenye majimbo kadhaa licha ya upepo wa kisiasa kuwa upande wao (chadema)? Je yawezekana ni dalili ya kutokuwa tayari kuongoza kitu ambacho kinatumiwa na CCM vizuri sana?
  - Ili waweze kukubalika kuliongoza taifa ndani ya mwaka mmoja na nusu hivi ni vitu gani vifanyike kwa Chadema au chama kingine cha kisiasa ambacho kitasababisha kuanguka na kuporomoka kwa utawala wa CCM?
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mimi naona pamoja na kuambia wananchi CCM wameshindwa kufanya nini pia wakazanie kuwaambia wananchi wao wata fanya nini tofauti na CCM. Lazima waonyeshe kuwa wao ndiyo the better party. Huwa nasemaga mara nyingi, sidhani kama wananchi walio wengi wanaijua Chadema vilivyo na ndiyo maana waweza kuta sehemu nyingine CCM inashinda by the virtue of name recognition. Wamejitahidi kuanzisha operesheni Sangala ila sijasikia ripoti yoyote ikielezea hiyo operesheni inakwendaje na imekisaidiaje chama mpaka sasa. Chadema can be a force to be reckoned with, kilicho baki ni wao kulive up to their potential.
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  chadema haiwezi kuanza kufikiria kuongoza taifa wakati viti vya ubunge hata 10 hawana! ..
  wajipange kwanza kuanza kujuulikana vijijini ambapo ndio kuna wapiga kura wengi zaidi.
   
 4. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,211
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 180


  Bad logic. Kabla ya TANU kuanza kujipanga kuongoza Tanganyika ilikuwa na viti vingapi?

  CHADEMA iongoze maandamano ya kudai mazungumzo ya kubadili katiba. Lazima kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi kwanza. Kwa sasa CCM inazunguka ikitishia kuwafukuza kazi viongozi wa Tume ya Uchaguzi. Hilo litabadilika kama Tume ya Uchaguzi itachaguliwa na vyama vyote, na kuajibika kwa Bunge na sio kwa Rais.

  Dr. Slaa is Presidential material. Akisimama atakumbatiwa na wananchi. He has name recognition and is charismatic. Na ni sumu ya CCM.
   
 5. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu Augustine Moshi hivi Mzee Slaa unamjua vizuri? Au na wewe umeingia kichwa kichwa kwenye ushabiki wa kutaka Slaa agombee Urais? Si kila king'aacho ni dhahabu!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu mfumo wa Tanzania siyo kama Marekani ambapo bunge linaweza kushikiliwa na chama kimoja halafu serikali ishikiliwe na chama kingine. Ili raisi kuweza kuongoza ni lazima awe na majority bungeni na kama ikitokea hana itamlazima aunde alliance na chama/vyama vingine kupata majority ya kuunda serikali. Katiba ya Tanzania ni kwamba waziri mkuu na mawaziri watatoka kwenye chama chenye idadi kubwa zaidi ya wabunge. Sasa Chadema washinde uraisi halafu majority iwe CCM hiyo serikali itakuwa ya nani? Chadema au CCM? Kuwa na idadi ya kutosheleza ya wabunge na uraisi go hand in hand, one can't exist without the other.
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu yaelekea unamjua vilivyo Dr. Slaa. Hebu tueleze basi unavyo mjua wewe. It's good to look at both sides of the shilling.
   
 8. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,211
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 180
  Sala yangu ni Chadema ishinde Urais na ipate wabunge wengi kuliko chama kingine chochote.

  Kama Watanzania wanataka mabadiliko katika hali yao ya maisha, itabidi wabadilishe chama tawala. CCM imeshindwa kuwaletea nafuu yoyote.

  Nijuavyo mimi Dr. Slaa ni kiongozi jasiri, na mwenye uwezo mkubwa wa kuongoza.
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Waachane na Urais, wajikite kwenye kuliteka Bunge kwanza, wakifanikiwa kuliteka hilo, watafanya mabadiliko yote ya sheria na katiba yatakayowarahisishia kuupata urais
   
 10. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu hapo umenena. Tatizo inaelekea vyama vingi vya upinzani havina short term na long term plans. hawajui nyumba inaanza kujengwa msingi then mnapanda juu. Vyama vya upinzani haviwezi kushinda uraisi kwa sasa ambapo hata wakiungana they are still are minority kwenye bunge.
   
 11. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mwanafalsafa ukitaka nyeti za Mzee Slaa kaa na aidha Cardinal Pengo au Askofu Kilaini wakueleze vizuri,kama wakikubali waombe wakueleze ya Episcopal Council miaka ya 80 na early 90's.................etc.

  P.S: Omuhaya ati 'Kitandugao'!!!!
   
 12. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu nadhani wengi wetu hapa pamoja na mimi hatuna ukaribu wa kiasi hicho wa kumfuata Pengo au Kilaini mpaka wakawa tayari kuongelea kitu kama hicho. Ndiyo madhumuni ya JF, kupata habari ambazo wengine tusingeweza kuzipata sehemu yoyote nyingine. Kama member mwenzetu mkuu ingekua vizuri ukatueleza. Lakini kama hauwezi hamna neno mkuu maana siwezi kujua your position mkuu.
   
  Last edited: Jun 30, 2009
 13. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Huu sasa ndio unaitwa umbea bin umbea. Wewe umeambiwa ueleze hizo kasoro za Dr. Slaa (kama unazijua) unasema nendeni kwa Cardinal Pengo...
   
 14. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mwanafalsafa,with due respect kwa uhuru wa kulonga ndani ya JF kwa hili mimi naomba Kanisa Katoliki likitaka ndo liongee,nisamehe ndugu yangu.
   
 15. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu sawa nimekuelewa lakini siyo vizuri kutoa madai bila kuthibitisha. Maana hapa umesha jenga perception fulani kwetu juu ya Dr. Slaa na unakua haumtendei haki kumtolea madai bila kutoa maelezo. Ni sawa sawa na umetuambia tu kuwa we should just take your word for it.
   
 16. I

  Idda Member

  #16
  Jun 30, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wandugu,
  Kwanza salamuni.
  Mada kuu ni nzuri sana.
  Tujadili mada hasa kwa uwezo wa chama na siyo kubishana kuhusu watu wa chama.
  CHADEMA yaweza kuongoza nchi?
   
 17. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kuongoza wanaweza. I don't think anyone can do much worse than CCM has already done. Tatizo ni kufikia huko kwenye kuongoza nchi.
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Naona kama wajikite kwenye kampeni za ubunge na udiwani mpaka vijijini. Hii itawapa wananchi option ya nini wachague.Ilivyosasa vyama vya upinzani vipo mijini tu. Wananchi wengi wa vijijini hawavitambui mpaka wakati wa uchaguzi.Sio rahisi kushinda chama tawala chenye mizizi mpaka huko chini.
   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Tujiulize na sisi wenyewe humu ndani tunagombea nafasi zipi uchaguzi ujao na kwa vyama vipi au tunabaki kama tulivyo kutumia majina bandia, kuwatukana walioko madarakani na kutukanana sisi wenyewe, kuonyesha tuna uchungu na nchi yetu kwenye mitandao huku tukila kuku kwa mrija nje ya Nchi yetu,.....
  Hakuna CHAMA cha kuiondoa CCM madarakani au Bungeni kwa miaka kadhaa ijayo endapo vyombo vya DOLA havijaridhia. Tuvielimishe vyombo hivi kwanza hasa UwT na Polisi.
   
 20. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu tunavilimishaje? Hebu tupe njia ambazo wewe ungezi tumia kuvielimisha hivi vyombo vya dola. Maana mimi naona tatizo la vyombo vya dola vina tokana na mamo makuu mawili:
  1.Kuna nafasi nyingi sana ambazo mtu huteuliwa na raisi na anaweza kuondolewa muda wowote raisi atakapo amua. Hivi nafasi ni pamoja na msajili wa vyama, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, mkurugenzi wa UwT, mkurugenzi wa Takukuru nk. Sasa watu hawa unategemea uwaminifu wao utakuwa wapi kama siyo kwa raisi? Na tunajuaje kama wenyewe hawapewi hizo nafasi on the basis of being loyal members of CCM?

  2.By default watu huogopa aliye juu yake. Kwa hiyo unakuta mtu anafanya yale yanayo mpendezea CCM bila kujijua kwa maana mtu anataka kumridhisha boss.

  Mimi ushauri wangu ni kwamba tuangalie vizuri hizi nafasi zinazo teuliwa na raisi zina madhara gani. Kama mtu kula yake ina tegemea furaha ya raisi hata uumpe somo vipi hata kuelewa. Leo hii hata wewe Wilcard kama unamtegemea mtu kwa ajili ya maisha yako hata nikueleze vipi hafai huto nisikiliza and that is human nature.
   
Loading...