Uchaguzi mkuu 2020 Magufuli atapita bila kupingwa

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,812
Kwa kasi hii aliyonayo mambo yafuatayo yamedhihirika.1. Upinzani umeishiwa hoja...umeishiwa watu na umejikatia tamaa.2. Utendaji wake mahiri wa kazi umewapa wananchi imani kubwa kwake kwamba hili ni jembe ulaya tulilolihitaji miaka mingi sasa tumelinyaka....ataongoza nchi hii hadi yeye aseme sasa basi..3. Suala la majibu sasa linatarajiwa kuanza rasmi..hii iliyopita ilikuwa ni trela.long live Mzee wa Chato..siijutii kura yangu hata chembe.. majipu ptuuuu
 
never in tanzania.

ategemee utendaji wake katika miaka mitano hii aliyopewa ndio mtaji wake.

akumbuke rate ya ignorance kwa watanzania inashuka kwa kasi sana na hivyo asiishie tu kwenye kutumbua majipu bali kufikia 2020 impact iwe imeonekana katika maisha ya watu mmoja mmoja au kwa makundi yao.

ushindani utakuwa mkubwa kwa maana mwanzoni ameweka matumaini ya watanzania kuwa juu sana na hivyo ni rahisi sana kupoteza trust ya watanzania. watanzania hawa hawatabaki kusikiliza habari za nani katumbuliwa tu bali wanataka kuona baada ya majipu kutumbuliwa je miili yao imeacha kuumia au majipu yametumbuliwa na maumivu yamebaki palepale?

atambue kipindi cha sasa ni cha mpito kutoka katika siasa za uongo na kwenda katika siasa za kusema ukweli, siasa za mikakati ya kweli, siasa za ahadi za kweli.

walionyamaza si wapinzani tu bali wanasiasa waliokuwa kwenye ulingo wa siasa kwa sasa wako kimya maana upepo wa siasa umebadilika na mitaji yao haifanyi kazi. ni sawa na kuwa na bidhaa umerundika dukani alafu bidhaa hizo zinaonekana hazifai hivyo unabaki na bidhaa zako.

tatizo la wapinzani wamebaki kugangania milango iliyofunga ya kuuza majina ya watu na sio kuibuka na mikakati ya kutatua shida za wananchi, wamebaki kutafuta fitina bila kujua wananchi sasa wanaangalia ukweli, wamebaki kutafuta hoja moja moja kuikomalia kumbe wananchi kwa sasa wanasikiliza hoja pana za kila sekita kuhusu taifa zima. ukija na hoja yako moja wakati wao kila siku wanategemea habari mpya wanakuchoka.

lakini changamoto ndio mtaji wa maendeleo. hakuna mwanadamu angevumbua mwavuli kama mwanadamu huyo asingenyeshewa na mvua.

ki mtizamo wangu siasa zitabadilika na kufikia mwaka 2020 raisi atapata upinzani mkubwa katika siasa hizi ambazo ninaweza kusema kaziasisi.

atakuwa na mtaji mkubwa kama atafanya vizuri mpaka kwa mwananchi katika maisha yake lakini atambue 2020 tutegemee ushindani mkubwa.

mtaji wake katika yale atakayoyafanya vizuri ajue kwa yale atakayoshindwa ndio utakuwa mtaji wa kuanzia wa washindani wake. lakini wananchi wawe makini kuwa siasa za kutafuta kumkwamisha katika yale anayoyafanya leo ili 2020 iwe ni mtaji ni siasa za kihuni ambazo kamwe taifa halitakiwi kulea.

wananchi wafuatilie siasa kwa makini na waone yanayotendeka na kujua ni watu wa aina gani wanatakiwa kuwa viongozi wao. wawasikilize walioko nje na kupima kama malengo yao ni kukwamisha ua kutaka wananchi wapate maendeleo na huko mbele wafanye maamuzi.

raisi wa sasa anaweza kuwa mzuri lakini haimaniishi kuwa hawawezi kupata mzuri zaidi yake. wakati wa uchaguzi si wakati wa kulipa fadhila hivyo wajiandae kuchagua chaguo lilobora kwa wakati wote.

kama katika wataojitokeza ndiye bado ataonekana kuwa bora basi watakuwa na haki ya kumrudisha lakini kama wataona wanaweza kupata kiongozi bora zaidi wasisite na sio kwa kubeza juhudi zake bali kama kocha anavyoona mchezaji uwanjani amefanya kazi kubwa wakati mwingine huamua kumpumzisha na kuweka nguvu mpya ili timu isianze kupoteza bali iendelee kucheza kwa kiwango kilekile.

Kwa kasi hii aliyonayo mambo yafuatayo yamedhihirika.1. Upinzani umeishiwa hoja...umeishiwa watu na umejikatia tamaa.2. Utendaji wake mahiri wa kazi umewapa wananchi imani kubwa kwake kwamba hili ni jembe ulaya tulilolihitaji miaka mingi sasa tumelinyaka....ataongoza nchi hii hadi yeye aseme sasa basi..3. Suala la majibu sasa linatarajiwa kuanza rasmi..hii iliyopita ilikuwa ni trela.long live Mzee wa Chato..siijutii kura yangu hata chembe.. majipu ptuuuu
 
Hakuna Mfano,Mh.Raisi wangu usiwaangalie Usoni wamekula hawa hadi na wapambe wao wanaokuja JF kukukatisha Tamaa Rudisha Nchi kwenye Reli Mheshimiwa Una SAPOTI ya WANANCHI WANYONGE Tunakuombea USHINDE VITA HII

Mimi kinachonishangaza ni kwamba huyu mh.simuelewi anayepokea mshahara mkubwa anamchukia na ambaye amejitolea kutokupokea kabisa naye kwake ni tatizo,sijui anahitaji nini huyu mzee!
 
Nchi hii! Mbona ina raia wajinga kiasi hiki? Unampimaje mtawala kwa miezi sita na kutabiri yatakayotokea miezi hamsini + mbele.Acheni kutoa tatmini kwa mpenzi kwani ni upofu na ujinga.Ukweli mchungu ni kuwa watakaomtoa madarakani JPM ni chama tawala wenyewe anamwaga ugali wao saa hizi watamwaga mboga.Lowasa alikuwa na Nguvu na watu Sembuse yeye!
 
naona pumba tu humu.
-wiki chache zilizopita-hatuhitaji sukari kutoka nje kwa sababu tuliyonayo inatosha-rais Magufuli
-siku chache zilizopita-tuna upungufu wa tani 100 za sukari na tumeagiza kutoka nje-pm Majaliwa.
kama uko karibu naye mwambie awe makini sana na hao washauri wake. wengine wanampango wa kumharibia kuliko kuja kupoteza muda hapa kumsifia wakati kila mmoja anaona kinachotokea.
miaka 5 sio mingi. awe makini sana ukizingatia tofauti yake na mpinzani wa karibu ni kura chache tu.
urais wa Tanzania ni 10 years max. hatuhitaji usultan.
 
Kwa kasi hii aliyonayo mambo yafuatayo yamedhihirika.1. Upinzani umeishiwa hoja...umeishiwa watu na umejikatia tamaa.2. Utendaji wake mahiri wa kazi umewapa wananchi imani kubwa kwake kwamba hili ni jembe ulaya tulilolihitaji miaka mingi sasa tumelinyaka....ataongoza nchi hii hadi yeye aseme sasa basi..3. Suala la majibu sasa linatarajiwa kuanza rasmi..hii iliyopita ilikuwa ni trela.long live Mzee wa Chato..siijutii kura yangu hata chembe.. majipu ptuuuu
Hakuna cha ajabu hapo, kwa hapa Tanzania chochote chawezekana...hivi hujui genge la wezi, CCM, nalo limeapa kutoachia madaraka hata kwa miaka 100? Huko Zanzibar nako hujui Shein anaiongoza Zanzibar hadi aseme sasa basi? Sasa kitu gani kitamzuia Pombe asitawale mpaka atakapochoka?

Kwa ufahamisho wako ujue jinsi kuletwa kwa kivuko cha Bagamoyo, MV Dar es Salaam, kilivyosaidia kupunguza tatizo la foleni mjini Dar es Salaam. Nyumba za serikali nazo hazirudi ng'o, CCM mbele kwa mbeleee! Wewe unadhani hayo magari 700 ya polisi yaliletwa kwa shughuli gani?
 
Leta mchango wa mawazo wa kuendeleza nchi huu sio wakati wa kampeni, ebo!!! Ni ujinga uliopitiliza kuwaza kampeni wakati huu. matokeo yake nchi kuwa kwenye kampeni kwa muda wa miaka mitano. Kama umetumwa, kafie mbali na mawazo yako ya hovyo hovyo
 
Sawa mwambie sasa ni muda wa kuwa na tume huru ya uchaguzi kabla ya uchaguzi
 
Mimi kinachonishangaza ni kwamba huyu mh.simuelewi anayepokea mshahara mkubwa anamchukia na ambaye amejitolea kutokupokea kabisa naye kwake ni tatizo,sijui anahitaji nini huyu mzee!
Uwe mdadisi wa mambo ili uweze kuishi vizuri. Hebu fuatilia vizuri ujue ni kwa nini bosi wa TIC katumbuliwa. Jiulize, kama alikuwa hapokei mshahara, alikuwa anaishije?
 
Rais wetu mpendwa alipoingia madarakan sukari ilikua 2200 sasa hv imefika 2600, ama kwa hakika rais wetu aendelew kutawala tu sisi tunafurahia majipu kuliko uhalisia wa maisha ya mtaani
 
Pia kishasema kwamba kupatikana kwa katiba mpya ambayo itatuletea Tume huru ya uchaguzi si kipaumbele chake kwa kuwa anajua fika kwamba kutafanywa wizi wa hali ya juu wa kura na pia hii Tume ya CCM ya uchaguzi kuhusika katika kupindisha tena matokeo ya uchaguzi kama ilivyokuwa 2005, 2010 na 2015. Kiongozi ambaye ana mapenzi ya kweli na nchi yake na kujali maslahi ya nchi na raia wake kamwe hawezi kukubali kuona matatizo makubwa yanayosababishwa na chaguzi zetu nchini miaka nenda miaka rudi lazima atasimama kidete ili kuhakikisha hali hii inakomeshwa na hivyo kutojirudia tena katika chaguzi za siku za usoni, lakini yule ambaye anajali maslahi ya chama chake na maslahi yake binafsi basi hili la kupatikana katiba mpya kamwe haliwezi kuwa kipaumbele chake.

Hakuna cha ajabu hapo, kwa hapa Tanzania chochote chawezekana...hivi hujui genge la wezi, CCM, nalo limeapa kutoachia madaraka hata kwa miaka 100? Huko Zanzibar nako hujui Shein anaiongoza Zanzibar hadi aseme sasa basi? Sasa kitu gani kitamzuia Pombe asitawale mpaka atakapochoka?

Kwa ufahamisho wako ujue jinsi kuletwa kwa kivuko cha Bagamoyo, MV Dar es Salaam, kilivyosaidia kupunguza tatizo la foleni mjini Dar es Salaam. Nyumba za serikali nazo hazirudi ng'o, CCM mbele kwa mbeleee! Wewe unadhani hayo magari 700 ya polisi yaliletwa kwa shughuli gani?
 
ataongoza nchi hii hadi yeye aseme sasa basi..

okay,,.....kwamba atageuka kuwa Nkurunzinza...ati eeeehhhhh

Upinzani umeishiwa hoja...umeishiwa watu na umejikatia tamaa.

Hujui ukisemacho.....Hakuna jambo lolote la tofauti lililofanywa na serikali hadi sasa zaidi ya media stunts

Utendaji wake mahiri wa kazi umewapa wananchi imani kubwa kwake kwamba hili ni jembe ulaya tulilolihitaji miaka mingi sasa tumelinyaka....ataongoza nchi hii hadi yeye aseme sasa basi

Maisha yamezidi kuwa magumu...mfano bei ya sukari kwa sasa ni Sh 2800...Baadhi ya Supermarkets kama Nakumat wame restrict idadi ya kilo ambazo mteja mmoja anweza kununua.....ili wapate watu wengi....Inflation iko juu sana....hakuna creativity serikalini...watu wanafanya kazi kwa woga

siijutii kura yangu hata chembe.. majipu ptuuuu

Si muda mrefu kutoka sasa utakuwa mnyonge sana..Na Utaijutia sana kura yako...kwa sasa bado uko honeymoon
 
Nchi hii! Mbona ina raia wajinga kiasi hiki? Unampimaje mtawala kwa miezi sita na kutabiri yatakayotokea miezi hamsini + mbele.Acheni kutoa tatmini kwa mpenzi kwani ni upofu na ujinga.Ukweli mchungu ni kuwa watakaomtoa madarakani JPM ni chama tawala wenyewe anamwaga ugali wao saa hizi watamwaga mboga.Lowasa alikuwa na Nguvu na watu Sembuse yeye!
akili za kupinga ukweli ni akili za vipofu. na ikiwa kipofu atawaongoza vipofu wenzao mwisho wake ni mbaya.
 
Kwa kasi hii aliyonayo mambo yafuatayo yamedhihirika.1. Upinzani umeishiwa hoja...umeishiwa watu na umejikatia tamaa.2. Utendaji wake mahiri wa kazi umewapa wananchi imani kubwa kwake kwamba hili ni jembe ulaya tulilolihitaji miaka mingi sasa tumelinyaka....ataongoza nchi hii hadi yeye aseme sasa basi..3. Suala la majibu sasa linatarajiwa kuanza rasmi..hii iliyopita ilikuwa ni trela.long live Mzee wa Chato..siijutii kura yangu hata chembe.. majipu ptuuuu

NA NDIO MWENYE AKILI KUZIDI WOTE WALIOMO CCM,,,,, WENGI WAO WANAVICHWA VYA KUKU.
 
Ushafanya analysis mtaani ukasikia watu wa maisha ya kawaida kabisa wanasema nini kuhusu huyu jamaa? Je unaweza sema kuwa mwananchi wa maisha ya kawaida kabisa kanufaika vipi na hii tumbua chunusi inayoendelea, je imeshusha gharama za mkate wa kila siku? au umedanganywa na haya maigizo ya juzi ya 9%? Subiri ndugu, mwezi bado mchanga kutabiri sana kutabiri safari.
 
Back
Top Bottom