Uchaguzi Mkuu kusimamishwa?

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Kuna habari kuwa uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka huu huenda usifanyike endapo serikali itaendelea na msimamo wake wa kutoruhusu mgombea binafsi inasemekana kuwa mawakili mbalimbali wakishirikiana na Mwenyekiti wa DP Mchg. Christopher Mtikila na vyama vingine wamejipanga vilivyo kwenda mahakamani mara hukumu itakapotolewa kuruhusu mgombea binafsi ili kusisitiza hukumu hiyo itekelezwe

Tetesi kutoka kwa mawakili zinapendekeza kuwa endapo kama serikali itaona muda uliobaki hautoshi kuandaa mgombea binafsi basi uchaguzi uahirishwe hadi Februari mwaka ujao au hadi serikali itakapokuwa tayari, hukumu hiyo imepangwa kusikilizwa tena April 8 ingawa serikali iliomba muda wa miezi minne kujiandaa iliyopingwa na Mahakama ya rufaa

Je tetesi hizi ni za kweli?
 
Hilo haliwezekani Tanzania. Mahakama za Tanzania haziwezi kamwe kufanya uamuzi kama huo. Ndio maana hata viongozi waandamizi wa serikali (Deputy AG) na wanasiasa (Philip Marmo) wamekuwa wakitoa taarifa za kusisitiza kuwa mgombea binafsi hataruhusiwa kwenye uchaguzi ujao.
 
Yaleyale kama Zanzibar. Kuna kuchaguana basi nchi hii? Mgombea binafsi wa nini wakati huu? Hata kutafuta mchumba tu hauwi mgombea binafsi! Mnataka akina RA, EL, Mzee Mengi, Manji, Mtume na Nabii Mwigira, Kakobe, Sheikh Ponda, Prof Majimarefu, Dr Remmy Ongara, .....wagombee Urais?
 
Tanzania ni nchi ya pekee ndio maana Mahakama tena Jaji Mkuu akiwamo, inatoa tamko anatokea Waziri kama Marmo anasema "Hakuna".... sasa kama anajua watashinda kesi anawezaje kutoa tamko tena bungeni, kwani hiyo pekee ni kuingilia mahakama na ni kosa la jinai ambalo anaweza kushitakiwa na kuhukumiwa. Wanasheria nisaidieni.
 
Haya aliyasemea Bungeni hana wa kumshtaki. Baba wa watu kasema yaliyo moyoni mwake na kwa kuzingatia "hali halisi" kama lilivyo jina lako.
 
Haya aliyasemea Bungeni hana wa kumshtaki. Baba wa watu kasema yaliyo moyoni mwake na kwa kuzingatia "hali halisi" kama lilivyo jina lako.

well kama Marmo kasemea bungeni hawezi kushitakiwa mbona kuna wabunge wengine huzuiwa kuzungumuza bungeni mambo yaliyo mahakamani wakati mwingine hukalishwa chini au kupewa karipio na Spika huoni hiyo ni double standard?
 
Kama ulimsikiliza vizuri alikuwa anaongelea muda. Ni swala ambalo litahitaji kubadili KATIBA. Linahitaji mchakato mrefu kidogo. Hukumu ya mahakama haibadili katiba automatically.
 
Hii kesi bado inawapasua kichwa vigogo wa CCM ambao wamezoea kuwadhibiti wabunge watukutu [vigezo vyao] kwa kutumia vikao vya chama eg NEC & CC.Wagombea binafsi kwa mawazo yangu wataongeza chachu ya demokrasia Tanzania ambayo kwa kiasi kikubwa imekandamizwa na huyu mdudu CCM.Tunaweza kumdharau Mtikila lakini anaweza kuja kufanya mambo ya ajabu kwa kusimamisha uchaguzi mkuu mwaka 2010.
 
CCM watakapoona mahakama imewabana kisawasawa walitalisukuma suala hili kwenye kura ya maoni. Wana mbinu na njia nyingi za kutokea. Kwa kifupi ni kwamba wasichotaka CCM kifanyike nchi hii hakitafanyika.
 
Uchaguzi Mkuu hauwezi kusogezwa mbele kwa sababu hiyo, hata huo uamuzi wa mgombea binafsi, utahusisha wagombea ubunge na udiwani tuu, na sio urais, kugombea urais, itabakia hivyo hivyo kwa sharti la kudhaminiwa na chama, na ikikubaliwa mgombea binafsi hadi urais, them wataweka sharti kuwa mgombea binafsi asiyedhaminiwa na chama, atajigharimia kampeni.

Kwa sasa, kila mgombea urais uchaguzi ujao, atahudumiwa kwa kupewa ulinzi na free publicity kwenye media ya umma pamoja na kupatiwa kitita na Milioni 50 za kujikimu. Wakijitokeza watu 100, wengine target yao ni kujipatia tuu hilo fungu la kujikimu itakuwaje?.
 
CCM watakapoona mahakama imewabana kisawasawa walitalisukuma suala hili kwenye kura ya maoni. Wana mbinu na njia nyingi za kutokea. Kwa kifupi ni kwamba wasichotaka CCM kifanyike nchi hii hakitafanyika.

Wewe umewaelewa vyema hawa watu ni wa kupindua pindua matakwa ya watanzania ndo maana kinaitwa chama cha mapinduzi.Watanzania wanapaswa kujua kwamba ni lazima kazi ya ziada ifanyike ili kuleta mabadiliko ya kweli yatakayowanufaisha wengi.

Kwa hali ilivyo sasa CCM itaendelea kusuppress demokrasia mpaka watanzania kwa umoja wao wasimame na waseme enough is enough huku wakimaanisha.Vinginevyo ngoma zitaendelea kuchezwa na nyimbo nyingi tuu zitaimbwa lakini demokrasia haitatekelezwa Tz.
 
Yaleyale kama Zanzibar. Kuna kuchaguana basi nchi hii? Mgombea binafsi wa nini wakati huu? Hata kutafuta mchumba tu hauwi mgombea binafsi! Mnataka akina RA, EL, Mzee Mengi, Manji, Mtume na Nabii Mwigira, Kakobe, Sheikh Ponda, Prof Majimarefu, Dr Remmy Ongara, .....wagombee Urais?
Haki ya Watanzania "shouldn't be raped for whatever means by the so called rulers" What is a problem wakirihusu hiyo? Waruhusu tu. watakaoshinda kwa mwelekeo huo ni wachache sana na sana sana sio kwa nafasi ya rais. JK will win and that has no doubt!! Whowever says no, he is blinding himself. He will win not necessarily on performance but on the background that we used to have whereby more youths do not want to come out and vote or they don't go campaign meetings/rallies so that they can make informed decisions. People are still not educated well about haki zao na wanadhani vitu wanavyopata kama vipo ni kwa hisani ya serikali ya CCM. Na ndiyo hata maana DC wa Tarime amediriki kusema mapambano ya kikabila ni kwa sababu wamechagua Chadema...huyu nadhani ni mvivu wa kusoma historia na ni mwongo kwani hata kabla ya vyama vingi huko tarime bado walikuwa wanapigana, je huko rorya, nayo Chadema imeshinda??? ndiyo viongozi tulionao, wanawapotosha wananchi!
 
Kama ulimsikiliza vizuri alikuwa anaongelea muda. Ni swala ambalo litahitaji kubadili KATIBA. Linahitaji mchakato mrefu kidogo. Hukumu ya mahakama haibadili katiba automatically.

Ndugu WC
nafikiri hapa suala si kubadili katiba hukumu iliyoko ni utata wa katiba yenyewe sehemu moja inaruhusu nyingine hairuhusu Mtikila anachosema ni katiba iheshimiwe kwa hiyo kama atashinda kesi katiba haitabadilishwa kwa sababu imeshasema wazi kila mtu ana haki ya kupiga na kupigiwa kura kinachotakiwa kubadilika ni sheria tu za uchaguzi na si katiba.
 
Hao watu washeria wametafakari gharama za kuahirisha uchaguzi..Do they know concequences ya kupostpond,Gharama yake itakuwa kubwa kul;iko hata ya mgombea binafsi..By the way kama Rais hana good will na hili uchaguzi utafanyika tu..Rais yuko juu ya vyote.
 
Ndugu WC
nafikiri hapa suala si kubadili katiba hukumu iliyoko ni utata wa katiba yenyewe sehemu moja inaruhusu nyingine hairuhusu Mtikila anachosema ni katiba iheshimiwe kwa hiyo kama atashinda kesi katiba haitabadilishwa kwa sababu imeshasema wazi kila mtu ana haki ya kupiga na kupigiwa kura kinachotakiwa kubadilika ni sheria tu za uchaguzi na si katiba.
Soma KATIBA yetu ibara ya 39(1)(c). ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
 
Yaleyale kama Zanzibar. Kuna kuchaguana basi nchi hii? Mgombea binafsi wa nini wakati huu? Hata kutafuta mchumba tu hauwi mgombea binafsi! Mnataka akina RA, EL, Mzee Mengi, Manji, Mtume na Nabii Mwigira, Kakobe, Sheikh Ponda, Prof Majimarefu, Dr Remmy Ongara, .....wagombee Urais?

Kwani hawa watu hawana haki ya kugombea hiyo nafasi ya urais?

Kumbe nawewe umeanza kampeni za JK awe mgombea pekee, apite bila kupingwa.

Suala la mgombea binafsi ni umiza vichwa kwa vyama vyote vya siasa, kwani wanajua hawatakuwa na uwezo tena wa kulazimisha wabunge kuwa kasuku.

Asiyekubaliana na maamuzi ya chama wakimuwekea mizengwe anasimama peke yake!!!

Manake kuna watu kwenye vyama vya siasa wamevifanya mali ya familia kwakuwa tu alishiriki kukianzisha, au baba/babu yake alikuwa muanzilishi basi wanataka waendelee kuwa wao tu.

Mgombea binafsi akiwepo kwenye uchaguzi itapunguza fitna ndani ya vyama na zaidi itasaidia vyama kuweka maslahi ya nchi mbele badala ya maslahi ya chama mbele.
 
Soma KATIBA yetu ibara ya 39(1)(c). ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;

Soma KATIBA hiyo hiyo ibara ya 21(1) inasema

21​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
 
Back
Top Bottom