Uchaguzi Mkuu CCM:: MAAMUZI YA NEC:: Wenye kupitishwa wapitishwa, wengine watupwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi Mkuu CCM:: MAAMUZI YA NEC:: Wenye kupitishwa wapitishwa, wengine watupwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bagwell, Sep 25, 2012.

 1. b

  bagwell Senior Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vigogo kadhaa wakiwamo wabunge wameenguliwa katika mchakato wa uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Majina ya vigogo hao yaliondolewa na Kamati ya Maadili iliyoketi mjini hapa kwa siku tatu mfululizo chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo.

  Rais Kikwete jana asubuhi alisema kazi ya kupitia majina ua wagombea ilikuwa ni ngumu na kwamba Kamati ya maadili ilifanya kazi nzuri na itafanya vikao vinavyofuata kwenda kwa kasi nzuri.

  Akifungua kikao cha Kamati Kuu (CC), Rais Kikwete alisema kuwa Kamati ya Maadili imekuja na mapendekezo mengi tofauti na yale yaliyoliyopendekezwa na vikao vya mikoani.

  Rais Kikwete alisema Kamati ya Maadili imefanya kazi ya kupitia jina moja hadi jingine ili kufahamu kwa nini waliochwa kupendekezwa wamefanyiwa hivyo.

  “Tumefanya kazi ya kupitia jina moja hadi jingine kuona nani amependekezwa na wasiopendekezwa na kwa nini wameachwa na kuna maeneo tumekuja na mapendekezo tofauti na yaliyotolewa mikoani kwa sababu mbalimbali,” alisema.

  Alisema wagombea 2,853 waligombea nafasi mbalimbali ndani ya chama na wengine 2,104 waliwania mafasi za uongozi kupitia jumuiya za chama hicho.

  Taarifa kutoka ndani ya chama hicho ambazo imelifikia gazeti hili jana, zilisema kuwa waliodaiwa kuenguliwa na kikao hicho ambacho kilimalizika juzi saa 9:30 usiku, ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, anayetetea nafasi yake.

  Wengine ni Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe anayewania nafasi ya uenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama hicho (UWT) mkoani Tabora na Mbunge wa Kahama, James Lembeli.

  Kada mwingine ambaye taarifa za uhakika zinaeleza ameenguliwa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mkoani Dodoma, Antony Mavunde, ambaye anagombea Makamu Mwenyekiti Taifa.

  Habari zaidi za uhakika zinasema kuwa wengine ambao majina yao yameondolewa katia orodha ya wagombea ni wabunge Victor Mwambalaswa (Lupa) na Godfrey Zambi ( Mbozi Mashariki).

  Zambi na Mwambalaswa walikuwa wanagombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya.

  Hata hivyo, chanzo chetu kimesema kuwa kuna vigogo wengine ambao wamependekezwa waenguliwe na hivi sasa wanasubiri huruma ya vikao vya CC na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, baadhi wabunge waliowania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama, majina yao yamepitishwa.

  Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema CC imekuwa ikitumia busara katika kupitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali kwa maslahi ya chama.

  “Hata kanuni inasema kuwa anaweza kugombea kwa kibali maalum cha Kamati Kuu. Majina yanapofika tunasema huyu ni mbunge, tunaangalia je, inafaa tena kugombea nafasi nyingine inaporidhika basi inatoa kibali kwa mtu kuwania nafasi ya uongozi,” alisema.

  Alisema CC imewahi kuruhusu na kukataa maombi ya watu mbalimbali kwa hivyo hilo halitakuwa jambo geni kama litatokea katika vikao vinavyoendelea.

  Chanzo hicho kilisema kuwa Kamati ya Maadili iliamua kurahisisha kazi ya vikao hivyo kwa kuchambua jina moja baada ya jingine na kutoa mapendekezo yao kulingana na sifa walizonazo wanaomba kugombea nafasi hiyo.

  Nape alipoulizwa na gazeti hili jana kuhusiana na taarifa za vigogo hao kuenguliwa, hakudhibitisha wala kukanusha taarifa hizo zaidi ya kusema kuwa hayo ni maneno ya barabarani.

  Pia Nape aliwahi kukaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa vikao hivyo siyo vya mwisho kutoa maamuzi na kuwa maamuzi hayo yanaweza kubadilishwa na vikao vingine.

  Kikao cha mwisho kutoa maamuzi ni NEC ambacho kinatarajiwa kuanza leo.

  CHEGENI, KAMANI WAWAGAWA VIJANA BUSEGA

  Jumuiya ya Vijana ya CCM (UVCCM) Wilaya ya Busega, imeingia katika mvutano baada ya mwenyekiti wake, Samuel Ngofilo, kutoa kauli yenye utata.

  Moja ya kauli hizo ni kwamba vijana wamemchukulia fomu ya kugombea ujumbe wa NEC, mbunge wa zamani wa Busega, Dk. Raphael Chegeni.

  Viongozi wa umoja huo wameitisha mkutano wa waandishi wa habari na kumkana mwenyekiti wao wakisema huo ni uongo na uzushi na kumtaka awaombe radhi.

  Katika mkutano huo kwenye mji mdogo wa Lamadi jana, vijana hao ambao ni wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya Wilaya ya Busega, walidai kuwa kitendo cha mwenyekiti wao kuzungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa kuna njama zimesukwa za kutaka jina la Dk. Chegeni likatwe kwenye kugombea nafasi hiyo ya ujumbe wa NEC pia ni uzushi.

  Pia walidai kuwa wameshangazwa na Ngofilo kumtuhumu Mbunge wa Busega, Dk. Titus Kamani, kwamba aliandika barua kwenda kwa katibu wa CCM mkoa wa Mwanza, akiomba jina la Dk. Chegeni lisipitishwe kwenda ngazi ya Taifa.

  Wakiongozwa na Juma Kaduka pamoja na Muddy Gimonge, walisema wakiwa kama wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya vijana wilaya ya Busega, wanashangaa sana kwa kauli tata za mwenyekiti wao na kwamba anataka kuwagawa vijana.

  Walisema kuwa kauli ya mwenyekiti wao hazikupitia kwenye vikao halali vya baraza au kamati ya utekelezaji UVCCM ya wilaya.

  “Tunakanusha vikali kwamba sisi kama vijana tulimchukulia fomu Dk. Chegeni za kugombea NEC kama mwenyekiti wetu alivyotangaza kwenye vyombo vya habari,” alisema Gimonge.

  Aliongeza: “Lakini pia mwenyekiti wetu amedai kuwa Dk. Kamani ameandika barua kwenda kwa katibu wa CCM mkoa eti jina la Dk. Chegeni likatwe kwenye kinyang’anyiro cha NEC, huo pia ni uzushi sisi kama vijana hatulijui jambo hilo.”

  Walisema kumuingiza Dk. Kamani katika mambo hayo ni kumuonea kwa sababu yeye siyo mgombea katika kinyang’anyiro cha NEC.

  Walisema kuwa katika kikao chao cha juzi kilichoketi katika kijiji cha Nyang’anga Kata ya Nyashimo, Baraza la UVCCM lilikuwa na ajenda moja ya kukamilisha uchaguzi wa Kamati ya Utekelezaji ya Wilaya ya Busega na wala hawakuwa na ajenda tofauti na hiyo.

  Juzi Mgofilo alikaririwa na vyombo vya habari akitoa kauli hizo, ikiwemo ya kusema kuwa vijana wa CCM wilayani hapa ndiwo waliomchukulia fomu Dk. Chegeni ya kugombea NEC na pia Dk. Kamani ameandika barua kwenda kwa katibu wa CCM mkoa wa Mwanza ili jina la Dk. Chegeni likatwe.
   
 2. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  huyo mgeja ilikuwa budi aondoke maana alionekana wazi kuwa si mwenzao
   
 3. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Hiki ni chanzo gani?? kama ni gazeti, ni gani?? la lini?
   
 4. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Je hawa nguli watakao mwagwa kwa fitna je watakuwa na uvumilivu? maana inasemekana ukienguliwa hapa ujue hata kwenye kura ya maoni ya kugombea ubunge 2015 hautaruhusiwa kwani hauna vigezo vya kuwa kiongozi!!Je baada ya hapo CCM kutakalika??
   
 5. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Mkuu source tafadhali
   
 6. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi nchini, Mh Kinana hakugombea tena Ubunge wa jimbo la Arusha mjini, kwa kuogopa hoja ya Uraia wake. Mh Makongoro Nyerere alishinda kwa Ticket ya NCCR- Mageuzi. Mwaka huu Mh Kinana ghafla anaamua kujitoa kugombea ujumbe wa halmashauri kuu ya CCM ya Taifa, basi kuna kashfa kubwa ameiona itamvunjia heshima yake.
  CCM baada ya JK kuchukua madaraka, ilimegeka, sasa hivi wanachofanya ni kuhujumu nchi
   
 7. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,897
  Likes Received: 5,359
  Trophy Points: 280
  imeguka mara ngapi
   
 8. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Mbona CCM imeshakuwa vipande vipande siku nyingi?
  Au ni CCM ipi unayo izungumzia?
   
 9. c

  chama JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Huu ni uzushi wa pro Chadema kama kawaida yao

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 10. E

  EMMANUEL NSAMBI JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sasa kama vikao vya chini vinapitisha jina kisha linaondolewa baadae demokrasia
  iko wapi?Kwanini isipigwe kura ijulikane ni nani anakubalika zaidi?Hapa Nape anataka
  tuamini kuwa hiyo ndiyo demokrasia?
   
 11. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Hili nalo neno. Tusubiri tuone..
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nachotaka kujua,,,how wajumbe wa kamati ya maadili clean they are?????kwa yeyote aniambie,na pia niwajue kwa majina yao,wakwanza BABA MWANAISHA AKA MWANAASHA
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  wanaoiombea ccm ife watakufa wataiacha-JK,
  sijui ndo alikua anawaambia aliowaengua au la
   
 14. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280

  Baba MwanaaAsha a.k.a mkweree hana ubavu wala MORAL AUTHORITY ya kuwatosa chenge na Lowassa kwenye kugombea Nec ya magamba!!
   
 15. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,233
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Acha wafu wawazike wafu wenzao...........!!
   
 16. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #16
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Bashe, kingwangala mh!
   
 17. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #17
  Sep 25, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kuwatoa mgeja na Lembeli ni utoaji kafara wa kihuni kwa ajili ya maslahi ya kisiasa ya majangili CCM, natabiri na Chenge atatolewa kuua nguvu upande mmoja. Chama hiki kimebaki chama cha kikundi cha watu.
   
 18. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #18
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ccm ilikufa kitambo
   
 19. magino

  magino Member

  #19
  Sep 25, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii kali ila kweli
   
 20. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #20
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Imekuwaje kwa Mke wa Rais, mtoto wake, nadhani na wajomba kibao wanaogombea. Nao wanaachwa au hao ndo wenye vibali maalumu?

  Chama kinakufa!
   
Loading...