Uchaguzi Mkuu 2015

Paw

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
2,113
2,000
JF imekuwa sehemu salama na sahihi kwa watu wengi wanaoitembelea kwa makusudio mbalimbali yakiwemo Kupata taarifa mbalimbali na hata kushirikisha jamii taarifa mbalimbali....

Pamoja na kwamba katika wengi hakukosekani mengi, lakini mara zote JF imekuwa mahala sahihi na chaguo la wengi.

Neno langu ni moja tu.

Siku ya Jumapili tarehe 25/10/2015 Taifa la Tanzania litapitia katika mtambuka wa kutafuta kiongozi mpya wa taifa hili kupitia sanduku la kura. Mikakati ni mingi, miradi ni mingi na hata kupitia vinywa vya wahusika wengi tumesikia mambo mengi sana. Hivyo niwaombe bila kujali itikadi za kila mmoja wetu. Tusimame kuiombea AMANI Tanzania. Sababu za kuleta ombi hili kwenu ni kwa sababu zifuatazo

  • Matamko na matendo yanayohatarisha utulivu na amani ya nchi kipindi cha uchaguzi
  • Kupitia midomo ya wanasiasa wameonyesha kuhamasisha wanaowaunga mkono kufanya kile wakitakacho hata kama kinaweza kuleta dosari katika amani ya nchi.
  • Waathirika wakubwa wa matukio ya uvunjwaji wa amani siyo wavunja amani bali wanawake, watoto, wazee na wasiojiweza....
Nina imani kubwa kwamba inawezekana uchaguzi ukafanyika kwa amani ila tulithibitishe hilo kupitia sala na maombi yetu.

Tuiombee nchi
Tuiombee Tanzania
Tudumishe amani

Kuna maisha baada ya uchaguzi
========================================

NB
Sijaweka hili bandiko kwa niaba ya JF
 
dolevaby

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
10,703
2,000
AMANI haiombewi AMANI ni TUNDA la HAKI kila mmoja atimize wajibu wake
 
Madenge Origino

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,794
2,000
JF imekuwa sehemu salama na sahihi kwa watu wengi wanaoitembelea kwa makusudio mbalimbali yakiwemo Kupata taarifa mbalimbali na hata kushirikisha jamii taarifa mbalimbali....

Pamoja na kwamba katika wengi hakukosekani mengi, lakini mara zote JF imekuwa mahala sahihi na chaguo la wengi.

Neno langu ni moja tu.

Siku ya Jumapili tarehe 25/10/2015 Taifa la Tanzania litapitia katika mtambuka wa kutafuta kiongozi mpya wa taifa hili kupitia sanduku la kura. Mikakati ni mingi, miradi ni mingi na hata kupitia vinywa vya wahusika wengi tumesikia mambo mengi sana. Hivyo niwaombe bila kujali itikadi za kila mmoja wetu. Tusimame kuiombea AMANI Tanzania. Sababu za kuleta ombi hili kwenu ni kwa sababu zifuatazo

  • Matamko na matendo yanayohatarisha utulivu na amani ya nchi kipindi cha uchaguzi
  • Kupitia midomo ya wanasiasa wameonyesha kuhamasisha wanaowaunga mkono kufanya kile wakitakacho hata kama kinaweza kuleta dosari katika amani ya nchi.
  • Waathirika wakubwa wa matukio ya uvunjwaji wa amani siyo wavunja amani bali wanawake, watoto, wazee na wasiojiweza....
Nina imani kubwa kwamba inawezekana uchaguzi ukafanyika kwa amani ila tulithibitishe hilo kupitia sala na maombi yetu.

Tuiombee nchi
Tuiombee Tanzania
Tudumishe amani

Kuna maisha baada ya uchaguzi

Katika hili la kudumisha AMANI basi bora JF itoe tamko rasmi kwa NEC la kuomba tuwe Uchaguzi HURU na HAKI. Kwani bila ya HAKI amani ya Tanzania itakuwa mashakani!
 
Njilembera

JF-Expert Member
May 10, 2008
1,464
2,000
Huyu mkabila sijui Mkamba, sijui Mmasai naye vipi! Mambo ya Mikasi au kichinjio mwisho ni kesho. Tusimame kama taifa!
Amani itadumu kama hatutatunishiana misuli. Haki ni neno sahihi, lakini unyenyekevu ni neno jema zaidi. Hakuna aliyezaliwa kumgandamiza mwenyewe, hakuna aliyezaliwa kurusha ngumi na mateke kwa mwingine. Kama maandiko yanavyonena, usimjibu akuchokozae wala usimrejeshee akupigaye kofi. Nawe usimtishe mwenzio asije akadhani anajihami kumbe ndio anashambulia.

Ninasali nikimwomba Mungu awajalie viongozi wangu na hasa Rais wangu JK, viongozi wa Jeshi la Polisi wawe wavumilivu, wawanyime askari wetu kile wanachovuta au kukinywa ambacho huwapa murari usio na kifani wanapolazimika kumzuia mwananchi aliyezidiwa raha/karaha. Waone yule ni binadamu na mhalifu atakayekuwa amesalimu amri basi asipigwe kama tulivyokwishaona huko nyuma. Kumpiga mateke, kumsukumia mitutu ya bunduki huamsha hasira ya wengine.
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,345
2,000
Waathirika wakubwa wa matukio ya uvunjwaji wa amani siyo wavunja amani bali wanawake, watoto, wazee na wasiojiweza....

Hao waliochangia uzi wako umewaona wanawake wangapi na wazee wangapi? Wa kulaumu hapa ni hao viongozi wetu wenye ncha mbili. Hawataki kuachia madaraka wanadhani wamezaliwa kuongoza milele.
Amani haiombwi hupokewa kwa moyo wa kukubali
 
Freeland

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
14,501

Amani ni Tunda la Haki.....Bila Haki hakuna amani
 
rpg

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
3,513
1,225
Ni muhimu polisi wakatimiza wajibu wao, waepushe fujo kwa kuheshimu haki za bi9nadamu.
 
Top Bottom