Uchaguzi Mkuu August 2022: Je, ni zamu ya Raila Amollo Odinga?

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,814
2,000
Maisha ni safari ndefu sana

"Never say never"

Hatimaye vingunge wawili nchini Kenya Mh. Rais Uhuru Kenyatta na mtunduizi RAO (Raila Amollo Odinga) wanakutana huko PWANI kupanga mipango ya kwenda pamoja uchaguzi mkuu ujao.

Ni mipango ya kutengeneza mwamvuli utakaokuwa na vyama vya JUBILEE na ODM.

Upande wa pili Mh. Naibu Rais William Rutto naye anakusanya nguvu katika muungano wa chama cha UDA (United democratic alliance).

Siasa za Kenya zinafurahisha, kushangaza, kuajabisha sana 🤣🤣🤣

Waliokuwa marafiki sasa ni mahasimu.

Waliokuwa mahasimu sasa ni marafiki.

Kweli NEVER SAY NEVER

Je, RAO (Raila Amollo Odinga), BABA AGWAMBO, AKOM atakuwa Rais wa Kenya baada ya Mh. Uhuru Kenyatta?

#The time is not our best ally
#The time will tell

*****************

#KaziInaendelea
#NchiKwanza (Tanzania)
#SiempreJMT
 
Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
8,420
2,000
Sina hakika kama Gikuyu watakubali huo mchezo mchafu! Watasema kama hakuna Gikuyu wa kuchukua nafasi basi bora Kalenjin achukue kuliko Luo! Kwa ufupi Uhuru kamchezea rafu mwenzake aliyemsaidia kuingia ikulu (UhuRuto).
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,814
2,000
Sina hakika kama Gikuyu watakubali huo mchezo mchafu! Watasema kama hakuna Gikuyu wa kuchukua nafasi basi bora Kalenjin achukue kuliko Luo! Kwa ufupi Uhuru kamchezea rafu mwenzake aliyemsaidia kuingia ikulu (UhuRuto).
Kweli. Ila katika SIASA chochote kinawezekana.
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,814
2,000
Sina hakika kama Gikuyu watakubali huo mchezo mchafu! Watasema kama hakuna Gikuyu wa kuchukua nafasi basi bora Kalenjin achukue kuliko Luo! Kwa ufupi Uhuru kamchezea rafu mwenzake aliyemsaidia kuingia ikulu (UhuRuto).
👍
 
MastaKiraka

JF-Expert Member
Jan 10, 2015
1,912
2,000
2022 ni zamu ya hustlers Nation, Ruto amejitahidi sana kuandaa itikadi yake ya kisiasa isiwe na mrengo wa kikabila bali iwe inagusa taifa zima. Amefanikiwa pia kuwa Man of the show, atakachozungumza ama kufanya wapinzani wake ndio hukichukua kama agenda na kuanza kukijadili, suala hili linamuongezea sana mileage ya kisiasa. Wapinzani wake kadiri wanavyosua sua na kurushiana maneno inaonesha ni jinsi gani hawakujipanga ama kasi ya Hustler nation imewavuruga.

Baba a.k.a Man RAO issue ya BBI itamtafuna yawezekana ilikua ni agenda nzuri ila imekuja wakati mbaya, Ruto The chief Hustler anaitumia kama fimbo na kuwaaminisha wananchi wa kawaida ya kuwa hawa Dynasties wao wanafikiri kuhusu nafasi zao tu ndani ya serikali na matumbo yao tu.
 
🤣
 
Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
6,419
2,000
Ruto the hustler kwanza alitumia mbinu za lowasa kwanza nyumba za ibada misikiti na makanisa kaishaiteka, akaja kundi la vijana kamaliza halafu alishuka kwa machinga na mama nitilie, baadae akatafuta support kwa museveni na kagame, alipomaliza hiyo kazi akaingia Arusha kupumzika wiki moja, baada ya pale akawa na ziara mombassa akaenda kuvuruga akateka akina kingi, jicho pevu then kachukua mashangingi akina aisha jumwa pwani kaimaliza then kaandaa upinzani mkubwa kuipinga BBI hapo ujue wananchi wengi BBI hawaitaki kabisa maana inaonekana kupendelea royal families pekee ili wagawane vyeo, hapo sasa majority wako na hustler ikulu nyeupe labda hali ibadilike lakini kwa mbinu za Raila bado sijaona kama ataweza awamu hii kumpita hustler
 
May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,950

Sio 'alitumia' ndio anayotumia hata jana jpili alikuwa Kanisani akiendeleza siasa zake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom