HORSE POWER
JF-Expert Member
- Feb 22, 2015
- 2,067
- 1,386
Habari zenu wanaJF,
Kama ilivyo ada kwa mujibu wa Katiba yetu, mwaka huu pia kutakua na Uchaguzi Mkuu hapo mwezi Octoba.Ni fursa kwa wananchi kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani.Ni katka harakati hizi za kusaka 'uheshimiwa' tutashuhudia minyukano, kejeli, matusi, vitisho n.k.
Lakini pia tutashuhudia pia wale wanasiasa wachovu na wasio jiamini wakigawa rushwa kama peremende hasa majimboni na katani.Wapo watakaohonga khanga, vitenge, ubwabwa, tshirt n.k.Lakini kuna wale watakaoenda mbali zaidi hapo.
Hawa watajiongeza maradufu maana wataona Mwenyezi Mungu hatoshi kuwafanikishia malengo yao hivyo watahamia kwa 'waona mbali' ili mambo yawe mepesi.
Wanasiasa hawa waliofilisika sera, hoja, maono na ushawishi, matumaini yao watayahamishia kwa hawa 'waona mbali' ambao wengi wao ni waganga washirikina.Huko tena makafara ya ajabu ajabu yatafanyika na mahela yatatapanywa.
Yatapishana mashangingi huko kutafuta madaraka na ulaji.Kwa hakika ni msimu mnono na kabambe kwa hawa waganga washirikina...!!
"Na atakayemfanya shetani ndiye kiongozimsaidizi wake, hakika amepata hasara iliyokuwa wazi."
Sent using Jamii Forums mobile app