Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
Ninapendekeza ili kuruhusu haki kutendeka kwenye matokeo ya kuhesabu kura katika chaguzi za nchi yetu, serikali ipeleke Bungeni kwa hati ya dharura kuomba mabadiliko ya sheria ili kuondoa jukumu la kuhesabu kura toka NEC na kuhamishia jukumu hilo NECTA na majukumu mengine ya uchaguzi hadi kutangaza matokeo yabaki kuwa chini ya NEC.
NECTA ambayo sasa hivi inaongoza Afrika kwa mfumo imara wa kuratibu mitihani inao uwezo wa kitaalam, kiufundi, kiusalama, kiteknolojia kuratibu uhesabuji wa kura bila dosari yoyote na bila kuingiliwa na mtu au mamlaka yoyote ile kama inavyofanya kwenye utungaji mitihani, usimamizi wake, usahihishaji wake, utoaji alama na utangazaji matokeo. NEC izuiliwe na sheria kuingilia zoezi la uhesabuji kura utakaofanywa na NECTA na ikiwezekana hata matokeo yatangazwe na NEC kwenye uwepo wa NECTA kama shahidi. Chaguzi za ndani ya vyama pia zinaweza kufanyika kwa mfumo huu wa uhesabuji kura ili kupata wagombea wenye sifa ambao hawatokani na matokeo ya kuhesabu kura zilizohujumiwa.
Kura zikihesabiwa kwa mikono. Taswira kwa hisani ya google.