Uchaguzi Mkuu CCM:: MAAMUZI YA NEC:: Wenye kupitishwa wapitishwa, wengine watupwa

Hii ni pumba imepostiwa hapa,unajaribu kugeuza maana za maneno aliyozungumza kikwete ili upate wajinga wa kuwadanganya muendelee kujazana ujinga.
 
Kikwete leo amefungua kikao cha NEC ya CCM kilichotanguliwa na Kamati Kuu na Kamati ya Usalama na Maadili. Amewaacha mdomo wazi akina Lowassa aliposema wamekata majina ya watu wengine japo wanazo sifa na wengine wamepungukiwa sifa kwa makusudi ili kujenga chama chenye ari mpya na vijana wengi wasomi ambao ndiyo future ya chama hicho. Aliwamaliza zaidi aliposema "tunaunda timu ya ushindi wa chama na si timu ya ushindi wa mtu." hapa kama ni kisu basi kimegonga mifupa ya akina Lowassa wakabaki midomo wazi nilikuwa nawatazama vizuri walivyokaa katika siti moja Lowassa, Sumaye na Kingunge huku wapambe wao akina Mgeja wakilia kupoteza nafasi. Tena Kikwete amewaeleza anajua mjadala wa kwa nini fulani kakatwa jina na mwingine yupo utakuwepo lakini chama kwanza na anayetishia kuondoka ccm kwa kukatwa jina atangulie mapema wanamtakia kila la kheri, anasema anashangazwa na mtu anapoanza kusema chama kibaya pale anapokosa fursa ya uongozi. Ritz upo? asubuhi niliona umeleta uzi wa kumsifu Lowassa.

umejitahidi kweli kumlisha kikwete maneno kwa manufaa yako na wafuasi wako,haya utawapata wasioshughulisha bongo zao.
 
Ndugu si Vyema kutumia neno la Mungu, kwa kejeli!
Lets politics run on the lines of politics and lets the words of God run on the line of God's words.
(‘‘Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya kuzimu hayataweza kulishinda.)
 
Hata mimi sijaona ni kivipi amemkatisha tamaa,JK anakula kotekote ili yeyote atakayeshinda asimbugudhi.JK will never be straight,si JK huyu tunayemfahamu.Hawezi kumgeuka EL moja kwa moja na wakati dili la Richmond lilikuwa lao wote na alijiuzulu kumnusuru.JK ni msanii msiingie mkenge,wapi magamba aliyomtuma Nape atoe siku 90?Hamna kitu hapo.

Kwani toka alipompigia kampeni ni kipi kimebadilika?RA ni woga wake tu,hata yeye angeweza kugoma,sema kunguru mwoga ukimbiza bawa lake.

Mkuu hata RA sio uoga alitumika kwa makubaliano ili kuwatisha wezake kina Vijisnti na EL waogope wamwage manyanga...lkn jamaa wakachanganya na za kwao
 
Vikao vinaendela ndani ya ukumbi wa NEC Dodoma, ambapo katika hali ya kutatanisha na isiyotarajiwa na wengi ni kwamba, nafasi ya Makamu Mwenyekiti inakwenda kwa wanawake ambao ni Theresia Mtewele, Faiza Salimu na Cresency Maindo.

Wakati hali ikiwa chanya kwa wagombea kutoka Zanzibar, nafasi ya Mwenyekiti majina yaliyopita ni Thabiti Jecha Kombo, Nadra Hamis na Vuai Amdan.

Hali hii imewastua viongozi wa UVCCM pamoja na waliowatuma kwenye kinyan'ganyiro hicho.
Vilio na nderemo vinatawala mjini Dodoma Usiku huu.

Souece: Mjumbe makini wa NEC na CC
 
Mkuu hata RA sio uoga alitumika kwa makubaliano ili kuwatisha wezake kina Vijisnti na EL waogope wamwage manyanga...lkn jamaa wakachanganya na za kwao
Mkuu mimi watu wanafiki nawachukia kama wauwaji tu,JK ni mnafiki vibaya mno!Sasa kumbe EL alimshtukia?Ngoja tuone ni kivipi watamtimua EL kama wana ubavu huo,wataishia kutulia wanyolewe.Otherwise chama kitampasukia mikononi,uzuri wa unafiki ni kwamba una mwisho wake.Na mnafiki mara zote huumbuka kwasababu at the end hakuna anachokisimamia.
 
pole zao vipandikizi waliokatwa!kilio kwao waliokuwa wamewapanda!hapo chacha!jamani hosp zitakula vichwa vinono wiki hii!presha kibao!
 
Usishangae hatawagombea urais 2015 ndo itakavyokuwa, magamba wananipa raha kila kifo chao kinapokaribia
 
Hao vijana wanaondaliwa ni wepi, Nchemba? au Ngeleja? Au Adam Malima?

Tukiachana na mambo ya kashifa ambazo hatuna huakika nazo, mimi binafsi huwa naona Mh Ngeleja pamoja na mapungufu yake kam binadamu wengine lakini ni mtu anaye jiamini sana na anajuwa sana kujieleza, sina uhakika kama mambo ya wizara yake alihusika kweli au aliamini watendaje wake ambao walim-let down! NGEREJA ni mtu mahili sana - kama atagundulika hana kosa basi ni vyema alirudishwe kwenye CABINET.

Mtu mwingine ambaye huwa namuona ana busara sana na mwenye uchambuzi wa hali ya juu ni kijana ADAM MALIMA - anajuwa sana kujieleza na kufafanua mabo kwa kina, mpeleke wizara yoyote mpe three weeks alafu muhulize swali lolote kuhusu wizara husika - utashangaa atakavyo jibu swali lako, mtu unaweza kufikili alishakaa kwenye wizara miaka. Juzi juzi hapa niliona alivyo kuwa anajibu maswali kuhusu wizara ya kilimo ambayo alikuwa amehamia karibuni tu, hata kama walikuwa wamemwandikia baadhi ya majibu lakini additional questions ambazo hazina majibu ya moja kwa moja alikuwa anayamudu sana, mtu unamuona ni mtu mwenye akili sana, sijuhi kwa nini hapewi Uwaziri kamili - mambo mengine ya ujana yasimukwaze bwana mradi anajuwa kupiga mzigo.
 
Duh, pole sana Antony Mavunde. Umepewa mtihani wa kubadili jinsia kama Sitta kwenye uspika, umeshindwa.
Kaa chini, tafakari, chukua hatua.
 
Takukulu kila siku tutachunguza hiki, tunachunguza kile hakuna lolote. uchaguzi wa mwaka 2010 mlikamata watu kibao
lakini hakuna kesi hata moja mliyoweza kushinda ingawa wagombea wengine wa ccm walikamatwa live wakigawa rushwa
kama Dr. Beth machangu aliyekamatwa chumbani guest house akigawa rushwa, mke wa sitta saa kumi usiku na bahasha
zake zilizojaa fedha na yule baba wa shinyanga aliyekamatwa anagawa vichwa vya cherehani live. mapendekezo yangu Takukulu ifutwe pesa zitumike kununua madawati ya watoto mashuleni.
 
Mkuu hata RA sio uoga alitumika kwa makubaliano ili kuwatisha wezake kina Vijisnti na EL waogope wamwage manyanga...lkn jamaa wakachanganya na za kwao

Mkuu ni kweli RA alitumika kimakubaliano na mkakati wao ulifanikiwa kwa 100%, EL na AC walimtanguliza kujilipua ili CCM waone uchungu wa kupoteza majimbo kwa upinzani na walishajipanga kulipoteza lkn JK akasoma alama za nyakati akamuangukia RA awasaidie kwenye kampeni si unajua RA ni mfanya biashara sio mwanasiasa kivile hivyo hana alichopoteza, kwa tabu waliyopata Igunga wakafyata kuwagusa wengne hivyo mpango ukatimia.
 
Kama EL anaujuwa utajiri wa Riziwani basi haendi mahali.Kwasababu anafahamu kuwa JK si mpinga mafisadi,sanasana ataona ni kama amechaguwa fisadi jingine badala yake yeye.Yani ataona kama anapendelea fisadi mwingine na siyo kwamba eti anaupinga kwa kuteuwa mtu safi.Ukichukulia na the fact kwamba alijiuzulu kumlinda,haendi pahala na hakuna kitu JK atamfanya,i said the same thing kuhusu Mkono...

Msiingizwe mkenge,nashangazwa sana.
 
Back
Top Bottom