Uchaguzi mkuu 2020: Kila apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Tuna viongozi waliotokana na mchakato wa WIZI wa kura, tutavuna matunda yake...!!

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani/wawakilishi Tanzania ulifanyika tarehe 28/10/2020, umekwisha na kupita.
Hakuna mjadala kwa hili...

Mjadala ni umekwishaje na nini matokeo yake. Hapa ndipo ilipo ishu nzima na ndiyo msingi wa mjadala huu...

Watu wengine kwa midomo yao ama through social medias wanasema Magufuli na Tanzania kwa sasa ni maarufu sana duniani kwa tukio hili...

Yes. Labda yaweza kuwa ndivyo hivyo kweli. Swali ni hili:

Wanazungumzwa kwa umaarufu wa sifa zipi...?

Mwanamke malaya mjini anapozungumzwa sana na watu kila mtaa kwa sababu ya umalaya wake halafu akawa anashangilia kama zuzu kuwa sasa yeye ni maarufu mji mzima, huyo atakuwa mpumbavu...!

Je, washangiliaji wa Rais Magufuli na "Tanzania" kwa kuandikwa ama kuzungumzwa sana huko ktk mataifa ya nje kwa kuunajisi uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi jana ni UJUHA ama WEREVU...?

Kusema ukweli reaction ya taasisi za kimataifa, nchi wahisani na nchi washirika wetu wa kimaendeleo juu ya mchakato mzima wa uchaguzi uliopita na kumweka Magufuli (T) na Dr Mwinyi (Z) kama marais, umekuwa criticized sana kuwa haukuwa HURU na HAKI na ulijaa WIZI na UDANGANYIFU msingi...

Kwa ujumla huu haukuwa uchaguzi bali maigizo ya uchaguzi. Kila mtu huru na timamu aweza kushuhudia hili bila woga wala hofu na kwa ushahidi kamilifu...!

Baadhi ya taasisi hizi za kimataifa, mashirika haya kimataifa, nchi wa hisani na washirika wetu wa maendeleo wameshaanza michakato ya kufikiria hatua za kuichukulia Tanzania...

Hii ni pamoja na kusitisha ama kupunguza misaada ya kibajeti ama kuweka vikwazo vya kisiasa na kiuchumi kwa nchi yetu nk nk...

Hili si jambo jema hata kidogo. Hakuna anayeweza kushangilia na kufurahia hili bila shaka...

Lakini kwa upande mwingine, wana haki ya kufanya vile kwa sababu, kiongozi wa nchi yeyote anayeingia madarakani kwa nguvu bila kufuata njia za WAZI na HAKI za kidemokrasia tafsiri yake ni moja tu kuwa;..

Huyo si MWAMINIFU, huyo si MSAFI na huyo automatic ni MWIZI na FISADI kwa 100%...!

Katika hali hii, huwezi kushirikiana na taifa lenye kiongozi mwenye sifa hizi na kamwe huwezi kutoa fedha za walipa kodi wa nchi yako wanaojinyima kuwasaidia wenzao wa nchi nyingine zenye uhitaji ukitambua kuwa zitaishia kwenye mifuko ya viongozi walafi na wenye tamaa ya ubinafai na wasiojali utu wa binadamu...!!

Sasa watawala hawa kupitia kwa mawakala wao wanaanza kujinasibu kuwa, shida haipo kwa sababu tunaweza kusimama wenyewe...

Hata ingekuwa, kusimama mwenyewe haina maana kuwa hutahitaji mahusiano na dunia....

Na kusema kweli ishu hapa siyo siyo fedha. Kupata msaada wa kifedha au vitu toka kwa rafiki ni matokeo ya uhusiano mzuri mlionao na rafiki huyo. Hiki ndicho kinachotafutwa na nchi ama mtu yeyote...

Tanzania ni nchi miongoni mwa nchi nyingi duniani. Hatuwezi kuwa peke yetu baada ya kutengwa na jumuiya ya kimataifa...

Kwa hiyo tunapaswa kwa kila hali kuhakikisha kuwa mahusiano yetu na mataifa mengine yanakuwa imara...

Tusikubali viongozi wachache wenye tamaa zao za madaraka kuumiza mamilioni ya watanzania kwa sababu zao za tamaa ya madaraka tu...

Si hivyo, baada ya mwitikio hasi wa jumuiya ya kimataifa juu mchakato mzima wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu kugubikwa na udanganyifu na wizi wa kura, hawa walioshinda kwa wizi wa kura wanaanza kulia lia na kututaka tushikamane nao baada ya kunusa dalili mbaya kwao...

Mimi binafsi nasema, siwezi kushikamana na uovu. Siwezi kushikamana na viongozi wa nchi wezi...

Maana kiongozi aliyepata uongozi kwa njia haramu zsma wizi wa kura, atashindwa nini kuyalinda madaraka ya uongozi wake hata kwa gharama ya damu za watu yaani kuwapoteza ama kuwaua wanaomkosoa...?

Laiti jumuiya ya kimataifa ingekuwa inatuonea tu sisi Tanzania kama nchi na kuwa kila kitu kiko na kimeenda sawasawa, hakika tungeshikamana kupambana nao...

Lakini ukweli ni kwamba, hiki kinachotokea ni matokeo ya UJINGA, UPUMBAVU na TAMAA na UBINAFSI wa nafsi za hawa wanaotulazimisha tuwakubali na kuwaita viongozi wetu...!

Kila dhambi atendayo mtu, atalipwa kwayo. Na kila kile mtu apandacho, ndicho atachokivuna...

Huwezi kupanda UOVU utegemee kuvuna matunda ya WEMA...!!
 
Kumbe Mr Mzungu alivuna alichopanda, alipokataliwa kwenye ballot box hatimaye kusepa zake, baada ya kufurumusha "me-two-sea" weee, uongo sana, uzushi kibao, chuki na kupinga "killer-key-two" mwanzo mwisho kwenye kampeni zake, badala ya kunadi sera na kutunza amani & mshikamano wa kitaifa???
 
JIWE NI MPUMBAVU SANA AMEHARIBU TUNU ZA TAIFA LETU.

Tuliheshimika sana Duniani.
Tulipendwa sana Duniani.
Tuliaminiwa sana Duniani.
Tulithaminiwa sana Duniani.

Ameharibu kabisa ndoto za Waasisi wa nchi kwa kujiona ana akili nyingi wakati hata HATA KUTUNGA SENTENSI MOJA YA KIINGELEZA HAWEZI.
 
JIWE NI MPUMBAVU SANA AMEHARIBU TUNU ZA TAIFA LETU.

Tuliheshimika sana Duniani.
Tulipendwa sana Duniani.
Tuliaminiwa sana Duniani.
Tulithaminiwa sana Duniani.

Ameharibu kabisa ndoto za Waasisi wa nchi kwa kujiona ana akili nyingi wakati hata HATA KUTUNGA SENTENSI MOJA YA KIINGELEZA HAWEZI.
Uliheshimika, ulipendwa, uliaminiwa kwa sababu rasilimali zilikuwa zinasombwa na hao mabeberu zako wakati nchi ikiendelea kuwa maskini. Nasema JPM aendelee KUKAZA hiyo kamba ya chuma hadi waondoke hao walafi wote na makuwadi wao.
 
Uliheshimika, ulipendwa, uliaminiwa kwa sababu rasilimali zilikuwa zinasombwa na hao mabeberu zako wakati nchi ikiendelea kuwa maskini. Nasema JPM aendelee KUKAZA hiyo kamba ya chuma hadi waondoke hao walafi wote na makuwadi wao.
Uko zamu leo ndugu Mataga?
 
Back
Top Bottom