Uchaguzi mkuu umekaribia.....

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125




Kidole na Mdudu

Yarabi nipe hamasa, waja niwape pazia
Napata shauku sasa, mjengoni kuzungumzia
Kupata yanayopasa, hakika siyo kazia
Mdudu aumaye, upuuzi kumpa kidole

Hebu tizameni hasa, wajao kupakazia
Mbio kasi waja hasa, wenzao kupakazia
Hawatuambii sasa, yepi watazungumzia
Mdudu aumaye, upuuzi kumpa kidole

yepi watazungumzia, mjengoni wakiingia
hata tu wakikazia, majungu watakimbia?
Hatapo wakikazia, aibu watakimbia?
Mdudu aumaye, upuuzi kumpa kidole

Hila zimewazidia, maneno wakidandia
Hata kutwa yawadia, sera hajatuambia
Kote hakuna fidia, wanavyotuharibia
Mdudu aumaye, upuuzi kumpa kidole

Uchaguzi wawadia, hata hawana hisia
Kutwa tu kushadadia, vitambi tu wasifia
Wengine hutuambia, muda hakusaidia
Mdudu aumaye, upuuzi kumpa kidole

Wakipata kuingia, eti wanatuambia
Bure hawataishia, maendeleo ya mbia
Hima watasaidia, huduma watuambia
Mdudu aumaye, upuuzi kumpa kidole

Ni bure waturingia, siku zote twawajua
Mjengoni wakiingia, tumboza husaidia
Wadhani hatuna nia, waja kujisaidia
Mdudu aumaye, upuuzi kumpa kidole

Mwisho wao wawadia, mara hii twawajua
Mjengoni hatafikia, yule asiyetujua
Hatutaki kufikia, kwake asiyetujua
Mdudu aumaye, upuuzi kumpa kidole
 
Back
Top Bottom