Uchaguzi Mkuu Nigeria waahirishwa! Tume ya Uchaguzi yasema hakuna shinikizo la Kiusalama wa Kisiasa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,552
2,000
Uchaguzi Mkuu nchini Nigeria uliokuwa ufanyike leo Jumamosi Februari 16 umeahirishwa kwa wiki moja.

Tume huru ya uchaguzi nchini humo imetangaza uahirishwaji huo zikiwa zimesalia saa tano kabla ya vituo vya kupigia kura vifunguliwe kote nchini.

Uamuzi huo, kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Mahmood Yakubu umetokana na changamoto mbalimbali zinazohitaji kutatuliwa

UPDATES:
Huku wagombea uchaguzi nchini Nigeria wakishutumiana kwa tangazo la ghafla la kuahirishwa uchaguzi, tume ya uchaguzi inasema kuwa tangazo hilo halikushinikizwa kisiasa wala kiusalama.

Wagombea wakuu wa uchaguzi nchini Nigeria wanatupiana lawama kutokana na uamuzi wa ghafla uliochukuliwa na tume ya uchaguzi kuahirisha uchaguzi wa rais kwa wiki moja hadi hapo tarehe 23 Februari, kila mmoja akimuotezea kidole cha lawama mwenzake, ingawa wote wakisisitiza haja ya utulivu.

Uamuzi huo uliotangazwa masaa matano tu kabla ya vituo vya kura kufunguliwa siku ya Jumamosi unatajwa kuigharimu nchi hiyo dola bilioni 2 za Kimarekani, sambamba na kuiathiri hadhi ya taifa hilo kubwa kabisa kufuata mfumo wa kidemokrasia barani Afrika.

Kwa sasa, mamlaka zinazohusika na uchaguzi zina kazi ya kuamua namna ya kuvifanya vifaa vya kupigia kura ambavyo tayari vilishawasilishwa kwenye vituo vya kupigia kura, huku hali ikiwa ya wasiwasi kutokana na matukio ya hivi karibuni ambapo majengo ya tume ya uchaguzi yalichomwa moto.

Tume ya Uchaguzi yakanusha kuingiliwa kisiasa
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, Mahmood Yakub, aliwaambia waangalizi, wanadiplomasia na waandishi wa habari kwamba kucheleweshwa huku kwa uchaguzi hakuhusiani na hali ya ukosefu wa usalama wala kuingiliwa kati kisiasa. Badala yake, mwenyekiti huyo alisema "mazingira mabara" ikiwemo hali mbaya ya hewa ndiyo iliyopekelea kuchelewa kwa ndege zilizobeba vifaa na pia moto kwenye ofisi tatu za tume yake.

Ikiwa uchaguzi ungelikwenda kama ulivyokuwa umepangwa, vituo vya kura visingeliweza kufunguliwa kwa wakati mmoja nchi nzima. "Ni muhimu sana kwa wananchi kuupokea uchaguzi ulio huru, wa haki na wenye kuaminika," alisema Yakub, akiongeza kwamba hadi saa nane usiku walikuwa na uhakika kwamba uchaguzi ungelifanyika, huku akihakikisha kuwa tarehe 23 Februari haina mjadala tena.
=====

Nigeria's presidential and parliamentary elections have been delayed for a week.

The Independent National Electoral Commission (INEC) made the announcement just five hours before the polls were due to open on Saturday.

"Proceeding with the election as scheduled is no longer feasible," commission chairman Mahmood Yakubu said, citing logistical issues.

He said the difficult decision was needed to ensure a free and fair vote.

The presidential and parliamentary votes have been rescheduled for Saturday 23 February.

Governorship, state assembly and federal area council elections have been rescheduled until Saturday 9 March.

The announcement came after an emergency meeting at the INEC headquarters in the capital, Abuja.

Nigeria's two main political parties, the ruling All Progressives Congress (APC) and the People's Democratic Party (PDP), swiftly condemned the move and accused each other of trying to manipulate the vote.

Why have elections been postponed?
Mr Yakubu said the decision was made following a "careful review" of the election "operational plan", adding that there was a "determination to conduct free, fair and credible elections".

He said the delay was necessary to give the commission time to address vital issues and "maintain the quality of our elections", but did not provide further details.
 

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
6,606
2,000
Demokrasia ni mchakato ila angalau wenzetu wa huko Afrika Magharibi wanaonyesha dhamira ya kweli, sio kama sisi wa kulazimishwa lazimishwa kuunga mkono juhudi.
 

Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,657
2,000
Duh! Miaka mitano ya maandalizi haikutosha na matatizo yake yatatuliwe kwa wiki moja iliyoongezwa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom