Uchaguzi mkuu 2020: Tundu Lissu (CHADEMA) dhidi ya Benard Membe (CCM), hapatatosha !

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,386
217,470
Kuna haja ya Watanzania kuanza kuwafuatilia mapema wagombea wa vyama vya siasa wanaotajwa kupeperusha bendera kwenye uchaguzi mkuu , hii ni muhimu sana kwa vile hutoa nafasi ya kuwajua kiundani wagombea wetu wanaotarajiwa kubeba jukumu la kuongoza nchi yetu iliyokumbwa na changamoto ya kidemokrasia , ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kukongoroka kiuchumi mithili ya ng'ombe mwenye watoto mapacha aliyekosa malisho

Wadadisi wanauangalia uchaguzi wa 2020 kama uchaguzi utakaoacha bumbuwazi kutokana na aina ya wagombea wanatajwa kupeperusha bendera za vyama vyao , Benard Membe ambaye ni mbabe wa diplomasia ya kimataifa anatajwa kupeperusha bendera ya ccm kwa almost 75%, huku wapinzani wakijiapiza kumpa nafasi Tundu Lissu ambaye ni mbabe wa Utawala wa Sheria anayejikita zaidi kuheshimu Katiba ya nchi na uhuru wa kujieleza .

Zipo taarifa pia za jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha Uchaguzi unakuwa huru na haki kuanzia kwenye kampeni hadi ndani ya sanduku la kura , Je kuna wa kumzuia Lissu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom