Uchaguzi mkuu afrika kusini tarehe 8 mei 2019, EFF, chama cha mfano afrika, julius malema kiongozi wa mfano afrika

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
UCHAGUZI MKUU AFRIKA KUSINI TAREHE 8 MEI 2019, EFF, CHAMA CHA MFANO AFRIKA, JULIUS MALEMA KIONGOZI WA MFANO AFRIKA.

Na.Comred Mbwana Allyamtu
Sunday-5/Mei/2019.
Marangu,Kilimanjaro-Tanzania.

Tarehe 8 Mei mwaka huu yani siku ya Jumatano ni tarehe ambayo taifa la Afrika kusini wananchi wake watapiga kura katika uchaguzi mkuu wa kumtafuta rais wa taifa hilo kubwa kiuchumi Afrika, uchaguzi huu unatazamwa kama uchaguzi muhimu sana katika mustakabali wa taifa hilo, wachambuzi wa maswala kadhaa huutazama uchaguzi huu kama duru muhimu mno Katika uchumi, maswala ya aridhi, migogoro ya kisiasa pamoja na suala la xenophobia nchini humo.

Nilizungumza na mchambuzi wa sayansi ya siasa za Afrika na rafiki yangu wa mda mrefu Ilankunda Timu mapema jana huku tukiangazia hali ya uchaguzi huu huko Afrika kusini na nafasi ya chama cha EFF Katika uchaguzi huu.

Pamoja na yote nilimuhaidi kuwa ntaandika juu ya uchaguzi huo na muelekeo wa chama cha EFF Katika uchaguzi huu, kwakuwa leo Julius Malema na chama chake wanahitimisha kampeni zao huko Johanasbug itakuwa vyema tukafahamu hali ya siasa ilivyo na namna EFF inavyozidi kuimalika kisiasa.

Uchaguzi huu wa tarehe 8 Mei, 2019, ni uchaguzi mkuu wa 6 toka mwaka 1992 pale taifa hilo lilipoingia kwenye ukurasa mpya wa ukombozi (Freedom Charter). Hata hivyo uchaguzi huu vyama takribani 27 vitaweka wawikilishi wao kwenye ngazi mbalimbali za uwakilishi. Kuelekea uchaguzi huu mkuu, mpaka sasa wapiga Kura walioandikishwa ni milioni 26.8 kati ya hao milioni 26.7 ni wa ndani na laki 1.3 ni nje ya nchi.

Wapiga Kura wa ndani (Local Voters), Uandikishaji wake ulianza mapema toka Tarehe 10-11 Machi, 2018 na Tarehe 26-27 Januari, 2019. Katika mchakato huu wa uchaguzi vyama vyote vya Siasa Afrika Kusini walizindua kampeni ya kuhamasisha uandikishaji wa wapiga Kura kwa wananchi. Wanasiasa wengi waliwasisitiza vijana kujiandikisha ili waweze kupiga Kura chaguzi zinazofuata.

Tume ya uchaguzi ya Afrika kusini (EIC) kama ilivyoada ilitangaza kuandikisha wapiga kura wapya 700,000 kwa mwezi Januari, 2019 na 400,000 kwa mwezi Machi, 2018 na kufikia idadi ya wapiga Kura wapya 1.1 milioni. Tume ilijumlisha na wapiga Kura wa awali na kupata jumla ya wapiga Kura wa ndani 267,727,921.

Kwa upande wa Wapiga Kura wa nje (International Voters), Uandikishaji wake ulianza Tarehe 1-4 Januari, 2019 na Tarehe 14 Machi, 2019 Tume ilitangaza kupokea maombi ya watu 30,532 wanaoishi nje ya Afrika Kusini kupata nafasi ya kupiga Kura, katika hao maombi 29,334 mpaka kufika tarehe 14 March yalikubaliwa na wengine walikua kwenye mchakato wa kuwaandikisha.

Katika uchaguzi huu mkuu wa kumtafuta rais wa taifa hilo ambalo hutumia mfumo wa bunge kuunda serikali. Jumla ya viti vyote vya ubunge katika Bunge la Afrika Kusini ni 400, na viti vinavyohitaji ili uongoze Bunge na kuunda serikali ni viti 201 (Seats needed for a majority). Katika uchaguzi huu kumekuwa na mivutano mikali huku wagombea wanne wakionesha mchuano mkali katika kuhakikisha wanalidhibiti bunge la taifa hilo lilopo jijini Cape Town.

Wagombea wenye ushawishi Katika uchaguzi huu ni wanne lakini Kati ya hao ni wawili tu ambao wametajwa kufanya vizuri mpaka sasa kuelekea kwenye ushindi katika uchaguzi huu ambao ni Cyril Ramaphosa kutoka chama cha ANC na Julius Malema wa chama cha EFF. Hata hivyo tofauti na chaguzi zingine zilizo pita bado uchaguzi huu umeonekana kutawaliwa na suala la aridhi huku uludishwaji wa aridhi kwa wazawa likitawala majukwaa.

Wagombea 27 wanao shiriki katika uchaguzi huu ni wagombea wanne wanaotazamwa kulitawala bunge la SOZA la Afrika kusini, wagombea hao ni pamoja na;

CYRIL RAMAPHOSA, Mgombea huyu anatoka chama tawala cha AFRICAN NATIONAL CONGRESS (ANC), alichukua madaraka ya uraisi mapema mwaka jana kutoka kwa mtangulizi wake Jacob Zuma. Uchaguzi uliopita wa 2014 chama chake kilipata asilimia 62.15% ya kura, viti vya ubunge ilipata viti 249, na Ndio Rais wa Afrika Kusini kwa sasa.

MMUSI MAIMANE, Mgombea huyu anatoka chama cha DEMOCRATIC ALLIANCE (DA). Uchaguzi uliopita alipata Kura 22.23%, viti vya ubunge 89 hivyo anahitaji viti 112 kufikia viti 201 ili waongoze Bunge.

JULIUS MALEMA, Huyu anatoka chama cha ECONOMIC FREEDOM FIGHTERS (EFF). Uchaguzi uliopita alipata Kura 6.35%, viti vya ubunge 25 hivyo anahitaji viti 176 kufikia viti 201 walikamate Bunge.

MANGOSUTHU BUTHELEZI, huyu anatoka chama cha INKATHA FREEDOM PARTY (IFP). uchaguzi uliopita alipata Kura 2.40%, viti vya ubunge 10, anahitaji viti 191 kufikia 201ili aliweke Bunge kwenye himaya yake. Kiongozi huyu kinachomponza ni kuwakifu wapiga Kura baada ya kuongoza chama kwa Muda mrefu bila mafanikio ameanza kuingoza IFP tangu Tr. 21 Machi, 1975.

Baada ya kutazama kwa ufupi hali ya mambo katika uchaguzi huu utakao fanyika Mei 8.2019 huko Afrika kusini, sasa turejee kwenye maudhui ya makala hii ya leo juu ya chama cha EFF na ukombozi mpya wa raia wa Afrika kusini.

Turudi mpaka mtaa wa "78 De Korte Street, kiunga cha Braamfontein, jijini Johannesburg" yaliyopo makao makuu ya chama cha EFF (Economic freedom fighter)...

EFF ndio chama cha mfano kwangu (role model) katika vyama vya siasa barani Afrika, ni chama chenye maudhui ya maswala yawahusuayo walalahoi wa Afrika, ni chama kilicho beba ajenda ya ukombozi wa kweli kwa mwafrika ile iliyopiganiwa miaka ya 1950-1975 na wapigania uhuru wa Kweli Afrika. Aina ya siasa yao katika bara zima la Afrika inagusa ndoto za Mtu mweusi anaye ishi chini ya minyororo na ukaliwaji wa makabwela na mabeberu wasio jali maudhui ya uhuru na ukombozi wa bara la Afrika.

EFF, ni chama kilichobeba sura ya Vijana wazalendo wa Afrika Kusini wakiongozwa na JULIUS MALEMA (President,CIC), FLOYD SHIVAMBU (Deputy President), DALI MPOFU (National Chairperson), GODRICH GARDEE (Katibu Mkuu,GS), na Msemaji wa Chama Taifa (National Spokesperson) MBUYISENI NDLOZI. Vijana hawa wameamua kujitoa kupigania Taifa lao la Afrika kusini dhidi ya utawala mbovu unao kiuka shabaha ya ukombozi wa kweli (freedom charter) ambao ulipiganiwa kwa miaka mingi na waasisi wa taifa hilo wakina Criss Han, Robert Sobukwe, Visan Dube, Nelson Mandela, Oliver Thambo, Steven Bantu Biko, Govan Mbeki, Walter Sisulu, na wengine wengi.

Mpaka uchaguzi huu EFF ndio chama cha Siasa cha tatu kwa Ukubwa nyuma ya Vyama Vikongwe DA(Democratic Alliance) na ANC(African National Congress) ambacho ni Chama cha Siasa kikongwe zaidi nchini Afrika Kusini.

EFF kiliundwa Tarehe 28/7/2013.Miaka sita (6) iliyopita,chini ya Rais na Amiri Jeshi mkuu(President and Commander In Chief,CIC) Comrade JULIUS SELLO MALEMA,Alimaarufu kama JUJU na Viongozi wengine kadhaa waliokihama Chama kikongwe cha ANC.

CIC,JULIUS MALEMA alikua Kiongozi wa Tawi la Vijana la ANC Kitaifa,ANC-Youth League mpaka alipojitoa ANC na Kuunda Chama Kipya cha Siasa EFF mwaka 2013 Baada ya kutofautiana na Rais wa wakati huo JACOB ZUMA na wana ANC wengine alipoonekana ni tishio kwa Rais ZUMA na wana ANC wengine kama Makamu Rais wa wakati huo CYRIL RAMAPHOSA (ambae ndie rais wa sasa wa taifa hilo), kwani alihatarisha nafasi zao Siku za usoni alipoonekana kujijengea uungwaji mkono mkubwa ndani na nje ya Chana hicho.

EFF ni Chama kilichopata Uungwaji mkono mkubwa ndani ya Muda mfupi,Kwani katika Uchaguzi mkuu wa Afrika Kusini mwaka 2014, mwaka mmoja tu tangu kuundwa kwake kilikua tishio kwa ANC na DA, kwani katika Uchaguzi mkuu ule kilipata viti vya UBUNGE Ishirini na tano(25) kikiwa nyuma ya ANC na DA kwa wingi wa Wabunge Bungeni.

Pamoja na Kuwa na na Wabunge 25 kati ya Wabunge 400 wa Bunge la Afrika Kusini, EFF na Wabunge wametikisa Bunge la Afrika Kusini na Serikali ya ANC. kwa kuendesha Vuguvugu mbalimbali kama vile "ZUMA must fall", "Guptas must Go", "Marikana massacre movement" pamoja na "Nkhandra scander (Nkandla)". Vuguvugu zote hizi zilikuwa ni kampeni dhidi ya Ubadhilifu wa Rais zuma.

Mfano Katika tuhuma ya Nkandla Zuma alishutumiwa kujenga makazi Binafsi NKANDLA Kwa Zulu Natal kwa pesa ya Umma, Pia Mauaji ya Wachimbaji wa Mgodi wa MARIKANA zaidi ya 30 waliopigwa Risasi na Polisi chini ya Maelekezo ya Makamu wa rais wakati huo ndugu CYRILL RAMAPHOSA na Kufunguliwa kwa Kesi dhidi ya Rais Zuma katika Mahakama ya kikatiba "Constitutional Court" dhidi ya Matumizi mabaya ya fedha za umma kujenga Makazi binafsi kule Nkandla-KZN ambapo Mahakama ya kikatiba ilimwamuru Rais ZUMA kurejesha Fedha za Umma zilizotumika kujenga makazi yake Binafsi kule Nkandla kijijini kwake.

EFF inainyima usingizi ANC, na DA pia. Chama hiki cha EFF imejikita kutetea maslahi ya Masikini wa Afrika Kusini hasa Weusi walio wengi wanaoishi kama Wakimbizi katika Nchi yao, kwa kukosa ARDHI,AJIRA,ELIMU,Huduma za Afya,Nishati n.k kwani Maeneo yote yanayokaliwa na Waafrika walio wengi (Predominantly Black) mfano SOWETO kuna Umasikini wa Kutupwa na ufukura wa kunuka.EFF ni Chama kilichojipambanua kua Chama cha mrengo wa kushoto (Far-Left),Kinachoamini ktk Ujamaa,U marxi-U lenin(Marxist-Leninist),Umajumui wa Afrika(Pan-Africanism),U-Sankara(Sankarism) kikiongozwa na misingi ya Ujamaa na Umajumui wa Afrika uliopiganiwa na Wana wa Afrika kama KWAME NKRUMAH,PATRICE EMERY LUMUMBA,THOMAS SANKARA,SAMORA MOISES MACHEL,Mwl.J.K NYERERE na AHMED SEKOU TOURE.

Katika kapeni za uchaguzi huu EFF kilijielekeza zaidi katika siasa za kurejesha aridhi bila fidia kutoka mikononi mwa walowezi, pia ilitoa mwelekeo wa kumaliza tatizo la ajira nchini humo kwa kuwashutumu ANC kuinjinia mgogoro wa chuki wa xenophobia ili kujivua kulaumiwa na wananchi wa taifa hilo kwakuwa wameshindwa kutatua tatizo la ajira la taifa hilo. Malema alieleza kuwa kuwaondoa wageni wa kiafrika sio solution ya tatizo la ajira nchini humo.

EFF Chama chenye Umri wa Miaka 6 kinatarajiwa kufanya Vizuri sana katika uchaguzi huu,Kwani tangu kuzinduliwa kwa kampeni Miezi mitatu iliyopita, EFF imepata Uungwaji mkono mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika siasa za upinzani nchini humo.

Tangu Siku walipozindua Kampeni zao kwenye uwanja wa Orlando Stadium uliopo Katika eneo la "SOWETO" eneo la kwanza lenye wakazi wengi masikini Afrika na la pili duniani kuwa eneo kubwa zaidi linalokaliwa na watu masikini wa kutupa. Mpaka leo tarehe 5/5/2019, mitaa yote ya jiji kubwa la kibiashara la Johanasbug imefungwa kufatia kufulika kwa watu kushuhudia chama cha EFF kikifunga kampeni zake Katika uwanja wa Orlando uliopo Eneo la Soweto. Jambo hili katika kuhitimisha kampeni yao kuelekea uchaguzi hapo jumatano wameonesha Wana Nafasi ya kufanya mageuzi makubwa katika Siasa za Afrika Kusini hasa katika uchaguzi huu.


Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
FB_IMG_1557208956117.jpeg
 
Unapata wapi uhalali wa kumuita JULİUS MALEMA, president and CİC wakati bado hajapigiwa kura? Siku ANC wakishinda njoo hapa useme kura zimeibwa maana hamkawii kusema Tume ya uchaguzi, polisi ni vya ANC
 
Ajabu ya Tanzania..sidhani hao was SA wanmuda wa kujadili siasa zetu achilia mbali tu ya kumjua mtu kama zitto.tundu lissu au polepole..tunafeli wapi watanzania ???
 
Mungu saidia malema ashinde....binafsi naamini ushindi wa malema kwa kiasi kikubwa utabadili mwelekeo wa siasa za kiafrica, yaani kutoka kuhodhiwa na wazee mpaka kuhamia kwa vijana
 
Back
Top Bottom